Hakuna Sheria ya Kifo |

Hakuna Sheria ya Kifo

Iliyoandika na HERBERT EUSTACE


Umeamua kuishi au unakubali kifo? Una kitu ya kusema juu yake? Mama Eddy aliambia Calvin Frye ya kwamba jukumu lake lilikuwa kuishi na akadhibitisha. Si Mungu milele anasema ” niwatengenezee moyo mpya na roho mpya: kwa nini mfe, enyi nyumba ya Israeli?” Kwani sina raha kwa yule anayekufa…..kwa hiyo jigeuzeni, na muishi” {Ezekieli 18:31-32}

Uko na kitu chochote cha kusema kama utazeeka au la? Unajua madaktari wa leo wanasema kwa wazi uzee ni ugonjwa na haina uhusiano na miaka na ni kama ugonjwa mwingine wowote. Hivyo umri, kuongezeka kwa miaka haiwezi chukuliwa kuwa hatari. Imani ya kibinadamu hatimaye ilifanya kukubali haya kwa sababu ilikuwa tayari, kwa mda uliopita, imeimarisha kama ukweli wa akili ya kibinadamu ya kwamba mwili, kwa sababu ya kubadilisha kwa seli zake, haina umri zaidi ya miaka saba. Miaka inamaanisa tajiriba, na tajiriba kwa wakati wote ina umuhimu na inapatiana uhai,haina uaribifu kamwe.

Shida yako inasema ya kwamba unazeeka? Basi kumbuka ya kwamba akili ambayo inasema unazeeka ndio akili ile ile ambayo inayosema mwili wako hauko zaidi ya miaka saba. “ Kutoka kwa mdomo ule ule kunatoka baraka na laana. Ndugu zangu, mambo haya hayatakiwi kuwa vile. Je, chemichemi inatoa maji matamu na chungu kwa wakati mmoja?” {Yakobo 3: 10-11}

Kukubali umri ni moja, useme mtu Fulani “pale” au mtu Fulani “hapa” nyumbani. Ukiona miti, wanyama au kitu chocote kama zinazeeka si unakubali umri? Hakuna kitu kinachoweza zeeka. Ukikubali pendekezo ya kwamba vitu vinazeeka na kuzeeka kwa hali ya kudhoofika, basi lazima kifo kije. Kama mwanasayansi ya Kikristo unajua ya kwamba hakuna sheria ya kifo. Kwa nini tena kuinamia pendekezo la sheria kama ile? Sheria pekee ya kifo ambayo iko ni sheria ya uhai ambayo ni sheria ya kifo kwa kila kitu kilicho kinyume.