Mahali
Imeandikwa na Mary Baker Eddy
Unachokitafuta kinakutafuta. Unachohitaji, kinakuhitaji. Mtakatifu Mungu analeta hitaji na ruzuku pamoja kwa faida ya wote.Mungu kwa busara, hekima na upendo anadhibiti, kuongoza, kulinda,kufanikisha na kubariki huu muungano wa wazo lake {mtu} na shughuli yake ya kawaida {kazi}.
Haichukui mda kujenga mahali pako ama kazi yako kwa sababu haiwezekani kuwa wazo lisiwe na mahali pake, na mahali pake pawe pamendelezwa kama wazo linalojaza pale. Mahali pale lazima pakidhi mahitaji yote ya wazo kama imepatianwa na Mungu.
Yale unayotakikana kufanya ni kuona ya kwamba ufahamu wako uko tayari kikamilifu, umepanuka,uko safi, umeinuliwa, umejaa furaha, unatarajia wema usio na mwisho na pasiwe na hisia za ukomo inayoweza zuia udhihirisho kamili wa mapenzi ya Mungu kwa wazo lake, na unajua kwamba mapenzi yake Mungu kwa wazo lake ni ukamilifu, hakuna lingine.
Tunayohitaji kubadilisha ni hisia za utatanishi kwa ufahamu wa mshikamano wa serikali takatifu.
Ni nani anasema “Nimemaliza kazi yangu hapa na lazima nitafute mahali kwingine?” Mungu peke ndiye huamrisha na kuelekeza.Hujui kama ni sawa kukaa hapa ama kuondoka, ila kwa hatua ambazo zinawekwa mbele yako siku kwa siku. Hata kama matamanio yetu iko sambamba na maendeleo, lazima tusalimu ubinafsi na mipango yote kabla kupiga hatua sawasawa
Hakuna mapenzi ya mtu na mipango, hakuna mipango ya kiasili kwa Mtukufu Mungu; kwa hivo hauna nguvu ama mwelekeo wa kudhihirisha uongo wa aina ile. Yote ni uvumilivu, utiifu ulio tulia,kwa sababu Mungu ni yeye pekee na kila mahali. Yote ni utulivu, upendo, umoja wa kisayansi. Mungu yuko pahali unapoishi. Simama imara na uwe na maono. Hakuna binadamu mkatili, hakuna ukatili, hakuna hasira,tamaa, uchovu, ukosefu wa haki, ujasiri wa kibinafsi pahali popote wa kujiwakilisha wenyewe; hakuna kujionyesha kwao katika mazingira yako. Hakuna madai kama hayo ya kuleta dhiki, kukandamiza, ama ya kukushikilia chini.” Uumbe wa Mungu ni wa milele, uhuru, umoja,na faraja isiyo na mipaka.”
{S&H}, na unaangaza Mungu. Kwa hivo fanya kazi ya ufahamu wa shughuli yenye umoja na uondoe hisia za utu, mtu mzuri ama mbaya na ujue unamtumikia Kristo Bwana, na ujue hakuna kitu kinachoweza kuzuia, kuchelewesha ama kuweka kipimo kilichoelekezwa na Mungu na kilicholindwa na Mungu na shughuli iliyowekwa na Mungu.
Hauwezi badilisha mazingira. Tunaweza tu badilisha hisia za mazingira na hatuweza fanya haya kwa njia yoyote ile ila kwa kuinua mawazo yetu kuhusu mambo yote. Mungu pekee ndiye mazingira. Lazima tuweke wazi maono yetu,tufagie takataka ya hofu,ukosefu wa subira na makadirio ya uongo kwa binadamu wenzetu na tujue ya kwamba Mungu hung’aa kupitia watu wote na anasimamia watu wote. Sio lazima upange, kufikiria namna, ama wakati gani ama wapi; hiyo ni kazi ya Mungu- kazi yako ni kung’aa kwa maakini, kusikiza na kutii mwito unapofika. Mapenzi ya Mungu kwa wazi hutuita kila wakati na kutuambia mapenzi yake Baba; lakini tunaegemea kujifanyia mambo kwa njia zetu wenyewe badala ya kujua yamefanyika tayari, na kwa wakati hatusikii vile Mungu anasema. Mapenzi ya Mungu yanajionyesha kwa busara na yatakidhi mahitaji yako kwa busara kwa kuangamiza hisia zako za uoga.
Kwa kweli hauna hitaji lolote kwa sababu umekamilika ndani ya Mungu. Mungu yuawaza na unaangaza mawazo yake. Mungu yuafanya kazi na hakuna lingine laweza. Mungu yu aeleza, kuelekeza na hakuna anayeweza kukomesha mkono wake ama kumwambia “Unafanya nini?” Mungu atakwambia vile utakavyofanya kuhusu kazi yako. Atafafanua kila hatua kwa hivyo usitie shaka ama uwe na wasiwasi ama bika subira. Ako na mema yasiyo na mwisho juu yako. Fanya hima uwe mpokevu. Tunapaswa tujue kwamba ukosefu wa maadili hauwezi tatanisha kuanguka kwa kanisa, familia ama urafiki.Tunatakiwa tujue kwamba Mtukufu Mungu anajenga na anashikamanisha na kufanikisha.
Mungu na sheria kamilifu ya marekebisho inayoendeshwa na sheria ya sasa ya mvuto inaleta kwako yote unayomiliki.
Gundua kwa ajili yako mwenyewe kila siku, zaidi ya mara moja, kwamba nyanda ni nyeupe na mazao; kwamba Mungu yeye amekidhi na hukidhi kwa wakati wote mahitaji ypte ya binadamu. {S&H} Hitaji la kazi na hitaji lingine lolote anakidhi. Mungu yu hai na unaangaza uhai; ya kua kazi ni nyingi kwa wote; na yako ni yako na hakuna mwingine anaeweza kuifanya na inakuja kwako moja kwa moja na ruzuku ni kubwa. NA UJUE KWA KILA WAKATI HALI IKO VILE. Kamwe usiwe na hisia ya ukosefu wa kitu chochote ukae ndani yako. Ni makosa na inaleta aina zote za magonjwa na changamoto chungu mzima. Mungu ni wingi na anakidhi tu wingi. Kuonyesha kwa haya ni wingi wa Mwanga, Upendo, Ukweli na hekima kwa mahitaji yetu yote. Weka lengo, fuata maandiko yako na uwe na imani kwa kuelewa kwako kwa Sayansi ya Kikristo.
Mahali: Kwanza lazima tujue kwamba Mungu na sio mwingine yuafanya kuweka. Paulo asema, “Kwa maana ndani yake tunaishi, tunatembea na tunao uumbe wetu.” Kujua hivi kwamba mtu , wazo la Mungu, ako mahali pake sahihi yafanya kazi ya uponyaji, kwani mahali pale pako ndani ya Mungu saa hii na kwa hivyo mahitaji yake yamekidhiwa na Mungu, Upendo. Kwa hivyo kuishi kwa ufahamu huu utaleta tunachohitaji kwa tajiriba ya binadamu, iwe ni nyumbani ama kitu chochote kingine kizuri, kwa sababu hali hii ya ufahamu inatenga wazo lolote mbaya, kama hukumu za kifo ama hali zilizojaa, ukosefu wa mahali pazuri, uoga, kukosa uamuzi, ukosefu na kadhalika, na inasababisha bila nguvu na batili, alafu ukweli wa uumbe waletwa kwenye mwangaza na unadhihirika kwa tajiriba ya umoja. Baada ya kuzirusha nyavu kwa upande wa kulia, unapata mahitaji yako yamekidhiwa. Kataa kukubali hukumu ya binadamu kama maoni yako, ama mawazo yako.
Jua kwamba mawazo yote yanatoka kwa Mungu na mawazo yote ya ukweli yanaondoa imani zote mbaya kuhusu mahali na kadhalika, na madhara yanayoonekana yanatokomea. Ni sawa kwako uwe na watu wa aina yako, na ukimwamini na roho yako yote, itafungua njia. Kumbuka ” Mungu ako na rasilimali isio pungua.” kwa hivo usijizuie kwa njia yoyote. Hakuna sheria ya matendo mabaya ya maovu kupitia hali yoyote inaweza zuia kwa wakati wowote kudhihirika kamili kwa mpango wa Mungu juu yako hapa na sasa.