Jinsi ya kuokoa dunia
Iliyoandikwa na NANCY BEAUCHAMP
Mary Baker Eddy alifanya kauli ya ujasiri kwa Martha Bogue, mmoja wa wafanyikazi wa mwanzo. Alisema, “ Ukweli ya kwamba Mungu ni yote kwa yote na ya kwamba hakuna uovu, unaoshikiliwa kwa uaminifu na wanasayansi ya Kikristo, utaokoa dunia na ndio tu utakao iokoa.” {Nyaraka mbalimbali} Inavyoonekana, Mama Eddy alikuwa anaongea kuhusu mustakabali usio mbali. Alitupatia kidokezo kuhusu mkasa wa mustakabali wa dunia yote na wakati utakapotokea aliponukuu waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia ukurasa wa 106 katika Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko ya Bibilia.
“Sasa matendo ya mwili yanadhihirika, ambayo ni haya; uzinzi, uasherati, uchafu, tamaa za kimwili, kuabudu sanamu, uchawi, ugomvi, uasi, uzushi, wivu, mauaji, ulevi, sherehe za faraja, na kama haya: ambayo na waambia mbele na kama vile nimewaambia wakati uliopita, Ya kwamba wale wanaofanya mambo kama yale hawatauridhi ufalme wa Mungu.”
Kiashiria, unauliza? Aliandika kwa mlazo jina uchawi. Haijalazwa katika Bibilia ya mfalme Yakobo,{ Wagalatia 6: 19-21}. Sisi kama wanasayansi ya Kikristo tunapaswa kushughulikia imani ya uchawi,imani katika nguvu ingine kando na Mungu ambapo uovu unaabudiwa. Kamusi ya Webster ya mwaka 1828 inafafanua uchawi kama “utendaji wa wachawi; uchawi; mashawishi; ngono na shetani.” Uchawi unafafanuliwa kama “uganga ikiwa na usaidizi au usaidizi usemekanao wa roho mbaya.” Mashawishi ni “utumiaji wa sanaa za kichawi, laana au hirizi.” Basi, tunatakiwa kuwa na hofu juu ya uchawi na laana ovu? Hapana. Kama vile Sayansi ya Kikristo inafunza, Mungu ndiye nguvu pekee katika ulimwengu na zote tunapiga magoti kwa Kristo. Amri ya kwanza ni “ usiwe na Miungu wengine mbele yangu.” Hatutakiwi kuwa na imani au kuamini nguvu yoyote ingine isemekanayo.
Na Mama Eddy ametupatia njia za kushughulikia imani hii au mvuto katika taarifa yake kwa Mama Bogue, “Ukweli ya kwamba Mungu ni yote kwa yote na kwamba hakuna uovu, ikishikiliwa kwa uaminifu na wanasayansi wa Kikristo, utaokoa dunia na ndio tu utakao iokoa.”
Tunatakiwa kushikilia ukweli wa Mungu mwenye uwezo wote ambaye anaijaza nafasi yote, na haachi nafasi kwa uovu wa aina yoyote. Mungu ni, “ Mwenye macho safi na hawezi tazama uovu, na hawezi angalia uovu.” {Habakuki 1:13} Lazima tukemee imani ya pepo ya kwamba uchawi, haipnosia, roho mbaya ziko na nguvu yoyote au uwepo. Moja wapo ya amri za Kristo Yesu kwetu ni kukemea mapepo, au fikira za mapepo. Na tunawezaje fanya haya kama wanasayansi ya Kikristo? Mama Eddy anatuambia “ Njia ya kuchopoa uovu kutoka kwa akili za kimwili ni kumimina ukweli kupitia mafuriko ya Upendo.” {S&H ukurasa 201:17-18}
Lazima tumpende mwanadamu mwenzetu na kushikilia kwenye ukweli ya kwamba mfano wa Mungu hauwezi vutiwa na uovu wa aina yoyote. Na lazima tumimine huu ukweli kupitia mafuriko ya Upendo kwa wanadamu wote. Hii ndio tu pekee itakayo okoa dunia yetu.