Uhai
Kutoka kwa Jarida la Sayansi ya Kikristo la Aprili 1918
na Mary Baker Eddy
Haya mahubiri, ambayo muswada wake uko katika umiliki wa bodi la wakurugenzi wa Sayansi ya Kikristo, yametayarishwa na Mama Eddy, Dhahiri kwa toleo la mdomo, kwa mda wa miaka thalathini na tano iliyopita, hivyo mtindo wa maandishi unatofautiana kidogo na maandishi yake ya baadaye. Ili kuhifadhi kwa kikamilifu nguvu na asili za tamko hili, maandishi ya muswada asili yamechapishwa hapa chini kama yalivyoandikwa. Uakifishi imeongezwa, marejeleo ya Bibilia imethibitishwa, na maandishi ya herufi kubwa kufanywa kulingana na kanuni za Mama Eddy. Maneno machache ambayo yalikuwa yametolewa yanawekwa kwenye mabano, na katika hoja mbili ambapo msomaji anarejeshwa kwa Sayansi na Afya, Dhahiri vipengele vilivyotolewa vinarejeshwa na kupatianwa, ikiwa na idhini ya kitabu cha Sayansi ya Kikristo. -MHARIRI
Kwanza. “Mimi” ambayo inarejelewa katika maandishi sio mtu, ni Kanuni. Sio binadamu, ni Mungu. Yesu alisema, “Maneno ninayonena kwenyu sineni juu yangu.” Yesu alikuwa mwanadamu; alionekana dhahiri kwanza kwa hisia za kibinadamu kama mtoto ambaye mlio wake wa kitoto uliendanisha na kelele ya mbuzi na kelele ya ng’ombe, katika mkoa wa mbali wa Judea. Katika wakati ule wa Josephus, kulikuwa na watu kadhaa waliokuwa na jina Yesu {kwa kimwili} Yesu hakuwa Kristo; Kristo lilikuwa jina lingine la Mungu, na lilikuwa jina la heshima lililopewa Yesu kwa wema wake mkuu. Katika maandishi asili neno Mungu lilipata chanzo chake kutoka kwa neno wema, hivyo neno Kristo Yesu, mtu mzuri. “Sayansi na Afya ikiwa na ufunguo wa Bibilia, ukurasa 333:32
Katika kifungu, “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai,” “Mimi” inayoashiriwa ni Mungu ambaye ni Kanuni ya Kimungu ya mwanadamu Yesu na ndiyo ilimuongoza njiani mwake katika Sayansi. Kwa ufahamu huu wa Kimungu, vipindi hivi tofauti vimeambatanisha na maneno Uungu, Yehova, Kristo, na Mungu. Maneno haya yanatakiwa kueleweka kudhihirisha Mungu kama dutu ya Kimungu na ufahamu ambao sio wa binadamu wala mtu; lakini ni Kanuni ya milele. Tamaa ya mali katika chanzo cha enzi ya Kikristo, ilihitaji mwanadamu wa kiroho kufundisha Kanuni ya Kimungu na kuonyesha kwa kudhihirisha kwake ni nini hii Kanuni na matokeo ya kuifahamu.
Yesu alikuwa mtu wa enzi; alikuwa akielezea Uhai vizuri kama Mungu, lakini kanuni na kielelezo chake kilieleweka vibaya. Kanuni ya Kimungu ya yule bwana hawakuelewa; wangeielewa, wangekiri ya kwamba udhihirisho wa Yesu ulidhibitisha Kanuni yake, na Kanuni yake ilieleza udhihirisho wake. Ukweli na Uhai ukieleweka unatoa makosa, unaponya wagonjwa, unafufua wafu, na udhihirisho huu unaleta kwenye mwangaza Ukweli wa Uhai na Uhai wa Ukweli. Ukweli moja katika historia ya Yesu ni Dhahiri kwa wazi, yaani, ya kwamba Kanuni, sheria na mbinu za uponyaji zilikuwa za Akili sio kimwili, ya kwamba hakuhitaji dawa, sheria za kidini, au mafundisho ya kidini kusaidia katika kazi yake.
Alisisitiza tu kufanya chemichemi kuwa safi; alitoa hoja ya kwamba akili kwanza lazima iwe sahihi ili kuweka mwili sahihi, ya kwamba tunatakiwa kujua kanuni ya binadamu, na kuelewa Mungu vyema zaidi, ya kwamba tunatakiwa kuwa na Sayansi ya Uhai, kwa sababu bila kuwa nayo udhihirisho wa Uhai na Ukweli haiwezi fanywa. Sayansi inadai akili iliyo na afya na mwili ulio na afya, akili yenye afya kwa sababu imejawa na Ukweli, na mwili wenye afya kwa sababu unatawaliwa na hii akili. Mafundisho yote ya Yesu ilikuwa kwanza kuweka mawazo sawa na Ukweli wa uwepo; Pili, kusoma jinsi ya kutawala mwili na huu Ukweli; Tatu, Kutawala mwili na huu ukweli. Kuamini ya kwamba Mungu ni mtu, inazuia ufahamu wa Kanuni ya Kimungu na udhihirisho wake. Hatuwezi dhihirisha mtu, kwa hivyo mtu sio nguvu ambayo inaponya wagonjwa katika Sayansi; tunaweza uliza mtu kutibu ugonjwa wetu na kusamehe dhambi zetu, na hayo ndiyo yote tunaweza fanya, lakini tunaweza fanya zaidi ya haya tukiwa na Kanuni, tunaweza ifanyia kazi kupata matokeo haya, na kufuata sheria yake ya Kimungu, tukiwa nayo tunaweza haribu magonjwa, dhambi na kifo na hii ni kulingana na maandiko. “Fanya kazi ya wokovu wako …..kwa sababu ni Mungu ambaye anafanya kazi ndani yako.” Ukweli unaharibu makosa, kama vile mwangaza unaharibu giza. Dhambi, ugonjwa na kifo ni makosa; ni imani na huu ukweli ukijulikana utaziharibu kwa kirefu. Ukweli unaleta Uhai kama matokeo yake; kwa kuwa Ukweli ni uhai wa milele,na Ukweli wa Uhai utaharibu kifo. Lakini huu ufahamu huja polepole; hata kuelewa ya kwamba kimwili haina hisia na kazi kubwa, ingawa pendekezo hili rahisi ni dhahiri lenyewe.
Katika maandiko, “Mimi ndiye njia, Ukweli, na Uhai: hakuna mtu anayemjia Baba ila amepitia kwangu,” kwa kiasili tunauliza, Ni njia gani hii inayorejelewa? Ni njia ya uwiano na udhihirisho ni kupitia ufahamu wa Kanuni yake ambayo tunaweza toa uwiano ule. Mtu ambaye anaamini kutotosha , njia, kwa hivyo, kwa kuwa hii ni Sayansi na hakuna anaye kuja kwa Baba, ikimaanisha, anaweza elewa Kanuni ya uwepo isipokuwa kwa Sayansi. Kupitia Sayansi pekee ndio tunaweza elewa Uhai na kudhihirisha ufahamu wetu, kwa Uhai na sio kifo. Maandiko yanatwambia ya kwamba, “Upendo uliokamilika unafukuza hofu,” lakini amri hii ya kwanza ndio chaguo la mwisho; hata tunafundishwa kumwogopa Mungu, wakati ni Sayansi kupenda wema ya kwamba tunamiliki nguvu ya wema ya kuponya na kuokoa. Kama tungemfahamu Mungu , hatungekuwa na sababu ya kumuogopa; tunatakiwa kujua ya kwamba hawezi muadhibu mtu kwa Kutenda wema; kamwe hakutengeneza sheria ya kupooza akili kwa sababu ya ubinadamu mwingi, au upendo ulio kamilika, na hofu ya sheria kama ile na matokeo yake basi, yangekuwa kutupiliwa nje na wazo sahihi la Mungu. Tunaweza kukuongelesha juu ya metafizikia, Kanuni yake ya Kimungu, sheria na matumizi , mara moja kila wiki, lakini hii hukupatia mtazamo mdogo katika Uhai ambao kupitia kwake tumejua metafizikia na ambaye lazima usome kupitia kwake. Huduma hii ya wiki hata hivyo inaweza elekeza kwenye njia alama ya hatua ambayo ni yote. Na watahubiri aje , ila wawe wametumwa?’ Mtume anasema, “Watasikia aje bila muhubiri? Paulo alijua mazoezi ya kinadharia, na kusaga kwa maghala ya kisomo sio matayarisho ya Mwalimu mwenye maadili. Alijua msukumo waja kutoka kwa Ukweli, kutoka kwa Roho na sio maandishi. Mtoto aliye elekezwa na Munguana uwezo wa kunena Ukweli kwa urahisi na utamu wake na nguvu za Upendo kuliko theologia iliyotengenezwa; ndipo maandiko, “Kutoka kwa midomo ya Watoto…mumekamilisha sifa.” Sisi wote tutajua wakati Ukweli uko kazini katika Sayansi, kwa sababu utaponya magonjwa yetu na kusimamisha dhambi zetu. Kwa kiwango ambacho tunaelewa Ukweli utatuponya akili na mwili, na kwa kiwango ambacho tutakubali makosa, ndio italeta dhambi, magonjwa na kifo.
Pili. Uhai ni udongo na Roho? Uhai unachukuliwa; hata maandiko inarejelea kwake katika enzi za giza za sadaka zilizochomwa na dhabihu. Tazama Mwanzo 9:4, “Lakini nyama ikiwa na uhai, ambayo ni damu, hamtakula.” Lakini hii ilikuwa ni utaratibu wa kitamaduni, dini ya kimwili ambayo ilijaza dunia na damu. Katika injili ya Ukristo wa kiroho zaidi, tunasoma Uhai kwa kinyume. Katika Warumi 8:6 tunasoma,”Kwa kuwa na akili za kimwili ni kifo; lakini kuwa na akili ya kiroho ni uhai na amani.” Isaya 38:16, “Ewe Bwana, kwa haya mambo watu wanaishi, na kwa haya mambo yote ndio uhai wa roho yangu.” Warumu 8:2, “Kwa kuwa sheria ya Roho ya uhai katika Kristo Yesu imenifanya huru kutokana na sheria ya dhambi na kifo.” Timotheo wa pili, “….Kristo, ambaye amefutilia kifo, na ameleta uhai na maisha ya milele kwenye mwangaza kupitia injili.”
Dhana zetu kuhusu Uhai kama Roho zinatoka kwa Sayansi na zinainua malengo, kutakasa nia,na kusafisha hisia; lakini dhana za uhai kama udongo zinapunguza, kudhibiti, na kufanya kimwili. Ushahidi pekee ambao tunao wa uhai wa kimwili unaonyeshwa na hisia zile tano za mtu, na hisia hizi ni gani, ila ni kimwili? Mishipa na akili ni kimwili moja kwa moja kama uzi wa viatu, au Sokoto la matunda. Kupitia uwezo wa kuona, uhisi wa harufu, au uwezo wa kusikia, hatuwezi pata hisia hata kidogo ya Mungu; hatuwezi ona wala kusikia, kuonja, au kunusa Uhai. Kwa hivyo ni Dhahiri kwa lenyewe.
Miundo ya mwili inasema kwamba damu na mishipa inatufahamisha kwa usawa kuhusu uhai wa binadamu, hata kama ni wazi kuwa Uhai ni Roho, na kwamba kimwili haiwezi tambua Roho. Tena, tunasema mishipa inatambua uhai na uhai ni kikaboni, lakini mishipa inawezaje hisi au tambua uhai zaidi ya jiwe au umbo lingine lote la kimwili laweza hisi au laweza tambua? Uhai pekee ambao hisia za mtu zinatambua ni kupitia akili za kimwili na imani ya mfumo ya kwamba ajali inaweza haribu kulingana na imani ingine. Uhai ni Roho na sio udongo kimwili kamwe, wala haiwezi kuwa na umbo, kwa sababu ni wa milele. Tunasema tena, mishipa inatambua Uhai kama mwanzo na mwisho, hata kwa maua inayofifia hadi kwa dunia inayoanguka, kwa kifo cha nyasi hadi kwa kifo cha binadamu. Lakini wakati mishipa inatoa Ushahidi wa uongo wa uhai na kifo, kuna kitu kinachosema kwa wakati wote, “Naishi, Ni mimi, na zaidi ninasoma ya kwamba Uhai ni Akili na sio kimwili, na kwamba Akili inaunda maadili ya vitu zote; ya kwamba akili ya kimwili inaunda mboga, mnyama, na ufalme wa madini na uumbaji wake, ikiwapatia wote kioleshi chake cha kimwili, umbo, na rangi, wakati miundo ya Akili yenye uhai wa milele au Mungu haiwezi haribika, iko na uwiano na ni ya milele.”
Upande huu wa maumbile ambayo inakaa kwa hisia za kimwili ni pazia ambayo inaficha ukweli wa uwepo; Ulimwengu unao onekana ni picha ya mawazo ya akili, himisho ya mawazo, kumbukumbu ya maandiko ya michoro na kutafakari Mungu. Kwa maneno ya Starr King, “Hakuna sayari ambayo inaendesha duara ndogo kuzungukia mwali unaodhibiti, hakuna jua linalong’aa kwa mfululizo kwenye kina cha nafasi inayo zingira, hakuna kometi inayokimbia kwenye njia yake, hakuna muungano wa nyota ambao unaning’inia kama taa ya ndari kwenye kivuli cha mbingu, ambao sio kauli inayoonekana ya dhana ambayo inaishi kwenye Akili yenye nguvu zote. Ni kupitia amri kimya ya Akili ambapo mwangaza wa asubuhi hulipuka kama wimbi la utukufu juu ya ulimwengu wenye mpangilio.
Tatu. Mwenye kimwili huhisi ardhi chini ya nyayo zake ikiwa thabiti, lakini mwana Sayansi anahisi kwa uhakika uthabiti wa Ukweli. Kudumu kwa milele kwa vitu hakuonekani na hisia. Mtu anaweza kuwa na uhai kama vile apendavyo, akifanya kazi kwa usahihi. Kwa kuelewa uhai tunauongeza kama vile misuli inanenepa kwa utumiaji; tuna uhai zaidi kama vile tunao Ukweli, wema, fadhila na kadhalika. Uhai ni nini? Ni Roho. Roho ni nini? Mungu. Mungu ni nini? Akili. Asiye na makosa, wa milele na Akili ya milele. Lakini Mungu ni uhai unaoendeshwa kama msumari usio na akili ndani na nje ya kimwili? Kimwili hutawala Uhai, Mungu, na Uhai, Mungu hana kitu cha kusema juu yake mwenyewe? Tunauliza kukubali au makataa ya Akili kuzaliwa tukiwa watoto au kufa tukiwa mzee aliodhoofika? Si ubishi au kukubali kwa akili kwa matukio muhimu inazingatiwa kwa upungufu kuliko mlio wa mbwa kwa mlango wako? Lakini Sayansi kwa hivyo haihesabu haki maalum za Akili; lakini imeipatia taji Akili na Uhai, ukuu, na uhai wa milele. Mimi sio mwana panteisti kuamini ya kwamba Mungu yupo katika kimwili, vile mtu amepungukiwa kimwili ndio yupo karibu na Roho, Mungu, na anapotolewa kimwili yote, na mpaka wakati ule, hii Kanuni ya Kimungu itamfunika kwenye furaha na utukufu. Afya, Uhai na tabia kamwe hazitafika kilele chake mpaka tuachilie imani ya kwamba kimwili iko na uhusiano wowote na Uhai. Katika fizikia tunasema, Uhai umefungwa katika miundo yake, ya kwamba Uhai uko chini ya kukua na kuzoroteka; lakini hapa swali la zamani linajionyesha, ni nini ya kwanza, yai au ndege? Ua au mbegu? Kama yai ni ya kwanza, yai lilitoka wapi, na kama ndege ni ya kwanza, chanzo cha ndege ni nini? Kama hakukuwa na maua, mbegu yake ilitoka wapi, kwako kusema bila mbegu hakuwezi kuwa na maua; ingawa maandiko inatufahamisha aliumba kila mmea kabla ya uwe kwenye ardhi. Akili, na Akili pekee ndio muumbaji. Sayansi inaonyesha kwa undani somo ya kwamba kuna nguvu ya kawaida na uthabiti katika dunia ya Akili, na uumbaji wake, ambao kimwili ni mpito; kila kitu tunachogusa au kuona ni umbo na rangi ya wazo ambalo liko nyuma yake. Tunasoma kwenye metafizikia ya kwamba uhai uko katika mawazo badala ya kile kitu imeonyesha, na ya kwamba hii wazo liko na uhai wa milele kulingana na kiwango cha usahihi wake; ya kwamba uhai kamwe hauingii maumbo yake, kwa kuwa Uhai ni wa milele; ya kwamba Uhai hauingii katika mipaka ya mawazo yake, kwa kuwa Uhai na Akili ni moja. Niko na furaha ya kwamba kuna Mungu mmoja, Uhai moja na unaoneka katika mpangilio, uzuri na wema. Niko na furaha uovu hauna uhai au uhai wa milele, ya ‘kwamba uchungu wa kimwili chanzo chake ni vitu za imani, ndoto na sio ukweli, mabadiliko yasiyotarajiwa ya kimwili na sio wazo la milele; na ya kwamba haya kwa wakati mmoja yatasomwa na mwili kufanywa huru kama maoni ya ndege, na kila hisia ya udhaifu au uchungu utatoweka.
Nne. Kifo ni nini na ni nini hali ya binadamu baada ya kifo? Swali hili limepatana na majibu yake kwa majibu ya maswali mengine mbeleni, lakini kama metafizikia inapatikana kuwa Dhahiri kupitia maelezo juu ya kifo, kwa kushughulikia kitu kisichokuwapo kama kipo, tutaelezea kwa ufupi kwa hili fumbo la hisia ambalo halijatafitiwa. Tunahitaji ufunuo wa kuridhisha zaidi ya ukweli ya kwamba Ukweli na wazo pekee ni ya kudumu? Kwa kuwa tunajua hakuna katika ukweli kifo, ya kwamba Akili haiwezi kufa, na ile yote ambayo ni ya milele ni Akili na maadili yake. Lakini enzi hii haiko tayari kukubali ukweli huu, haiko tayari kamwe mwanzoni ukweli wa kwanza wa Kanuni. Lakini kwa haya yote lazima turudie ukweli vile vile mpaka ueleweke. Uchungu na furaha ya mwili ni imani iliyokaribishwa na mawazo ya kimwili, kwa kuwa kimwili haiwezi teseka wala kufurahia. Akili ikisema nina furaha, matokeo yatakuwa furaha na kinyume kwa kuwa hauna kitu kinachoweza kuongea juu ya akili. Udongo hauwezi jibu mfinyanzi, umenitengeneza hivi kwa nini? Kimwili haiwezi sema, mimi ni dhaifu; Mimi ni mgonjwa; mimi niko kwenye hali mbaya; Mimi nafa, au nimekufa. Ukweli, imani yenye makosa ya kimwili inaweza sema hivi kwa ile inayoita kimwili, lakini kimwili haiwezi sema. Kimwili iko na uhai wakati tunasema imekufa kama vile ishawai kuwa; na ambayo imekufa wakati tunaita yenye uhai.
Tazama pia maandishi mbalimbali, ukurasa 42.
Hakuna kifo, akili haiwezi kufa, na kimwili haina uhai, hivyo hakuna kitu ambacho kimebaki cha kifo kudai, Paulo Aliona haya na akasema, “Kifo, mshale wako uko wapi? Kaburi, ushindi wako uko wapi? Mshale wa kifo ni dhambi; na nguvu za dhambi ni sheria.” Alichukulia maumivu ya kifo kama imani ya kimwili, mateso ya mawazo, na sio ya mwili, na kwamba mawazo ya kimwili yalikuwa yametengeneza sheria hii ya mateso.
Moyo unaopenda umesema, Tutajuana mtu kwa mwingine pale? Na iko wapi Bahari hii inayong’aa, tutaitafuta na hatutalia tena? Kwani kutoka tuchunguze metafizikia na kupitia katika uhuru ufalme wa Akili, tumekuwa waangalifu kuzidisha dhamana ya uvumbuzi wetu, au kutaja yale ambayo hatukuelewa. Hatujadhihirisha hali sahihi ya uwepo wa binadamu kuzidia mipaka ya mtazamo wa hisia zetu, na tu kadri tunawaza kutoka kwa utoaji ndio tu inawezekana kufafanua hali hii. Nadharia yoyote ambayo imezidia hitimisho hili, tukitegemea hali ya walioondoka imeeleweka kwa kikamilifu, ni kadirio lisilo na faida, na lisilo na haiungwi mkono na wazo au ufunuo.
Kutoka kwa ukweli dhahiri kwa ufahamu na ulio kusanywa kutoka kwa Sayansi ya Nafsi, tunajua binadamu ni wa milele, na kwamba kivuli tuitacho kifo ni mpito wa imani ya kimwili. Hakuna mabadiliko ambayo yamefanyika tukisema, “Rafiki yangu ameaga;” rafiki yule anasema kwa ufahamu kamili wa uhai na mazingira yake, “ Sijawai kufa. Ilikuwa tu ni ndoto niliyokuwa nayo; kwa kuwa uhai unaendelea nami kama hapo awali. Mimi sio roho; mbali niko na nyama na mifupa kama nilivyo kuwa; mabadiliko pekee kwangu ni, siwezi wasiliana na marafiki wangu, na kwa nini? Kwa sababu hawanielewi sasa, Wananiita roho, lakini mimi sio vile; wanasema nilikufa, lakini sikufa; hawajui mimi ni nini, mahali nipo, au nafuatilia nini. Sitakuwa roho mpaka niachilie vikomo vyote; vimepoteza ushahidi wake juu yangu kupitia hisia za utu kwa sababu wanasema nimebadilika, nilikufa; mtazamo wao wenye makosa juu ya uhai umetutenganisha; imani ya kwamba uhai ulifika kikomo nami, au ulichukua umbo lingine jipya, imezuia ufahamu wao wa ukweli wa uwepo wangu wa sasa, hivyo kutenganishwa kwetu kupitia imani hizi zenye kinyume na hali zetu zenye kinyume kama matokeo. Mawasiliano zaidi kati yetu haiwezi fanyika mpaka imani yao ibadilike kupitia hatua ambazo yangu imepitia na iwe kama yangu. Mabadiliko haya yataitwa kifo, lakini hii ni imani yao kuihusu, sio yetu, ambao tumetoa pazia ambayo huficha siri ya wakati.
Mpangilio, uzuri, na wema. Wanadamu hudai kujua ya kwamba uchungu ni wa kweli , ingawa hauonekani; wanatakiwa kujua ya kwamba amani na furaha ni ukweli mkuu na kwamba hii dunia ni pazia ya utukufu uliong’aa zaidi ambao uko mbele yake.
Hivyo pitia haraka mbele ya ukumbusho katika awamu tofauti na hali za uwepo, makosa ambayo inatoweka polepole, na Ukweli kueleweka. Tufurahi ya kwamba Uhai kama ua linalofunguka unafunguka kwa ufahamu wetu furaha ya uwepo, kwa kuwa ndio vitu zote takatifu. Uhai, nguvu ni bure Kimungu, ukiwa na zawadi kwa wale waliopungukiwa za hekima na Upendo uliokomaa; ukiwazungukia na bawa la njiwa, uhai wa milele wenye uhuru. Ngonjeni kwa Subira enyi wote mliojitenga na sanamu za dunia, kumbuka ni mziki uliovunjika unaotoka kwa furaha iliyo juu lakini tumaini inayo malengo ya juu zaidi. Tutajuana pale. Tukio la furaha, ufahamu ulio wazi zaidi, mwangaza usiotingizika ndio urafiki utakuwa. Mziki wa Uhai uliojaa utatoa milio yenye furaha wakati moyo utapatana na moyo, ambapo zawadi za kuridhisha na safi zinawekelewa kwenye madhabahu inayofaa. Furaha inayo kisima chenye uhai, furaha ya milele. Moyo unasikitika, Mustakabali utakuwa na nini? Huu ndio mustakabali; mbinguni itakuwa yenyu, lakini wakati uhai wake utakuja hakuna mwanadamu anaye jua, hakuna “mwana ila Baba.” Dhambi zetu hazisamehewi mpaka ziachwe, hapa ama baada ya hapa, kwa kila dhambi kuna kiwango cha dhiki juu yake na kifo hakiwezi endeleza furaha yetu, au kutufanya werevu, bora au wasafi zaidi. Sayansi ya uwepo wote lazima isomwe kabla kushinda haya. Furaha sio faida ya wakati mmoja. Baada ya pazia kuanguka, lazima tusome kama sasa njia yetu Kwenda mbinguni, kwa hatua polepole na zenye unyenyekevu, kwani hakuna mwanadamu akujae kwa Baba ila kupitia Ukweli na Upendo.
Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko, ukurasa 201: 20; 479:9.