Wazo lako mwenyewe
kilicoabdikwa na Richard Oaks
Hii Makala inasifiwa kuandikwa na Mary Baker Eddy na mmoja wa wanafunzi wake na inaweza patikana kwa kitabu Insha na nyayo zingine
Yeyote anayedhihaki mwenzake anapunguza thamani yake mwenyewe. Yeyote anaye muona mwingine kwa upungufu kwa umbo la Mungu, anaharibu maono ya ubora wa ukweli wa uwepo wake, na utakatifu wa Mungu. Yeyote ambaye anatangaza hali ya kuanguka ya mwingine anakubali hali ile kwake mwenyewe na anajiweka wazi kwa majaribu yale, kwa sababu sisi ni ndugu; mtu hawezi dharau udhaifu wa mwingine na awe na nguvu mwenyewe. Mtu hawezi tamani kupata kwa mwingine alama za uchafu na asijipate akiwa na upungufu wa usafi. Katika Sayansi ya Kikristo inatambuliwa ya kwamba kukiri kwa uovu katika mawazo yetu ni uhalifu dhidi ya mfikiriaji, na uwepo wake ndio adhabu yake.
Mtu anatakiwa kujikinga kutokana na imani zake za uongo pekee; kwa hivyo, mfikiriaji mwenye makosa pekee, au mtendaji mwenye makosa ya kiakili, kunaye au kunaweza kuwa ni yeye mwenyewe. Boriti katika jicho la mtu ndio uovu wote. Ni nini kinajumuisha dhana ya kibinadamu na ni nani aliyeiumba? Vita zetu zote ziko ndani ya mawazo yetu. Uovu hauwezi patikana, kwa sababu hauwezi fungwa.
Unapoona uovu, lazima uharibu nguvu zinazoonekana kwa wote, na pamoja na wewe mwenyewe. Nakuponya sababu najiponya. Tutaona wazo na utambulisho wake wakati mawazo yamekuwa ya kiroho. Kila ufahamu wa mtu uko na mawasiliano milele na mawazo yote binafsi – ufahamu wa ulimwengu wa Kristo. Wazo la Mungu juu yetu ndio wazo pekee tunaweza kuwa nayo juu yetu. Njia pekee ya kufikia mtu yeyote ni kuwafikia kupitia Mungu. Mwanadamu ni kwa urahisi wazo la Mungu binafsi; kwa hivyo hili wazo la kiroho linasamehe dhambi zetu na kuponya magonjwa yetu kwa sisi kuwa wazo hili. Uhai, Ukweli na Upendo ni moja, yenyewe pekee, na wewe ni dhihirisho lake sasa.