Somo la Upendo |

Somo la Upendo

Kutoka kwa Kumbukumbu za dhamani Na CLARA SHANNON, CSD


Wakati ninaposoma sura juu ya “Wapende adui zako” katika mkusanyiko wa maandishi, tajiriba moja ambayo kiongozi wetu alipata mwakani 1899, na ambayo nilirekodi, nakumbuka akifundisha mafundisho katika sura ile, ikidhihirishwa katika maishani mwake. Mmoja wa wanafunzi wake wa hapo awali ambaye alikuwa ameonyesha uadui mkubwa dhidi yake na alikuwa anamsaliti na kutoa uongo juu ya tabia yake ilishughulikiwa kwa njia hii. Asubuhi moja kama Mwalimu wetu mpendwa alikuwa akiandika barua, aliniita na kusema, “Ni kwa nani unaweza fikiria nimeandika?’’ Kutokana na mtazamo wa sura yake nikasema, “ Nadhani kwa mtu Fulani ambaye hakuna mwingine ambaye anaweza mwandikia!” Alafu akasema, “ Ni Fulani, na nimemkaribisha kuja kuniona. Nimempatia siku mbili achague wakati ambao ni bora kwake, na nimemuuliza kunipasha barua kunijulisha siku.” Akaisoma barua kwangu na akaniambia niiweke stempu. Nikasema, “Mama, unawezaje mwandikia, ukijua anafanya awezalo kukudhuru, na hafichi, lakini anaongea kukuhusu?’’ Akaniambia, “ Lazima ujifunze kumpenda yule mwanamke.” Nikasema, “Unampenda?” “Ndio, na ninajaribu kumbariki! Kama mimi na wewe hatumpendi, nani atampenda?”

Kwa barua ile Mama Eddy hakupata majibu. Siku ya pili ilipowadia, kabla ya kuenda kwa matembezi yake, akavalia vazi lake maalum na kuagiza gari lake kuwa mlangoni tayari kumpeleka kwa matembezi yake lisa limoja mbele kuliko kawaida, ili kuwa nyumbani mapema kabla ya mgeni wake kufika. Kabla ya kuondoka, kiongozi wetu aliagiza gari lingine litumwe kwenye stesheni kumpokea mgeni. Wakati alipokuwa anavalia glovu mikononi mwake kabla ya kuingia kwenye gari lake, akaniita kutoka kwa maandishi yangu na akasema, “Utaahidi kitu?” Nikasema, “ Bila shaka, nitaahidi kama ni kitu ninachoweza kufanya.” Akasema, “ Kama Mama—atakuja kabla nirudi, nataka umsalimie kwa ukarimu.” Nikasema, “ Ndio, Mama, nitafanya vile.” Alafu akasema, “Kwa Upendo?” kwa ishara ya uchunguzi katika sauti yake. Jibu langu lilikuwa, “Nitajaribu.” Alafu akasema, “Ki mbinguni?” Nikajibu, “Nitaenda kwenye chumba cha juu na kumuuliza Mungu kunisaidia kafanya haya na kunionyesha vile nitafanya.” – kwa ukarimu, kwa upendo, na kimbinguni!”

Nikaenda kwa chumba changu na kuomba kwa dhati, kwa Upendo wa Kimungu kunisaidia, kwa sababu ilikuwa sahihi kwake kuhisi haya, ilikuwa ni sahihi kwangu kuyaonyesha. Kwa mda mfupi nikahisi tamanio la kuja kwake, na nilikuwa tayari kumkaribisha kwa njia ya kibinguni ambayo nilijua, kwa sababu nilijua baraka iliyomngoja kupitia mahojiano na kiongozi wetu na wema mkuu ungetokea.

Kiongozi wetu alirudi kutoka matembezi yake lisa limoja mapema kuliko kawaida yake, na wakati aliposhuka kutoka kwa gari lake, alisema, “Amekuja?” Nikasema, “ Hapana Mama.” “Usijali,” akasema, nitamngonja chumbani.” Wakati huu gari lilikuwa limetumwa mara ya pili na ya tatu kupatana na gari za moshi tatu zikifuatana.

Wakati wa mwisho ilikuwa saa za kuchelewa na kulikuwa na giza zaidi ya yeye kuja, na kiongozi wetu aliketi sebuleni kumngoja, na baada yake, akaamka kurudi kwenye chumba cha kukaa, na kusema, “ Oh ni baraka kuu aje ya upendo angepokea! Ingemuokoa na kumfariji!” Mimi pia nilihisi huruma kwake kwa kupoteza nafasi kama ile na baraka kuu. Nilijifunza somo la upendo ambalo sijawai sahau.