“Posho Ya Daima” |

“Posho Ya Daima”

KUTOKA KWA TOLEO LA SENTINELI YA SAYANSI YA KIKRISTO LA NOVEMBA 8, 1924 NA FRANCIS M. GORRELL


Kuna watu wengi duniani leo wanaofanya uhai wao kuwa wa masikitiko kwa kuhofia juu ya kesho na madai yake. Wana wa Israeli walisoma somo la kutafuta ugavi wa kila siku kupitia kukusanya mana ambayo walipatiwa siku kwa siku. Hakuna kuhodhi bure, hakuna kukimbilia kwa wazimu, iliyokuwa imekubalishwa, ni tu ni kazi ya bidii na kuendelea kukusanya kipimo cha kutosha kukidhi mahitaji ya siku. Kulikuwa na wito wa kazi ya kila siku, kwa kufanya bidi ili kukidhi mahitaji ya kila siku; na ili mradi walihitaji ushahidi wa uridhi wake Mungu na ugavi , na kukubali kwa hiari masharti yake, ndio tu waliweza kudumishwa.

Mwanafunzi wa Sayansi ya Kikristo, kupitia ufahamu wake wa uwepo wa milele wa wema na upendo wa Mungu, Baba-Mama, anatumia kwa shukrani kukusanya na kutumia mawazo ya wema yanayo mjia kwake kila siku, akijua hizi dhihirisho za upendo wa kimungu zinaendelea, hazishindwi, na hazina kipimo. Katika mstari wa mwisho wa sura ya mwisho ya wafalme wa pili tunasoma, “Posho lake ni la kuendelea aliyopatiwa na mfalme, kiwango cha kila siku, siku zote za maisha yake.” Wanasayansi ya Kikristo walio inuliwa kutoka kwa gereza la hofu na dhambi na kukata tamaa kama Jehoiachin, ambaye maneno haya yaliandikwa, aliinuliwa kutoka kwa gereza la kimwili la mfalme wa Babiloni, wakitambua uhuru wao kutokana na kifungo cha kimwili, vizuizi vya kibinadamu, na uchungu wa kimwili, kutosha kungojea kila siku kupata “kiwango cha kila siku?” Kuna uwezekano ya kwamba, katika uso ya yale yote tumefanyiwa hapo awali, bado tunatafuta leo kiwango cha kesho? Tunashangaa kama ujasiri tutakao hitaji kwa kazi ya kesho utatosha? Tunauliza wingi wa uvumilivu ambao majaribio ya kesho yatahitaji? Tunatumai bila kufafanua ya kwamba nguvu za kutosha kwa namna fulani zitatosha kutimiza majukumu ya kesho? Tunauliza kwa hamu kama kutakuwa na fedha za kutosha kutimiza majukumu ya kesho?

Sikiza tena maneno matamu ya ahadi, “ Kiwango cha kila siku, kwa siku zote za maisha!” Basi natuweke kando kila tashwishi na hofu na wazo la wasiwasi, na kwa shukurani na kunyenyekea tukusanye mana ya leo. Inamaanisha bidii na ujasiri na imani kufanya haya; inamaanisha ustahimilifu na uvumilivu na maombi. Lakini hakuna kutokuwa na uhakika, kuchelewa, la ukosekanaji katika matokeo; kwa sababu kuna mana ya kutosha kwa wote, – kuna wingi wa ugavi wa mawazo ya Mungu kukidhi mahitaji yote. Kiongozi wetu anatuambia katika “ mkusanyiko wa maandishi” {Ukurasa 307}: “ Mungu anatupatia mawazo yake ya kiroho, kwa mbadala, yanatupatia ugavi wa kila siku. Kamwe usiulize ya kesho: ni ya kutosha kwamba Upendo wa Kimungu ni uwepo wa karibu; na ukingoja, bila kusita, utakuwa na yote unayohitaji kila wakati.”

Kwa kugeuka mbali na kimwili au ijulikanayo kama vyanzo vya kimwili vya ugavi, tutapata utambuzi tosha wa wingi ambao Mungu hupatiana. Ufahamu wa Mungu kama uwepo wa milele, aishiye milele, na anayepatiana milele huondoa wazo la ukosefu wowote wa udhibitishaji wa wema. Tukipumzika kwa utulivu katika uhakikisho waumiminikaji wa upendo wa Kimungu, tunapata kwa shukurani kila wazo la wema kama Malaika wa Mungu, na kuharakisha kufuata yule Malaika katika ukamilifu wa furaha na amani na wingi.

Mungu ametupatia , “kwa utajiri vitu zote kufurahia;” na kila wazo la hofu juu ya wakati ujao ni tashwishi juu ya zawadi yake ya Upendo. Mungu hashindwi kamwe. Kushindwa kutambua wingi wa nguvu zake na ugavi ni kushindwa kwetu kumuelewa kikamilifu, na matokeo ya kutokuwa na nia ya kutazama Roho pekee kama chanzo cha ugavi wa kila hitaji, ingawa ndogo au kuu. Upendo wa Kimungu hauwezi isha. Wote wanaweza kula hii mana, ukamilifu wa wingi wa Upendo, na bado kuna wingi kwa wote.

Chochote ambacho ni hitaji, iwe ni upendo, uvumilivu, ujasiri, nguvu, au ugavi wa kila siku, utakidhiwa kupitia utambuzi wa wingi wa Mungu na utayari uliokamilika wake wa kuwapatia kila wanaomtafuta “kiwango cha kila siku, kwa siku zote za maisha yao.” Yote ambayo tunahitaji kesho itakuja, tukitumia kwa hekima mawazo ya wema yanayotujia leo, tukitafuta daima kuongeza na kubariki na kurahisisha njia ya mwingine; kwa sababu kulingana na mafundisho ya Sayansi ya Kikristo, hatuwezi pokea isipokuwa kwa kushiriki wingi ambao ni utambuzi wetu.