Mtazamo wa Upendo
Kutoka kwa Mafundisho Hotuba na
EDWARD A KIMBALL
Umuhimu wa Kukesha
Fikiria ya kwamba kila mmoja wetu anatakiwa kukesha kwa masaa kumi na mbili na tuone mara ngapi tunakubali makosa, au kutangaza makosa, kutangaza kitu ambacho kiko dhidi yetu. Utashangazwa kuona kiasi gani utafanya haya. Kama ungeendelea kuhesabu kwa masaa kumi na mbili, ni uwezekano mkubwa unaweza jiangalia milele. Tena, unafikiria utapata nini ikiwa ungeweka maanani mawazo yote ambayo ni kinyume na Upendo? Hapa ni wanadamu na tunawaona wamefinyiliwa na chuki katika aina zake tofauti. Watu wanachukia, na bado wanatarajia kujifunza kupenda. Madai ya Kimungu ni kujifunza kumpenda Jirani yako kama unvyojipenda; kujifunza kuwafanyia wengine vile ungependa kufanyiwa.
Kanuni ya dhahabu
Utaenda umbali upi kabla ya kupata makosa, ukiweka sheria ile katika utendaji? Ijaribu, – Ningependa Jirani yangu kunifanyia haya, kufikiria haya juu yangu? Kabla ya maneno yale maovu yatoke, kabla ya hisia ovu, kabla ya matendo maovu, tungeacha na kusema, “Ningependa anifanyie haya?” Ni mara ngapi ungesema, “Hapana?”
Thamana ya usaidizi kutoka kwa Mungu
Mpaka tusimame kwenye mlango wa mawazo, tukiwa na umaakini mkali, na kuweka kanuni ya dhahabu kama jaribio la mawazo yetu na hisia na vitendo, na kujifunza kutawaliwa ipasavyo, tunayo matumaini ya bure kwa usaidizi wa kutosheleza ,bure kwa mbinguni, kwa wazo zima la maisha, kwa sababu Upendo ni dutu, Roho, kanuni ya Uhai. Lazima tupate mtazamo wa Upendo, na tufanyie wengine kama vile tungependa watufanyie.
Usihukumu
Jifunze kusamehe, kusamehe kabisa. Ondoa ukali wa kutisha ambao unaharibu mwanadamu. Ondoa mzigo ambao umewekelea mwanadamu mwenzako, namaanisha hukumu. Ni mzigo wa kuhuzunisha ambao tunawekelea mwanadamu wakati tunapoingia kampeni ya hukumu! Ni mara ngapi sisi tumetenda kitendo cha kuhukumu, ambayo haimfanyii mema na hutuzuia? Ni kwa mda gani tutakuwa kwa kutosamehe? Hatutawai pata afya na kuwa na furaha katika undugu wa mwanadamu mpaka tujifunze kusamehe, kuwa na huruma, kuvumilia na kupenda.
Himiza na hamasisha wema kwa wengine
Kiasili, sisi wote ni wenye dhambi, kila mmoja wetu. Tunaangalia mtu ambaye ni mbaya kwa asilimia sitini na mzuri kwa asilimia arobaini na kuhukumu yale mabaya. Mama Eddy alijua ya kutosha kutumia asilimia arobaini ambayo ni nzuri. Sasa haya ndio lazima tufanye: kutumia vizuri asilimia arobaini ambayo ni nzuri kwa ndugu yetu mwanadamu, na kungoja iwe Hamsini na sitini, na kadhalika.
Jifunze Kupenda
Ni kitu rahisi kwa mtu kuruka juu ya jukwaa na kusema, “Bwana anasema.” Ni kwa kusita kukubwa nayafanya haya. Lakini nimejifunza haya. Sina pembe hata moja ya uovu juu ya mtu yeyote duniani na hakuna mtu yeyote siwezi samehea; nimekuwa na hasira wakati mwingine kama mtu mwingine ushawai ona. Ni ya kufariji zaidi kupenda; mara nyingi inayofurahisha, kwa kiasi kikubwa inayotosheleza. Ni ya kushangaza ya kwamba mtu anaweza kupumbazwa na kitu cha kushangaza kama chuki. Ni kuoza kwa akili. Hula kabisa; inaleta huzuni na magonjwa.
Hakuna uhai bila Upendo
Alafu kumbuka hukumu itakuwa juu yetu, na kama hatuna upendo, kisha hatuishi, kwani Upendo ni uhai. Kwa kikamilifu, unaona kama msafara, tunaelekea kwenye mafanikio haya, na yale ambayo yanayo yategemea ni upanuaji, uinuaji wa mawazo yetu; kuweka mawazo yetu yakifikia; yakichukua mwelekeo mkubwa wakati wote, ikiwa na Upendo zaidi. Iache ifanye yote inayoweza; na kutangaza mambo yanayostahili, tangaza kwa yale ambayo yangepita.