Mtazamo wa Mwana Sayansi ya Kikristo |

Mtazamo wa Mwana Sayansi ya Kikristo

na SUE H. MIMS

KUTOKA KWA TOLEO LA JUNI 7 1900 LA Christian Science Sentinel


Katiba

“Zingatia maua ya uga, vile yanavyo kua; hayafanyi kazi ngumu, wala hayasokoti: na bado nawanenea, Ya kwamba Suleimani na ukuu wake hakuwa amevalishwa kama mmoja wa haya. Kwa hivyo, kama Mungu anawavalisha nyasi ya uga ambayo leo iko, na kesho inawekwa kwenye jiko, zaidi hatawavalisha nyinyi, enyi wnye Imani ndogo?” – Yesu.

“ Mtu aliye na jembe” “hataiweka chini.” Anasimama kwa nyakati zote kama mwenye huzuni, mwenye masikitiko, katika uchunguzi, wakati upi? wapi? Yeye ni kilele cha shida za wanadamu. Jibu ni nini? Ushirika wa kijamii una jibu? Nadharia ya sifa ya mali iko na jibu ya hali hii? Hapana! Au ushuru, au serikali ya kibinadamu? Hapana! Kwa kiwango chochote cha kibinadamu msingi wa usawa wa leo ni ukosefu wa usawa wa kesho. Kuna suluhisho lolote? Ndio!

Kuna uovu moja chini ya jua, ambao kuongeza sauti kwake ni dhambi, umasikini, ugonjwa, kifo; uovu huu mmoja ni hisia za uongo, au uongo juu ya Mungu, mwanadamu, ulimwengu, na uhusiano wake. Hii hisia ya uongo ya kimwili Yesu alitupilia kama uongo, muongo, na baba wa uongo, na “muuaji kutoka mwanzo,” udanganyifu bila sababu; kwa Mungu, Ukweli, Sababu, Muumba.

Kuna dawa moja kwa huu uovu. Ni kujua ukweli juu ya Mungu, mwanadamu na ulimwengu. Yesu alidhibitisha ya kwamba ufahamu wa ukweli ungeangamiza kazi za shetani, au mmoja aliye muovu. “ Mtu aliye na jembe.” Alijibiwa milele wakati Yesu aliwalisha umati kwa kutambua uhusiano halisi wa Mungu na binadamu kama akili ya milele ambayo daima ipo, dutu ya kweli, chanzo kisichoshindwa, ambapo ni mwanzo wa yote. Aligeuza msimamo ambao ni wa kumtazama mwanadamu. Alisema, Usimuite binadamu yeyote baba duniani: mmoja pekee ndiye baba ambaye yu juu mbinguni.” Yohana na Paulo wanatangaza, “ sasa tu wanae Mungu, na warithi {sio wa umasikini au ugonjwa} lakini warithi na Kristo.” Kwa nguvu, ukuu na mamlaka. Yesu alisema, “Tazama juu,” na mazao yako tayari,” yako katika Akili, sio kwenye ardhi, wala kutoka kwake.

Mwanadamu kama kiumbe cha kiroho ni umbo la roho na ako na mamlaka juu ya hali zote za kimwili. Katika habari ya kweli ya kiroho ya uumbaji. Mungu aliumba kila “mmea wa uga kabla uwe duniani, na kila mmea wa uga kabla kukua,….na hakukuwa na mwanadamu kulima ardhini.”

Isaia alisema, “Achana na mwanadamu, ambaye pumzi yake iko kwenye mapua yake, atawajibikiwa aje?” na Paulo akasema, “ Wana wa mwili, hawa sio wana wa Mungu,” na “kutoka sasa hatumjui mtu yeyote wa mwili,” na Yesu akasema, mtaujua Ukweli, na Ukweli utawaweka huru.” Kuamka kutoka kwa ndoto ya Adamu, uwepo wa kimwili, kuingia kwenye uwepo halisi wa uwepo wa kisayansi na kumpata binadamu ambaye hajawaianguka, msafi na huru, akifanyisha kazi urithi wake wa kiroho, utawala, ni kumpata suluhisho la kweli latatizo la maisha.

Mazingira halisi ya mwanadamu ni wema wa milele, lakini kama watoto vipofu masikini, wanadamu wamekuwa wakitafuta yale ambayo tayari yako hapa.

Iko wapi bahari, Samaki wakalia,

Kama walipokuwa wakiogelea kwenye usafi unaoonekana,

Tumesikia juu ya mawimbi zamani,

Na tunatamani kutazama rangi ya samawati kwenye maji,

Wenye hekima hutuambia juu ya bahari isiyo kuwa na mwisho –

Oh! Nani anaweza tuambia juu ya yale?

Ndege wa shairi walipaa mwangazani wa asubuhi

Na wakaimba, wakisimama kwenye mabawa yenye jua;

Na huu ndio ulikuwa wimbo: Naona mwangaza,

Natazama kwenye dunia ya vitu vizuri,

Zikipaa na kuimba kila mahali,

Bila mafanikio nimefanya juhudi kupata hewa,

Kwa hivyo Sayansi ya Kikristo inasema kwa kila mtu: “Amka uliyelala,” na Kristo, Ukweli wa Uwepo utang’aa juu yako.

Tazama, Mungu yuko hapa. Yuko kila mahali, na tunaishi na kusonga, na tuna uwepo wetu ndani mwake; Bahari ya Upendo usioisha inazingira kila kitu, mazingira ya ufahamu wa kimungu unafumbua kwetu yale “ macho haijaona wala kusikia, wala kuingia katika roho ya binadamu .” Upendo wenye uhai wa milele haubadiliki, muziki wa duara bado unaimba uwiano wa uwepo, kama wakati “Nyota za asubuhi zilipoimba Pamoja na wanae Mungu wakapiga kelele kwa shangwe.” Tunatakiwa tu kujua ukweli wa Uumbaji na kutosheka tu tunavyoamka katika ufananisho wa kimungu.