Mkate na kikombe cga Sayansi ya Kikristo |

Mkate na kikombe cga Sayansi ya Kikristo

Kutoka kwa kozi ya umungu na makala mbalimbali. { Kitabu cha samawati} Iliyoandikwa na Mary Baker Eddy, ukurasa 142 -143


Ushirikiano unaweza kuja tu kupitia kuzaliwa tena, kupitia ubatizo wa Roho, kama inavyofundishwa kupitia Sayansi ya Kikristo. Huu ubatizo wa moto huleta harufu ya kweli ya Mungu, ikiimarisha uwepo wa Mungu, uliopewa mtu kwa kuponya walio wagonjwa kwa njia ya wokovu kutoka kwa dhambi na ushindi dhidi ya hisia ya kifo na ufahamu uliozikwa na kufichua mfariji anaye elekeza kwenye amani. Hii ndio kula mkate. Ni nini mkate wa Sayansi ya Kikristo?

Ni nguvu na Chakula ambacho Mungu huwapatia walio na moyo wa kuzimia na hatua za kusuasua katika masaa mbaya ya udhaifu wa binadamu; ndio! Ile nguvu yeye hupatiana ambayo sisi hupata utambuzi wake – utambuzi ambao haueleweki na maarifa, lakini na moyo mnyenyekevu. Ni nini kikombe cha Sayansi ya Kikristo? Ni kikombe ambacho kinanywa katika dhiki. Ni furaha ya kusisimua , baada ya kushinda majaribu. Ni matunda ya mzabibu ambao Mungu ndiye mkulima. Ni kiwanda cha divai ambapo mbegu za dhambi lazima zitapondwa, na ambaye nyayo zilizochoka haziwezi ondoka mpaka kila mbegu iliyomo imepondwa – kwamba kutoka kwa kiini hiki Mungu atatengeneza kiumbe kipya, ambacho kitashuhudia juu yake kama Upendo unaoponya. Tumefichwa kama washirika wa kanisa hii kushiriki katika sakramenti kimya, na kuja kwa meza aliyotayarishwa kwa shukrani. Kwetu kumenenwa amri, ” Mtoto wangu, nipatie roho yako,” wakati ni yetu kujibu:

Nifanye utafiti ewe Mungu, na ujue roho yangu; Nijaribu na ujue mawazo yangu;

Na uangalie kama kuna njia mbaya ndani yangu.

Tunaitwa kujitolea kila siku, kila saa, kwenye madhabahu ya kujitoa ya utegemezi kamili kwa Mungu, tukiinuliwa kwa kila jaribio mbaya, tukifurahia kila ukame kutoka kwa kikombe kinachotufaa kuwa washiriki na Yesu kwa mateso yake na ushindi. Nguvu hii tumepewa katika kiwango sawa kama vile tunavyo karibisha hisia za Roho ambayo ilimuimarisha, na tunaingia kwenye ukamilifu wa udhihirisho kwa kuwa tuna Akili moja ambayo ilikuwa ndani ya Kristo Yesu.