Ujasiri na wema |

Ujasiri na wema

Iliyoandikwa na MARY BETH SINGLETERRY


Wema ni ubora muhimu wa Mungu. Miaka michache iliyopita kulikuwa na toleo la sanamu ya kiingereza ya hadithi ya Cinderella. Haikuwa katika maumbile ya katuni, ilikuwa yenye uhai wa waigizaji halisi. Ilitengenezwa vizuri. Ilipita kiwango cha hadithi ya kifahari kufikia kiwango cha thamani zaidi.

Katika toleo hili, mama, mama wa kweli wa Cinderella, alimwambia akiwa mtoto akumbuke wakati wowote kuwa na ujasiri na kuwa na wema.

Hio iliacha alama kubwa kwa mtoto yule mdogo, na ule ubora wa Mungu – ujasiri na wema – ilimuweka Cinderella salama katika wakati mgumu kama ule wa mama wa kambo na madada wa kambo. Na kwa sababu alikuwa mwaminifu kwa yale -licha ya tabia ya kikatili dhidi yake- aliinuliwa kutoka kwa hali ile kwa hali ya maajabu kama vile unavyofahamu hadithi hii. Toleo hii ilipatiana maana ya dhamani na ya kina, na huwa ninaifikiria mara mingi katika maisha yangu – kuwa na ujasiri na kuwa na wema.

Ufafanuzi wa wema ni ”tabia ambayo hufurahia katika kuchangia kwa furaha ya wengine.” Wema huambatana na upendo. Hio ni kweli kiasi gani. Wema ni sifa nzuri sana na hakika itaponyesha matatizo mengi ambayo tunaonekana kuwa nayo siku hizi. Kwa hivyo kuwa na ujasiri na kuwa mwema. Wema wote unawezekana, kwa sababu kwa kufanya yale unaangazia Baba – Mama Mungu wako.