Pata Baraka
Iliyoandikwa na BRUCE SINGLETERRY
Nashukuru kwa usaidizi wa ajabu wa mtendaji wa Plainfield, nimepata nafasi ya kusoma somo kuu, ambalo ni la kupata baraka kutoka kwa kila tajiriba, hata zile zinakaa ngumu. Wakati mmoja, nilishiriki katika ajali ya barabarani na nikapata hasara ya gari. Sikujua nifanye nini Nilihuzunika juu yake. Nilimpigia simu mtendaji na kumueleza yale yaliyofanyika. Jibu mara moja kutoka kwa mtendaji ilikuwa kupata baraka kutoka kwa tajiriba hii. Hii ilikuwa ni dhana mpya kwangu, kuchukua tukio kama hili, ambapo nilipata hasara, na kupata baraka kutoka kwake. Kwa hivyo niliendelea nikapata gari lingine na nikaendelea kujikumbusha ya kwamba kulikuwa na baraka katika tajiriba hii.
Nilitambua ya kwamba kuanguka, kuvunjika moyo, na kulalamika kwa kila tatizo tunalolipata sio picha ya mtoto wa Mungu. Nikapata kuamua ya kwamba kama kitu kitakuja na mshangao mbaya, nitakuja na mshtuo wangu, ambao sio kuanguka na kulalamika, lakini kuinuka na nguvu zaidi. Niliamua kusisitiza kufanya mapenzi yake Mungu na kupata baraka yake Mungu. Na yoyote shetani atajaribu, haitafanyika. Hii ilihitaji juhudi thabiti kwangu, ambayo ni nidhamu nzuri. Hapajakuwa na tukio lingine la gari tena, na imekuwa miaka mingi sasa. Nashukuru kwa usaidizi wake mtendaji kunigeuza kwa Mungu, na Kutenda kama mtoto wake Mungu na kuwa na baraka yake.