Sehemu kuhusu Meno
Kutoka kwa mahubiri na Makala iliyoandikwa na DORIS WHITE EVANS
Tulisikia hadithi ya kuvutia juzi kutoka kwa mwanasayansi, rafiki yetu. Alipata kumuona rafiki yake wa zamani baada ya miaka mingi sana na akaongozwa kusema juu ya meno yake vile ilivyokuwa nzuri. Hakuwa ameitazama mbeleni. Na akasema, “Hio ni hadithi ya kuvutia; na ningependa kuwaambia ni yapi yaliyonifanyikia.” Alisema amekuwa na matatizo ya meno yake na akaenda kwa daktari wa meno. Daktari akasema, “ Meno yako yote yamebadilika rangi na imeoza , na yanahitaji kung’olewa mara moja.” Na akasema, “Sitaki kufanya kitu chochote juu yake sasa hivi,nitawasiliana nawe baadaye.” Na akampelekea Mungu shida ile. Alikataa mawazo yake kupotoshwa na matibabu ya kimwili yakijiita matibabu ya meno. Na akaamua kumuona binadamu aliyekamilika kila mahali. Alipata kifungu kizuri katika kitabu cha Nyimbo za Suleimani iliyosema kwa kina, “Meno yako ni kama kundi la kondoo; na hakuna ambaye hana uzao; wote wakiwa wamekamilika.” Akaanza kusoma maandishi ya Mama Eddy, na akapata ukweli wa kuvutia: Ya kwamba maneno mawili yalikuwa yameshikana katika maandishi ya Mama Eddy. Haya maneno yalikuwa “utengano” na “kuoza “ Alivyoendelea kufikiria juu yake kwa undani, alitambua alihitaji kurudi kwa tajiriba yake na kuona ya kwamba hakujawai kuwa na utengano kutoka wakati aliingia duniani. Alihitaji kupanguza imani ya kwamba kulikuwa na hali yoyote ya utengano ambayo ishawai kuwa maishani mwake. Alifanyia kazi haya kwa miezi mingi, akimtazama mwana aliyekamilika wa Mungu kila mahali alienda, akihakikisha hakumuona mtu yeyote asiye na upendo, asiye na subira, mgonjwa, au aliye na chuki, akikataa kuachilia makosa kupotosha mawazo yake. Baada ya miezi mingi, alirudi kwa daktari wa meno. Daktari akamtazama na akasema,” Hii sio meno ile iliyokuwamo,” kwa sababu yalikuwa yamekamilika, yanang’aa na nzuri. Na yalionekana kwa mdomo wake kama hayajaonekana mbeleni, na hakukuwa na alama yoyote ya kuoza.
Fikiria juu yake. “Utengano” na “kuoza” kila mara yameshikana katika maandishi ya kiongozi wetu. Rudi kwa mawazo yako na uhakikishe haujahifadhi picha ya utengano ambayo ilikaa kufanyika kwako miaka ya awali, ambayo unaweka karibu ambapo inaweza toka na kuleta picha mbaya, moja ambayo Mungu hakuiumba, ambayo Mungu haiungi mkono na kwa hivyo, kwa ufahamu safi wa Mungu inaweza vunjwa na kuharibiwa.