Mwanasayansi ya Kikristo juu ya meli ya Titanic |

Mwanasayansi ya Kikristo juu ya meli ya Titanic

Iliyoandikwa na LIEUT. C. H. LIGHTOLLER, OFISA WA PILI, MELI TA TITANIC


Ni vigumu kueleza tajiriba inayofuata, lakini wanafunzi wa Sayansi ya Kikristo wataona ndani yake ya kwamba kukubali ukweli ilifanya ushindi dhidi ya hofu kuwezekana, na kwamba Kanuni ya Kimungu inaweza tegemewa wakati wowote.

Wakati meli ya Titanic ilikuwa inazama, wakati ule wote nilikuwa nikifanya kazi kwenye mashua, nilishikilia ukweli hivyo kuondoa hofu yote. Sijifanyi kuwa ya kuwa mtu yeyote anaweza zama kutoka kwa meli Katikati ya usiku, kati ya bahari ya Atlantiki, na aweze kuondoa hofu bila kufanya kazi kwa bidii. Ilikuwa kazi ngumu, na bado hali ambazo zilipatikana pande ya bahari zenyewe zilikuwa dhihirisho la kazi ya Ukweli, kwa sababu hakuna shida yoyote ilipatikana, na mashua zote zikatolewa, ya mwisho, iliyokuwa upande wake wa chini wa kukujwa, ikipaa kutoka kwa staha ya meli.

Niliona ya kwamba kazi yote ya kimsingi ilikuwa imeisha, kwa hivyo kutoka mahali nilipokuwa kwenye vyumba na juu ya Daraja, nilitazama mbele na kutembea nikielekea kwenye maji. Kuingia kwa ghafla katika maji baridi kwa sekunde kidongo kulishinda mawazo yote, na nikaelekea bila kuona kuelekea kwenye kiota cha jogoo, ambacho kiko mwishoni, na kilicokuwa kwa wakati ule juu ya maji. Mara hiyo hiyo nilijipata nimevutiwa kwa nguvu nyingi dhidi ya kihungi kinachoziba kipulizi cha hewa, kipulizi kikubwa kinacho elekea kwenye fadhili ya meli. Katika msimamo huu nilienda chini ya sitaha Pamoja na meli.

Nataka kusisitiza kwa kina pointi hii, ya kwamba mara tu nilipokusanya mawazo yangu, baada ya kuenda kwenye maji, nakumbuka nikijisemezea, “ Sasa, nitaona yale ambayo nimesoma katika Sayansi ya Kikristo.” Hakuna tashwishi ambayo iliingia akilini mwangu juu ya uwezekano wa kuokolewa kwangu; yaani, juu ya uwezo wa nguvu za Kimungu kuniokoa. Nafikiri naweza sema kwa wazi kwamba na mawazo haya hofu yote iliondoka. Ilikuwa wakati huu nilipovutwa kwenye maji, nikijua ukweli na nilipokuwa chini ya maji, haya maneno kutoka kwa Zaburi 91 yakanijia kwa usafi na nikakaa kutambua maana yake halisi: “Atawapatia Malaika wake udhibiti juu yako.”

Mara hiyo hiyo, nafikiria, nilirushwa kutoka kwa kipulizi, na nikaja kupata kipande cha ubao mkononi mwangu, ambao ulikaa kushikanishwa juu ya faneli na waya. Wakati wa pili nilienda chini, nikiushikilia ukweli, na tena nikajipata kwenye uso. Kando yangu mlikuwa mashua yenye kukujwa. Niliishikilia, lakini sikufanya juhudi ya kupanda.

Nataka ieleweke ya kwamba wakati huu katika maji, ukweli ulinijia kwa utulivu na usafi ya kwamba kulikuwa na nguvu za kimungu ambayo ingetumiwa kwa namna ya vitendo, na pia ilionekana kawaida kwa kikamilifu kutegemea nguvu hii ikiwa na ufahamu wa kiroho ambao unazungumziwa katika Bibilia, na ambao unaelezewa katika Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko, iliyoandikwa na Mama Eddy. Sasa, kuzama kwa meli kubwa kama Titanic, kulikuwa kushinda kwa hofu kubwa ya kunyonywa na maji, na wakati huu faneli ya mbele ikaanguka, na ikarusha mashua, nami, na manusura wengine kama fiti ishirini mbali na meli kwa hivyo kwa kunyonywa hatukusikia kitu.

Watu kama thalathini tulielea usiku uliobakia kwenye mashua iliyokuwa imegeuka juu chini. Asubuhi tulipata mashua mbili zikielea karibu ambazo zilituchukua. Nilikuwa mtu wa mwisho wa Titanic kuingia meli ya Carpathia. Mmenyuko au adhari kutoka kwa uzamaji, ambao nilihakikishiwa kwa kuamini ungefanyika, hakukuwa; ingawa mshangao umeonyeshwa na wengi, inathibitisha ya kwamba “kwa Mungu yote yanawezekana.”