Kazi ya ulinzi ya sayansi ya Kikristo |

Kazi ya ulinzi ya sayansi ya Kikristo

Iliyoandikwa na BICKNELL YOUNG


Katika kufanya kazi ya “ulinzi” mtu anatakiwa kuchukua mda wa nusu saa kila siku na kutangaza ukweli juu ya ” ukosefu wa maadili.” Ukifanya haya, jua unashughulikia uovu ambao unajaribu kuzuia Wanasayansi wa Kikristo kuinua wafu. Uovu utakuja kwako wakati wote kama mtu, mahali au kitu. Wakati ni ukosefu wa maadili , itakuja kama mtu. Angalia kwa nakala yetu, Sayansi na Afya na utambue marudio ambayo “ujinga wa maadili” “wazo la makosa,” linatajwa na ukosefu wa maadili ya kiakili.

Ukosefu wa maadili ya kiakili haina sheria, haina chanzo. Ni uongo wa akili ya kimwili. Haina akili, haina utendaji, mfuatano, nguvu, akili, haina asili. Haifanyi kazi, na haiwezi, kupitia imani ya uhamishanji wa mawazo, wala kupitia imani ya hofu ya hali ya hewa au kuambukiza au janga. Haiwezi fanya kazi kupitia dhambi zozote kuu au kupitia kiburi, shauku, mashiko au hamu ya kula. Haiwezi fanya kazi hata kamwe. Hakuna kitu, vumbi kurudi vumbini.

Akili ya kimwili haiwezi fanya kazi kuadhiri kwa sababu ya sumu juu ya mwanasayansi ya Kikristo, wala kuathiri afya yake kwa njia yoyote, wala kusumbua akili yake. Akili ya kimwili haiwezi kufanya kazi kama ukosefu wa maadili kufanya kazi kama sheria; haina sheria, haina kazi, haina uwepo, haina uhai, haina dutu, haina mwanaume, haina mwanamke, haina mtoto, haina asili, haina njia, haina barabara, haina nguvu. Sio ya ukweli, ongo, na isiyowezekana, kwa sababu hakuna akili ya kimwili. Kuna Akili moja tu, hata Mungu, wema, bila shaka Akili pekee. Akili ya kimwili haiwezi jishinikiza kamwe, haiwezi fanya kitu chochote kizuri, kwa kiasili haiwezi fanya uovu wowote! Kwa maneno mengine, hakuna akili ya kimwili, kwa hivyo haiwezi fanya kitu.

Ukosefu wa maadili wa akili unaweza fafanuliwa kama kazi ya akili isiyofaa; inajaribu kufanya mwanasayansi ya Kirkisto kufikiria kuna kurudi kwa imani za zamani. Hakuna sheria ya ukosefu wa maadili ambayo yenyewe inaweza kuwa sheria ya kurejea, kurudi kwa imani za zamani. Kama mwanasayansi wa Kikristo ni mgonjwa, shughulikia ukosefu wa maadili. Kama sheria usishughulikie kitu chochote kingine.

Wakati unapompatia mwanasayansi ya Kikristo matibabu, tangaza: “Hakuna sheria ya ukosefu wa maadili ambayo inaweza fanya nisahau kitu chochote ambacho ni muhimu kufanya uponyanji huu mkamilifu, na ulio na mafanikio.” Fanya kazi kwa kina na uachie Mungu mengine. Wakati ugonjwa unaponywa na mwingine unakaa kufuata juu yake mara moja, hii ni ukosefu wa maadili wa akili; hakuna zijulikanazo kama sheria za ukosefu wa maadili; sio sheria. Hakuna sheria za aina ile. Mungu ni sheria , na Mungu ni yote.

Tangaza: ” Ukosefu wa maadili wa akili haiwezi jibishana kitu chochote; haiwezi jibishana au kupendekeza kwangu kitu chochote kiovu, aitha kwenye kimya au kwa sauti, ambayo inaweza kuwa na athari kwangu au kwa wagonjwa wangu. Haiwezi kufanya kazi kujibishana kupitia imani au kutoamini katika nguvu za sayansi ya Kikristo kuponya au kuokoa. Haiwezi zuia athari za uponyaji wa hii sayansi ya Kikristo. Haiwezi tengeneza sheria kushawishi au kuadhiri au kupindua matibabu haya, wala siwezi vutiwa kuwa na shaka juu ya nguvu zake, ufanisi, ukamilifu na uamuzi wake. Matibabu haya ndio nguvu pekee, kazi, ufanisi, uwepo na dutu ya wema wa milele. Ni neno la Mungu. Ni jiwe ambalo wajenzi walikataa. Inafanya kazi wakati wote kwa sababu ni ” Mungu pamoja nasi.” { Matt. 1:23}”

Watu wengine wanakuwa wagonjwa na ukosefu wa maadili ya akili. Kuishughulikia kunamaanisha afya, kutoishughulikia kunamaanisha hatari. Haijalishi madai ni nini, shughulikia ukosefu wa maadili wa akili. Lazima ujue haina madhara, haina sheria, haina kazi, haina akili kwa sababu haina chanzo, haina hisia, haina uhai. Yote haya ni uongo. Ugonjwa hauwezi kuhamahama, au kuhama kwa umbo moja hadi lingine kwa ukosefu wa maadili. Haiwezi elekezwa kwa msomaji katika kanisa , kwa mfano. Msomaji anaendelea vizuri, lakini mtu katika famiia yake anaweza adhirika. Hii ni imani ya uongo na haiwezi fanya kazi kama sheria ya kurudi. Usiwache iakisi kwako na kwa mwalimu wako, kwa sababu unaweza fikiria inachukua kulenga fulani kwa mtu unayemjua, kama haiwezi kugonga. Shughulikia ukosefu wa maadili wa akili kupitia upendo: Utaishughulikia mpaka utajua ya kwamba Upendo ndio mfutaji wa chuki. Upendo ni nguvu na hakuna nguvu nyingine.

Kwa kiini macho, shugulikia akili ya kimwili na imani potofu ya uhai kando na Mungu, sio mtu. Hakuna madai ya akili ya kimwili ambayo inaweza chambua, gundua au kusoma mwazo yako. Jua: “Mawazo yangu yako ndani ya ufahamu na hayawezi chukuliwa au kupatikana na sheria yoyote au athari ya ukosefu wa maadili.”

Tambua: “Haya matibabu huzuia na kuharibu sheria zote au nguvu za ushirikina wa kuona mbele, numerologia, urithi, nyenzo za matibabu na ulafi. Ukosefu wa maadili hauna akili, hauna kazi, hauna chombo cha njia ya nguvu, hauna serikali. Mungu ni serikali: ukosefu wa maadili sio kitu. Ukosefu wa maadili hauwezi tengeneza sheria ambayo siwezi fichua nia yake ambayo imeelekezwa kwangu. Mara nyingi inaelekezwa kwa kusudi ya kufanya uovu aitha kwa ujinga au kwa uovu, kwa hivyo lazima nikumbuke kujilinda dhidi ya chuki na wivu.” Mwanasayansi ya Kikristo ambaye “hafanyi kazi” huwa amevutiwa na hali ya kutoshughulika. Ana uzoefu wa kuvutiwa. Shughulikia haya na ujue: “Hakuna majibishano yanayoonekana na yasiyoonekana ambayo yanaweza kufanya kazi kama sheria ya ukosefu wa maadili wa akili kupitia imani ya Ukatoliki wa Kirumi, kuelekeza sheria kupindua matibabu haya, kufanya kitu chochote ambacho hakikuhusudiwa kufanywa.”

Usalama mkuu ni kutibu ukosefu wa utu wa uovu kwa kimya na kuweka madai yote nje ya mawazo yako, ukikumbuka ya kwamba hakuna sheria ambayo inaweza fanya kazi kama ukosefu wa maadili wa akili, hakuna sheria ila sheria ya Mungu na hiyo sheria haiwezi badilishwa.

Ukosefu wa maadili wa akili haiwezi shughulikia au kueneza kupitia masharti maalum ya mwelekeo, kukata tamaa, kuchukia na ukosefu, wala kwa ijulikanayo kama mwelekeo wa katiba. Haiwezi fanya kazi kama imani ya tabia, kujipeleka wala mapenzi yeyote au hisia zingine, kama tamaa, matamanio, au imani zingine zozote za wanadamu. Ukosefu wa maadili wa akili hauwezi fanya kazi kama sheria ya akili ya kimwili kuchanganya au kupunguza mawazo yako, au kuondoa kutoka kwenye enzi uwezo wa kufikiri, kuzuia, kuingilia, au kupindua tamko la Sayansi ya Kikristo. Haiwezi guza au kudhalilisha kwa sababu wewe ni mwanasayansi wa Kikristo. Hauwezi ibiwa fursa ya mwanasayansi wa Kikristo, wala uwezo wa kuyatumia.

Tiba ni kazi na neno la Mungu. Hairudi kwake utupu lakini ni athari ya mwisho na kamilifu na matokeo yake. Saa zingine ukiwa na hisia ya kwamba hauwezi pata matokeo tangaza ukweli kwa njia hii: ” Hii tiba ni kiini cha dhati, nguvu, uwepo na kazi ya wema mkamilifu na wa milele. Inafanya kazi yake kwa sababu ni ” Mungu pamoja nasi,” na inafuta , kufutilia mbali na kuharibu. Inaipunguza kwenye ubatili wake wa asili imani yoyote ya kimwili katika nguvu kando na Mungu. Mungu ndiye nguvu pekee. Mungu ndiye uhai pekee – hakuna sheria ya kupindua. Ukosefu wa maandili wa akili haiwezi tengeneza sheria ya kupindua, haiwezi fanya kazi kupitia imani ya hofu, kwa sababu ” upendo uliokamilika unatupa hofu:….” {1 Yohana 4:18}, na Mungu ni Upendo.”

” Ukosefu wa maadili wa akili hauwezi fanya kazi kupitia imani ya hali ya hewa, tabianchi au anga,kunigusa au kuniathiri kwa njia yoyote; haya ni mapendekezo ya akili.”

Usiogope hofu kamwe; ni mvuto tu. Ushirika na Mungu ndio sheria ambayo inaharibu uwepo wa kuonekana kwa uovu wakati wote. Hii ni ukweli; Ukweli hauna mwisho. Hauna upingamizi. Hauna mpinzani. Ukweli uko kila mahali, kwa hivyo uovu wa jina lolote au asili haina nguvu au uwepo. Ukweli ndio tamko lake mwenyewe, ushawishi wake mwenyewe. Haiwezi pingwa. Hakuna kitu kinachoweza kusimama dhidi yake. Hakuna kitu kinachoweza kuchelewesha, zuia, au kupunguza kazi yake au kuathiri uthibitisho wake. Hakuna kitu kinachoweza kupunguza uwezo wake wa imisho. Kwa kweli ni neno la Mungu ambalo “….halitarudi kwangu utupu, lakini litatimiza kile ambacho kinacho nipendeza, na litafaulu kwa kitu ambacho nilichokituma.” { Isaya 55:11}