Zaburi ya 23
Iliyoandikwa na Peter kutoka Australia
Somo la wiki hii la UPENDO linahamasisha has ana na lina muhimu. Nawashukuru wanaotayarisha somo la wiki. Kwa kweli wanatia moyo.
Juzi nilichukua mda nikisoma Zaburi 23 kwa undani. Yafuatayo ni maoni kadhaa yakifuatiwa na toleo lililobadilishwa:
{UPENDO WA KIMUNGU} ndio mlinzi wangu; napenda ufafanuzi wa jina la utendaji, “kulinda” ambaye ni kuongoza au kuelekeza kwa mwelekeo maalum. Sitahitaji kitu chochote Hitaji linaweza onekana kama tumaini la kibinadamu. Sitakuwa na tamanio za kibinadamu, Upendo wa Kimungu utaniongoza.
{UPENDO }hunilaza katika malisho yenye majani mabichi. Hii ina nguvu nyingi. Ninahimizwa na Upendo kujilaza au kujiwasilisha kwa utunzaji wa Mungu na kukubali utajiri wa Mungu.
{UPENDO} huniongoza kando ya maji yenye utulivu. Maji yenye utulivu huonyesha mahali pa uaminifu ambapo naweza tazamia upendo bila vishawishi na kuja kujua niko na umoja na Mungu
{UPENDO} unarejeshea moyo wangu {hisia za kiroho} kurejesha ni kurudisha kitu katika hali yake ya awali. Kuona ukweli wangu kama wa kiroho.
{UPENDO} huniongoza kwa njia za utakatifu. Ufafanuzi wa utakatifu: adabu,uadilifu, kutokuwa na hatia, Upendo unaniongoza. Nafuata nyayo za Upendo, kwa ajili ya jina lake, kwa sababu ya utukufu wa Mungu.
Ndio, hata kama napitia kwenye bonde Mama Eddy anafafanua bonde kama mfadhaiko na giza ya kivuli cha mauti, kivuli hakiwezi toa dutu. Kwa hivyo kifo sio cha ukweli. Sitaogopa hisia za uovu, akili za kimwili kwa sababu {UPENDO} unami; fimbo ya {UPENDO} fimbo ni silaha ya kulinda kondoo na inaonyesha ulinzi dhidi ya akili za kimwili na fimbo ya {UPENDO}. Fimbo inatumiwa kusaidia na kuongoza kondoo kwa hivyo inaonyesha Upendo na ulinzi wa Mungu juu yangu, zinanifariji. Mizizi ya Ugiriki ya jina ” kufariji” ni “kuita”. Pia kuhimiza .
{UPENDO} hutayarisha meza mbele yangu mbele ya adui zangu: Upemdo hunidumisha bila kujali vile akili za kibinadamu zinasema.
{UPENDO} hunipaka mafuta kichwani mwangu. Hii ni ilani ya zamani ya ulinzi. Aliye pakwa mafuta pia ni yule aliye chaguliwa, Kikombe changu kimejaa. Upendo hauna mwisho. Mahitaji yangu yamekidhiwa.
Kwa kweli wema na Fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu. Kwa sababu na fuata katika nyayo za upendo, wema na Fadhili kwa uhakika zitanifuata. Kwa hivyo nimezingirwa mbele na nyuma, ma upendo; na nitaishi kwenye nyumba {Ufahamu} wa {Upendo}milele.
Kuzingatia haya, nimebadilisha Zaburi hii kuisoma kama ifwatavyo:
{UPENDO WA KIMUNGU} unaniongoza; sitakuwa na matamanio ya kibinadamu, Upendo wa Kimungu utaniongoza.
{UPENDO} unanihimiza kuwa mnyenyekevu kwa utunzi wa Mungu. Nafuata katika nyayo za upendo na ninajua niko katika umoja na Mungu.
{UPENDO} ni, na umekuwa hisia za kiroho kwa siku zote: Nafuata katika nyayo za Upendo za heshima, uhakika wa maadili na usafi wa moyo. Sio kwa utukufu wangu lakini kwa utukufu wa Mungu.
Ndio, hata nikipitia msongo wa mawazo na giza, haya hayana dutu. Hakuna kifo. Sitaogopa hisia za kimwili au akili za kimwili: kwa sababu {UPENDO} unami; Fimbo ya { UPENDO} yanipa changamoto na kunilinda kutokana na akili za kimwili na fimbo ya {UPENDO} yaniongoza kusonga mbele, Upendo unaniita na kunipa nguvu.
{UPENDO} hunidumisha bila kujali mapendekezo ya akili za kimwili. Mahitaji yangu yote yamekidhiwa. {UPENDO} Unanilinda. Upendo umenichagua. Upendo hauna mwisho.
Kwa sababu nafuata katika nyayo za Upendo, wema na Fadhili zitanifuata mimi. Nimezingirwa na Upendo: na nitaishi katika { Ufahamu} wa {UPENDO} milele.