Changamoto ya Kukata Tamaa
Kutoka kwa Hotuba juu ya Sayansi ya Kikristo na PETER V. ROSS
Hatujakosa usaidizi katika mchanganyiko na msukosuko wa nyakati. Tuko na uwezo wa kuangamiza, bila kelele na kwa kumaliza , ushawishi wa hisia kali zinazojitahidi kuharibu viwanda na serikali, na jamii yenyewe. Watawala wa kiimla wanafikiri kipindi hiki cha ukosefu wa maadili kimefika. Wanakadiria ya kwamba saa imefika ya kuvunja demokrasia na utamaduni wa Kikristo.
Fikra kamili zinatambua ya kwamba kupotea kwa kijamii, siasa au uhuru wa kiuchumi inaweka kwenye hatari uhuru wa kiroho. Hivyo ndivyo mkristo sio mshtawishi au mwingilizaji wakati uhuru uko hatarini. Silaha yetu ni ya aina ya kwamba ushawishi huu usio wa kawaida hauwezi ona au kushughulikia. Silaha yetu ni ukweli ya kwamba Kanuni hutawala wakati wote na mahali popote, ikifanya nguvu zisizochini ya kanuni kukosa athari. “Bwana atawafanya wawe dhihaka.”
Viongozi katika kazi, katika biashara, katika serikali lazima wajifunze ya kwamba Mungu huelekeza shughuli za wanadamu. Anatawala pale leo, kama vile amefanya kwa wakati wote, bila kujali uongozi unaoonekana wa ubinafsi, migogoro na unyanyasaji. “Anasikitisha vifaa vya wajaja.” Hakuna serikali ingine kuzidi yake. Hatimaye hii serikali itaonekana ikishinda.
Uyakinifu wa kimabavu, ukikosa ufasaha wa kiakili, lazima uzame kwenye kuchanganyikiwa na kushindwa unapokabiliwa na nguvu za kawaida na za kiroho za Sayansi ya Kikisto. “Mungu mwenye uwezo wote anatawala” sio shaba inayopiga kelele. Wala uhakika, “ Anaharibu mikakati ya walio wajanja.” Ahadi za Bibilia zinatimizwa, kwa sababu ziko zaidi ya ahadi, ni ukweli usioshindwa.
Kila mtu binafsi lazima aombe kwa dhati ya kwamba taifa lake liendelee kwa hekima na kwa haraka katika tatizo. Kila siku anatakiwa kuweka mda kando kutambua: “Mungu yuko kati yake; hawezitingisika.” Ombi hili linatakiwa kupanuka kwa kusisitiza ya kwamba waume na wake walio katika nyathfa za uwajibikaji watakuwa na ujasiri na ubunifu kuchukua jukumu lao katika ulingo wa dunia.
Nguvu za uovu zinabeba ndani yake mbegu za uangamizi wake. Hazina ufahamu. Wanakaribia wazimu. Tunatakiwa kusema na kujua haya mambo, kwa mfululizo na kwa matarajio. Ukweli unapoachiliwa hautarudi bure. Ni Neno la Mungu linalotimiza ambalo limetumwa.