Heshima ya Kazi na Biashara
PETER V. ROSS
Yeyote aliye na haja ya kazi atasaidika pakubwa kwa kuweka akilini ukweli kwamba ameumbwa kwa kusudi muhimu.ya kwamba kuna nafasi inayo mngoja, ya kwamba ufahamu wa Kimungu unafanya kazi kupitia kwake, na utamuongoza mahali ambapo kazi ile iko, na kumpatia uwezo wa kuifanya. Hatakiwi kuacha anapo gundua ukweli huu, lazima aufanyie kazi ukweli huu. Atajitayarisha kwa kazi, ataitafuta, akitarajia kuipata, na kuikubali anapoipata. Hatua za kibinadamu ni muhimu. Kusoma tu na kutafakari ukweli wa Sayansi ya Kikristo, ingawaje inavyohamasisha, haitoshi. Lazima ifanyishwe kazi.
Umeona picha za wavuta mawimbi wa bahari za kusini. Wanakaa kuegemea nguvu ambazo hazionekani na kupata msukumo wake. Wanapitia juu ya mawimbi wakiwa na uhakika kama vile wengine wanapita kwa Barabara za mjini.
Unaweza jenga uzoefu wa kuegemea kwa Akili ambayo inajua yote na kuikubalisha kukupatia mwelekeo. Hii Akili itakuzuia kufanya makosa, mbali na ajali. Itaachilia ndani yako mawazo ambayo itakuwezesha kujenga biashara bora zaidi, au kazi bora zaidi ambayo hujapata. Akili inaweza kuweka ndani yako mawazo ambayo itakuwezesha kuanzisha biashara mpya kabisa kwa nyanja ambayo haijachunguzwa, ambapo hakuna mashindano.
Kama wasioajiriwa wataegemea Akili, itawaelekeza mahali wanapohitajika. Kila mmoja anahitajika. Hakuna aliyewekwa duniani asiyekuwa na kazi. Mungu ako na kazi kwa kila mwanaume na mwanamke wake. Ako na jukumu muhimu kwa kila mmoja wetu, kusudi ambalo haliwezi choshwa.