Picha Iliyo ndogo ya Yusufu
Mafundisho yaliyotolewa juu ya siku ya Bwana asubuhi, Julai, 24, 1881, na Charles H. Spurgeon katika thehebu ya Metropolitan Newington.
“BWANA ALIKUWA NA YUSUFU.” MWANZO 39:2
Maandiko kwa mara nyingi hukusanya maisha ya mwanadamu kwa sentensi moja. Hii ni hadithi ya Yusufu iliyoandikwa kwa hamasa – “ Mungu alikuwa naye,” hivyo Stefano akashahidi katika hotuba yake ya kufana iliyorekodiwa katike Mitume 7:9. Hapa kunayo hadithi ya Ibrahimu – “Ibrahimu alimwamini Mungu.” Juu ya Musa tunasoma, “Musa alikuwa mnyenyekevu.” Tazama maisha ya agano jipya, kama ya Yohana Mbatizaji, na unayo katika mstari – “Yohana hakufanya miujiza, lakini mambo yote aliyonena kuhusu Yesu yalikuwa kweli.” Jina la Yohana – “Mwanafunzi aliyependwa na Yesu” – inaweza kuwa kama jiwe la ukumbusho kwake. Inaonyesha mtu na historia yake. Maandiko matakatifu yanafanya vyema katika onyesho kuu la picha hizi ndogo! Michaelangelo anasemekana kuchora picha kwa mchoro mmoja wa kalamu, na hivyo Roho wa Mungu unavyochora maisha ya mtu kwa sentensi moja. “Mungu alikuwa Pamoja na Yusufu.” Tazama, hata hivyo, kwamba picha za maandiko zinatuonyesha sio nje pekee, lakini ndani mwa maisha ya mtu yule. Mwanadamu huangalia umbo la nje, lakini Bwana huangalia moyo, na kwa hivyo ufafanuzi wa maandiko sio wa maisha yanayoonekana pekee, lakini ya maisha yao ya kiroho. Hapa tunaye Yusufu kama vile Mungu alivyomuona, Yusufu wa kweli. Kwa nje haikuonekana kwa wakati wote ya kwamba Mungu alikuwa naye, kwa sababu Yusufu hakuonekana mtu aliyekuwa na ufanisi. Lakini ukija kuangalia kwenye nafsi ya mtumishi huyu wa Mungu, utaona umbo lake la kweli – aliishi katika ushirika na Mungu, na Mungu akambariki –“ Mungu alikuwa na Yusufu na alikuwa mtu mwenye ufanisi.”
Marafiki wapendwa, unaweza pendelea aje kuona vile biografia yako ya ndani itachorwa? Nafsi yako itaonekana aje, ikionekana kwa karibu mbele ya dunia yote kwa matamanio, mapenzi na mawazo? Maisha ya wengi yanaonekana mema kwa maandishi lakini ndani mwake mwandishi hakuingia ndani, au labda hangeingia ndani kama angekuwa na hofu kufanya vile. Hufikiriwa kihekima, katika kuandika kuhusu maisha ya mtu, kuficha mambo Fulani. Hii inaweza kuwa ya kumaakinika kama nia ni kulinda sifa, lakini ni mbali na ukweli. Roho wa Mungu hafichi makosa hata ya wale tunaowaenzi, lakini huandika kwa kikamilifu, kama Roho wa Ukweli, vile yuko. Mtu ambaye, juu ya wote alikuwa , “ mtu aliyeutafuta moyo wa Mungu,” alikuwa kwa kiwango , na makosa makuu, na akafanya kosa moja mbaya ambalo litabaki kwa wakati wote kama dosari katika tabia yake. Ilikuwa katika Daudi kushikilia kwenye imara na kusipotingisika juu ya Bwana Mungu na mapenzi ya kufanya mambo kwa usahihi – na kutubu kwa dhati wakati alipokosa, ya kwamba Bwana alimuona kama aliyetafuta moyo wake hata kama alimuadhibu kwa uzito kwa makosa yake. Daudi alikuwa mtu mwenye roho ya kweli hata kama alianguka kwenye makosa na ni moyo wa Daudi uliochorwa. Kwa hivyo hapa, Roho haangalii Yusufu sana kama mtoto wa kipenzi, au kama Waziri mkuu wa Misri, lakini kama Yusufu ndani na kweli, na kwa hivyo anamuelezea “Bwana alikuwa na Yufufu.” Hili umbo la Yusufu linatukumbusha juu ya Bwana wetu, yule Yusufu mkuu, ambaya ni Bwana juu ya Dunia yote kwa ajili ya Israeli.
Petero, katika mahubiri yake kwa nyumba ya konelias, alisema juu ya Bwana ya kwamba, “ Alitembea akitenda wema na kuponya wote waliokuwa wamefinyiliwa na shetani; kwa sababu Mungu alikuwa Pamoja naye.” Kama vile ilivyosemwa juu ya Yusufu! Ni ajabu ya kwamba maneno yaleyale yataelezea juu ya Yesu na Yusufu; mookozi aliye kamili na kiongozi wa kijamii asiyekamilika! Wakati mimi na wewe tunapo kamilishwa katika neema ya Kimungu, tutavalia umbo la Kristo na ambacho kitafafanua Kristo kitatufafanua! Wale ambao wataishi na Yesu watabadilishwa na ushirika wake mpaka wawe kama yeye. Kwa akili yangu, ni vizuri sana kuona kufanana kati ya mzaliwa wa kwanza na familia hiyo nyingine; kati ya mtu wa kawaida, Adamu wa pili na watu wale wameinuka katika uhai wake na kitu kimoja naye. Hii Bwana kuwa nasi ndio urithi wa watakatifu wote, kwani ni nini baraka ya mitume katika waraka lakini tamanio ya kwamba Utatu wa Mungu uwe nasi? Kwa kanisa la Roma, Paulo anasema, “ Sasa Mungu wa amani awe nanyi nyote.” Kwa kanisa la Korinitho, anaandika, “Neema ya Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, uwe nanyi nyote. Amina.” Kwa Wathesalonike, anasema, “ Mungu awe nanyi nyote.” Si bwana wetu mtukufu alisema, “Niko nanyi daima, mpaka mwisho wa dunia?’’ Nitawasalimu vizuri aje asubuhi hii ila kwa manene mazuri ya Boazu kwa wavunaji, “Bwana awe nanyi?’’ Ni jibu gani nzuri unayoweza nipa ila, “Mungu akubariki?’’
Juu ya milima ambayo inaunda ukuta wa nyuma wa Mentone, siku moja, nilipata kupatana na Mkristo wa Quaker katika mavazi ya kawaida.Alikuwa anawapenda kwa moyo wa upendo wale wote waliompenda Yesu. Alinisalimu na tukapata ushirikiano mkuu wa kiroho. Tulipoachana, nilisema, “Rafiki, Bwana awe nawe.” Na akajibu, “ Na roho yako,” akiongeza, ni kiwango cha kwanza cha ibada nishawaitumia.” Kwa kweli, vile mara nyingi tunavyoweza kutumia kwa roho zetu, ndivyo vizuri, kwa sababu hakuna anayeweza kupinga! Hivyo ndivyo ninavyosema kwenyu nyote siku ya leo, “Bwana awe nanyi!” Na ninajua mnajibu, “ Pia na roho yako.” Na mpate matamanio yenyu mmeyapata, kwa Roho Mtakatifu kuwa na roho yangu, niweze kuongea maneno yanayoweza kufanya mioyo yenyu upya.
Sasa natufikirie juu ya Yusufu natuone nini ambacho tunaweza kusoma kutoka kwake. “ Bwana alikuwa na Yusufu.” Natuzingatie, kwanza, ukweli; pili, Ushahidi wa huu ukweli; na tatu, matokeo ya ukweli. Kwanza, tutapitia maisha ya Yusufu na kuona UKWELI – “Bwana alikuwa na Yusufu.” Mungu alikuwa mkarimu kwa Yusufu akiwa mtoto. Babake alimpenda kwa sababu alikuwa mwanaye wa uzeeni wake na pia kwa sifa zake nzuri alizoziona kwake. Kabla awe na umri wa miaka 17, Mungu alikuwa amenena naye katika ndoto na maono ya usiku ambayo tunasoma kwamba, “Ndugu zake walimuenzi; lakini babake aliutazamia msemo akisema.” Wapendwa vijana, sio kwamba lazima Mungu aje kwenye ndoto zenyu, lakini ako na njia zingine za kuongea na kijana Samueli. Unakumbuka alisema, “Samueli, Samueli,” na mtoto yule mpendwa akajibu, “Ongea, bwana, mtumishi wako anakusikiza.” Na uwe wa kujibu kwa njia ile kwa wito wa Mungu kwa neno lake. Ilikuwa ni nafasi ya furaha juu ya wengine wetu kabla kuacha kuwa vijana kupata mawasiliano ya ukarimu kutoka kwa Mungu – Alituelekeza kwa toba, alituelekeza kwa imani katika Kristo na kufumbua upendo wake katika mioyo yetu kabla kutoka katika madarasani ya shule na uwanja wa michezo! Wanaaza vizuri wanaoanza mapema katika Kristo! Atakuwa nasi mpaka mwisho kama tuko naye kutoka mwanzo! Kama Yusufu hakuwa kijana mcha Mungu, hangekuwa mtu mkarimu. Ukarimu wa Kimungu ulimfanya kutofautiana na ndugu zake katika ujana wake, na akawa mkubwa wao siku zake zote. Kama tutakuwa wakarimu tukiwa watoto, tutakuwa na uhakika ya kwamba Bwana atakuwa mkarimu kwetu hata kama tutaishi mpaka uzeeni kuwaona watoto wa watoto wetu.
Unyenyekevu wa mapema ni uwezekano wa unyenyekevu unaostahili. Furaha ni kwa wale wanao Kristo asubuhi, kwa sababu watatembea naye siku yote na kupumzika naye jioni. “Bwana alikuwa na Yusufu. Wakati Yusufu alikuwa nyumbani na hakumtoroka wakati aliponyakuliwa kutoka kwa babake na nyumbani mwake na kuuzwa kama mtumwa. Chungu ni maisha ya mtumwa katika nchi yoyote na ilikuwa mbaya zaidi katika siku zile. Tunaambiwa na Stefano ya kwamba mababu, walikuwa na wivu, wakamuuza Yusufu Misri – lakini Bwana alikuwa naye – hata wakati Yusufu alikuwa anauzwa Bwana alikuwa naye. Lazima ilikuwa safari ngumu sana kwake kupitia jangwani, akisukumwa na Waishmaili wagumu, labda wakiwa kwa kikundi, kama vile watumwa wanafanywa katikati mwa Afrika leo. Na Mungu alete kikomo kwa mfumo huu wa chuki! Mtoto huyu mlainifu wa baba mwenye mapendeleo, aliyekuwa amevalishwa vazi la ukuu la rangi nyingi, sasa lazima avae nguo ya mtumwa na kutembea katika jua kali kwenye mchanga wenye joto. Lakini kamwe mtumwa alikuwa mnyenyekevu kwenye ukatili. Alivumilia kwa kumuona asiyeonekana. Moyo wake ulidumishwa na ujasiri katika Mungu wa baba yake, Yakobo, kwa kuwa” Yehova alikuwa naye.” Nafikiri namuona katika soko ya watumwa akiwa tayari kwa kuuzwa. Tumesikia kwa hofu yenye kutetemeka mtumwa anavyotazama nyuso za wale ambao wanaowanunua. Atapata bwana mwema. Atakaye mnunua atamtendea kama mtu, au atamtumia vibaya kuliko mnyama? “Mungu alikuwa Pamoja na Yusufu” alipokuwa amesimama pale ili kuuzwa na kuanguka kwenye mikono miema!
Alipopelekwa kwa bwana wake na kupatiwa majukumu, bwana alikuwa na Yusufu. Nyumba ya Mmisri kamwe haikuwa safi, yenye ukweli, na yenye kuheshimika mbeleni. Chini ya uongozi wa Yusufu ilikuwa kwa kisiri hekalu ya ibada na kwa kuonekana makazi ya kutosheka na ujasiri. Mtumwa yule Myahudi alikuwa na ukuu wa tabia juu yake ambao kila mtu aliona, na sana sana Mkubwa wake, kwa jili tunasoma – “Bwana wake aliona ya kwamba Bwana alikuwa naye na ya kwamba alifanya yote ili kufanikiwa mikononi mwake. Na Yusufu akapata neema katika machoni mwake, na akamtumikia – na bwana wake akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake na kila kitu alichokuwa nacho akakiweka mikononi mwa Yusufu. Na ikaja kupita kutoka wakati alimfanya msimamizi katika nyumba yake na juu ya kila kitu alichokuwa nacho, ya kwamba Mungu alibariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu; na baraka ya Bwana ikawa juu ya kila kitu kilichokuwa kwa nyumba na kwenye shamba.” Bidii ya Yusufu, uaminifu na upole ukamshinda bwana wake. Oh na wale wote ambao ni watumishi wa Kikristo waliweza kumuiga Yusufu kwa haya na kumaakinika ili wote waliokaribu waone ya kwamba Bwana yupamoja nanyi! Alafu ikaja mgongano katika historia yake, wakati wa majaribu. Tunamuona Yusufu akijaribiwa na majaribu ambayo wengi huangamia! Alishambuliwa wakati vijana wako wanyonge. Utu wake wa upole ulimfanya chombo cha ombi lisilo takatifu kutoka kwa mmoja ambaye wema wake aliutegemea kwa njia kuu. Wengi wa watu hawangemlaumu angetenda dhambi – wangewekelea mwenye kuleta majaribu, na kuupa samahani unyonge wa ujana. Sisemi vile. Mungu kataza nisiseme vile, kwa kuwa katika matendo ya uchafu, wote wanaotenda hakuna msamaha! Lakini Mungu alikuwa na Yusufu na hakuteleza katika mahali patepetevu.
Hivyo Yusufu alikwepa shimo lile refu ambalo walio chukiza Bwana huanguka. Aliokolewa kutoka mtego wa mwanamke yule, ambaye Suleiman amesema, “ Amewaangusha wengi na kuwaumiza; ndio, wanaume wengi wenye nguvu wameangamizwa naye. Nyumba yake ni njia ya Kwenda jehanamu, kuelekea kwenye vyumba vya kifo…utumwa, wenyewe, ulikuwa janga ndogo kulinganishwa na ambacho kingemtendekea Yusufu kama angefungwa na tamaa ovu. Kwa furaha, Bwana alikuwa pamoja naye na akamuezesha kumshinda mjaribu na swali, “ Naweza fanyaje uovu huu mkuu na nitendee dhambi dhidi yake Mungu?’’ Alitoroka. Kutoroka kwake ndio kulikuwa onyesho la ujasiri wake! Ndio njia pekee ya ushindi juu ya dhambi za mwili. Mitume anasema, “ Zikimbie tamaa za ujana ambazo zinapigana na nafsi.” Wakati Telemachus alikuwa katika kisiwa cha Calypso, Mwalimu wake alilia, “Paa, Telemachus, paa! Hakuna tumaini la ushindi ila kwa kupaa.” Kwa Hekima Yusufu aliacha nguo yake na kukimbia, kwa jili Mungu alikuwa naye. Picha ile inageuka na yule ambaye alikuwa wa kwanza, mtoto mpenzi nyumbani alafu mtumwa, – alafu aliyejaribiwa – sasa anakuwa mfungwa. Gereza za Misri bila shaka zilikuwa zenye hofu kama vile mahali pa aina ile kulikuwa wakati ule wa zamani na hapa yuko Yusufu katika shimo lililo na kelele. Kwa Ushahidi aliusikia ufungwa wake kwa sababu tunaambiwa katika Zaburi ya kwamba, “chuma iliingia katika nafsi yake.” Alihisi ikiwa kitu cha ukatili kuwa chini ya uvumi mbaya kama ule na kuteseka juu ya ukosefu wa hatia wake. Kijana mdogo msafi wa moyo, lazima alihisi ukali kuliko kiboko cha nge, kushtakiwa kama vile alikuwa. Hata hivyo alipokuwa ameketi katika giza la gereza lake, Bwana alikuwa naye.
Upungufu wa gereza haukuwa umekatiza rafiki wa Kimungu. Jina la Bwana libarikiwe, hawaachilii watu wake wakiwa mashakani! Hapana, Ni mwema kwao wanaposhtakiwa kwa uwongo kushinda wakati mwingine wowote na yeye huwashangilia katika wakati wa udhaifu. Mungu alikuwa na Yusufu na hivi karibuni tabia zake nzuri, upole, utendaji, ukweli, kazi ya Yusufu ilikuwa imeshinda juu ya msimamizi wa gereza ili Yusufu akainuka tena mpaka juu na kuwa kiongozi wa gereza. Kama kifuniko ambacho unaweza kukisukuma chini, lakini lazima kitainuka, basi ndivyo Yusufu alikuwa! Lazima angeogelea – hangezama – Bwana alikuwa naye! Uwepo wa Mungu ukamfanya mfalme na kasisi pahali popote alienda na watu wakakubali ushawishi wake. Katika ufalme ule mdogo wa gerezani, Yusufu alitawala, kwa ajili, “ Mungu alikuwa naye.” Akainuka zaidi ya hapo hata hivyo wakati nafasi itapatikana ya kuonyesha nguvu za unabii. Wawili wa wale ambao walikuwa chini ya uongozi wake walionekana kuwa na hofu asubuhi moja, na kwa upole wake wa kawaida akauliza, “ Kwanini mko na hofu leo?’’ Kila wakati alikuwa na wema na mwenye huruma na kwa hivyo wakamwambia ndoto zao na akafafanua kama vile matukio yatakuwa. Lakini kwa nini alifafanua ndoto? Ni kwa sababu Mungu alikuwa naye! Yusufu anawaambia hapo hapo, “ ufafanuzi unatoka kwa Mungu.” Sio kwamba alikuwa na ujuzi wa sanaa ya siri, au alikuwa mnjanja, lakini Roho wa Mungu alikuwa juu yake na kwa hivyo alielewa siri katika ndoto zile. Hii ilielekeza kwa hatua zingine kwa kuwa baada ya kujaribiwa kutoka 17 mpaka 30 – baada ya kutumikia kifungo cha miaka 13 cha huzuni – alikuja kusimama mbele ya Farao na Mungu yu ndani yake pia, pale!
Unaweza ona ya kwamba ndani yake ameinuliwa, kwa kuwa kijana yule Muhibirania anasimama imara na anaongea kumuhusu Mungu katika Mahakama yenye kuabudu sanamu! Farao aliamini miungu wengi – aliabudu mamba, kwarara, ndume – na kila aina ya vitu, kuenda chini hadi kwenye mboga na vitunguu, ili kwamba ilisemekana kuhusu wa Misri, “Watu wenye furaha ambao Miungu wao hukua hata kwenye mashamba yao!” Lakini Yusufu hakuona aibu kuongea juu ya Mungu wake kama Mungu pekee aliye hai. Alisema, “ Yale Mungu anatarajia kufanya alimuonyesha Farao… Kwa utulivu, na kwa njia ya heshima, anafunua ndoto na kuieleza yote kwa Farao, akikataa hata hivyo sifa yoyote ya hekima. Anasema, “Haiko ndani yangu: Mungu atampatia Farao jibu la amani… Mungu alikuwa naye, kwa kweli! Yusufu alifanywa kiongozi juu ya Misri yote na Mungu alikuwa naye. Mfalme alisema, “ Tunaweza mpata mtu kama huyu ambaye Roho wa Mungu yumo ndani mwake?” Sera yake ya kuhifadhi mahindi katika miaka ya wingi ilipata ufanisi wa kuridhisha, kwa kuwa Mungu alikuwa anafanya kazi naye kuhifadhi wanadamu kutokana na maangamizi ya janga la ukame. Mfumo wote wa Yusufu ukiangaliwa kama unafanyishwa kazi kwa faida ya Farao, mkubwa wake, ilikuwa zaidi ya kipimo cha kueleweka na chenye mafanikio. Hakuwa mtumishi wa Misri – Farao alikuwa amempatia mamlaka – na akatajirisha Farao na, wakati ule ule, akaokoa nchi kutokana na njaa. Mungu alikuwa naye katika kuleta babake na familia katika Misri na kuwaweka katika Gosheni. Na Mungu alikuwa na Yusufu mpaka wakati wake wa kufa, wakati yeye, “ alichukua kiapo juu ya wana wa Israeli, akisema kwa kweli Mungu atawatembelea, na mtabeba mifupa yangu kutoka hapa.”
Mungu alikuwa naye na akamuweka akiwa mwaminifu kwa agano na uzao wa agano, hata kwa kifungu cha miaka 110! Aliaga akiwa mwaminifu kwa kusudi la Mungu wa mababu wake, kwa sababu hangehesabiwa na waMisri, hata kwa kisomo na utajiri wake. Alichagua kuitwa muIsraeli na kushiriki na uzao uliochaguliwa bila kuzingatia bahati yao. Yeye, kama mababu, walikufa katika imani, wakitafuta uridhi wa ahadi, na kwa ajili yake kukataa utajiri na sifa za dunia, kwa sababu Mungu alikuwa naye.
Tutapitia Ushahidi wa ukweli ya kwamba Mungu alikuwa naye. Ushahidi ni nini ya kwamba Mungu alikuwa naye? Ushahidi wa kwanza ni – alikuwa chini ya ushawishi wa uwepo wa Kimungu na kuishi katika furaha yake. Sitahitaji kunukuu nyakati hizi – sio zote, kwa kiwango chochote , kwa sababu kila mahali, wakati wowote roho ya Yusufu inaongea – anakufahamisha ya kwamba yuajua Mungu yu Pamoja naye. Mtazame, sana sana katika majaribu. Ni huruma iliyoje kwake ya kwamba alikuwa mcha Mungu! “ Ninaweza tenda aje uovu wa aina hii, nimukosee Potifa?’’ Hapana. Ila angemkosea Potifa ambaye alikuwa bwana mwema kwake. Anasema, “Nitatenda aje uovu huu dhidi ya mwanamke huyu?’’ Kwani ingekuwa dhambi dhidi yake. Hapana. Kama vile Daudi alisema, “Dhidi yako, yako pekee, nimetenda dhambi, na kufanya uovu huu mbele ya machoni mwako,’’ nikionyesha pointi ya kwanza ikiwa dhambi dhidi ya Mungu, kwa hivyo ikawa Yusufu, alipokuwa akimtoroka mujaribu, ananena kuwa – “ Naweza tendaje uovu mkuu kama huu, nanitende dhambi dhidi yake Mungu?’’ Oh, kama wewe nami kila wakati tungemhisi Mungu akiwa karibu, akituangalia kila wakati, hatuwezi thubutu kutenda dhambi! Uwepo wa mkubwa hufanya mtu asitende ambayo angenuiya Kutenda. Na uwepo wa Mungu, ungetambulika, ungekuwa kinga dhidi ya majaribu na ungetuweka imara katika utakatifu. Wakati Yusufu, na wakati baadaye, aliongea kuhusu Mungu – wakati Mungu alimsaidia sio tu kusimama dhidi ya majaribu lakini pia kupatiana huduma – utaona vile anaufanya kuwa wa Mungu. Hatafafanua ndoto ya Farao bila kwanza kumuambia, “ Sio mimi: Mungu amemuonyesha Farao vile anatarajia kufanya.” Alikuwa na ufahamu wa uwepo wake Mungu wakati aliposimama mbele ya kiongozi yule mkubwa kama vile alimkataa yule mwanamke mwenye dhambi! Ilikuwa vile katika maisha yake. Acha nisome kutoka kwa rejista ya familia yake. Na kwa Yusufu kulizaliwa wana wawili kabla ya miaka ya ukame ije, ambayo Asenath binti ya Potifera, kasisi wa On, alimzalia. Na Yusufu akamuita mzaliwa wa kwanza Manase: kwa kuwa Mungu, alisema, amefanya nisahau kazi yangu ngumu, na nyumba yote ya babangu. Na wa pili jina lake akamuita Ifraimu: Kwa kuwa Mungu amenifanya kuzaa matunda katika nchi ya mateso yangu.” Wakati babake katika uzeeni alimuambia, “ Hawa ni nani?’’ Yusufu alijibu kwa uzuri, “ Hawa ni wana wangu, wale Mungu amenipa mahali hapa. Samahani kwa tabia hatuongeangi vile, lakini Yusufu aliongea. Bila hofu yoyote aliongea kutoka kwa moyo wake, akiwa na hisia ya uwepo wa Kimungu ukifanya kazi. Kama yeye, katika haya, kwa Bwana! Sina budi ila kuongea juu yake. Kama kuna jambo nzuri lililoonekana juu ya Bwana Yesu kuliko lingine ni hisia ya uwepo wa Kimungu. Unaiona akiwa mtoto – “ Hamjui kwamba lazima niwe katika kazi ya Baba yangu?’’ Unaisikia katika maneno , “Siko pekee yangu, kwa sababu Baba yunami.” Na tena, “ Najua unanisikia kila wakati… Unaiona katika wakati wake wa mwisho wa maisha yake ya duniani, wakati maumivu makali inayomtesa ndiyo inamfanya alie, “ Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?’’ Uwepo wa Mungu ulikuwa kila kitu kwa Kristo kama vile ulikuwa kwa Yusufu!
Sasa, kama wewe nami tutamueka Bwana mbele yetu kila wakati – kama nafsi yetu inaishi katika Mungu – na kuitegemea, Mungu pamoja nasi! Hakuna makosa juu yake. Kama uko chini ya ushawishi wa maandiko haya , “ Wewe, Mungu, nione. Unaweza kuwa na uhakika ya kwamba uwepo wake utaenda nawe na atakupatia mapumziko. Hakuna mtu aliyeona uwepo wa Mungu, na kwa hivyo kuishi katika utakatifu, na baadaye akagundua alikuwa katika undanganyifu. Neema katika maisha inaonyesha ya kwamba Mungu wa neema yunasi! Ushahidi unaofuata ni huu – Mungu alikuwa na Yusufu kwa sababu alikuwa msafi wa moyo. “ Wabarikiwao ni wenye moyo safi kwa kuwa watamuona Mungu.” Hakuna mwingine anayeweza kufanya vile. Mungu hatajionyesha kwa wale mioyo yao ni chafu. Aliye na mikono misafi na moyo msafi, ataishi juu. Bwana wetu Yesu alisema, “Kama mtu atanipenda, atahifadhi maneno yangu: na Babangu atampenda, na tutaja kwake, na tuishi naye.” Wakati moyo unashangaa juu ya dhambi na kutamani utakatifu, basi inaweza ingia katika ushirika na Mungu, lakini sio mpaka wakati ule. “ Wawili wanaweza tembea Pamoja ila wakubaliane?” Nikisikia Profesa wengine wakikiri wako na ushirika mdogo sana na Mungu, naweza shangaa juu yake? Tunaweza aje pata ushirika na Mungu ila kwa kutii amri zake? Ni ushirika upi uko kati ya mwangaza na giza, au ni ushirika upi kati ya Kristo na Beliali? Utakatifu wa Yusufu ni Ushahidi ya kwamba Mungu mtakatifu alikuwa naye! Ataweka nyayo za watakatifu wake. Wakati wanajaribiwa, atawakomboa kutokana na uovu, kwa kuwa uwepo wake unaangaza mazingira ya utakatifu karibu na moyo anaoishi ndani yake.
Ushahidi unaofuata katika kesi ya Yusufu ni bidii ambayo alikuwa nayo pahali popote alikuwa. Mungu alikuwa na Yusufu na kwa hivyo, mtu yule wa Mungu hakujali hali ya nje ya nafasi yake, lakini alianza mara moja kufanyia kazi yale ambayo ni mema. Alikuwa shimoni – ndio, lakini Bwana alikuwa naye na shimo haikuwa mbaya kwake. Alililia ndugu zake na ingawa hawakumsikia, alifanya juhudu yake kuwakanya dhidi ya hatia yao. Alifanywa mtumwa na waIshmaili, lakini katika msafara alikuwa salama, kwa sababu Mungu alikuwa naye. Wakati alikuja kuwa mtumwa katika nyumba ya Potifa, Bwana alikuwa naye na akawa mtu mwenye ufanisi! Mabadiliko ya mandhari haikuwa mabadiliko ya marafiki wake! Hakujifanya mwenye mamlaka na kuonyesha nia yake kuwa kubwa, lakini alifanya kazi alipokuwa na kufanya majukumu yake ya kawaida kwa moyo mwema – kwa ajili Mungu alikuwa naye! Wengi wangesema, “ Nimeuzwa kwa hatia mbaya kama mtumwa. Sitakiwi kuwa hapa na sitakiwi kuyafanya majukumu yoyote kwa Potifa, na sitamfanyia kazi bure.” Hapana, Bwana alikuwa naye, na kwa hivyo akajitweka kwa lile lilikuwa karibu na kulifanya kwa nia nzuri. Bila tashwishi alifanya kazi ndogo ndogo za nyumbani kwanza, alafu kwa kiwango akawa mkubwa wa nyumba. Mtu aliye na utakatifu yu tayari kwa kitu chochote – hachoki lakini anakubali hali aliyopatikana nayo – na anafanya wema katika ndani yake, kwa ajili ya Bwana. Bwana alikuwa na Yusufu, bila shaka, wakati alirushwa gerezani. Yusufu alijua Mungu ako naye gerezani, na kwa hivyo hakukaa kwa huzuni, lakini alijiimarisha kufanya vema katika hali ya mateso.
Kwa ajili Bwana alikuwa naye pale, alifarijiwa. Itakuwa vema kuwa na Bwana katika gerezani kuliko katika kiti cha Farao bila Mungu! Hakuomboleza na kuandika barua kwa Potifa au kuomba rufaa kwa Potifa. Alijitweka kuwahudumia kwa wafungwa wenzake na walinzi wa gereza na hivi karibuni akawa mbele, tena,kwa ajili, “Bwana alikuwa naye.” Wakati alikuja kuinuliwa na Farao akamfanya kiongozi katika Misri, tazama vile alivyofanya! Hakulegalega, wala kupeleka kesi yake kotini. Hakungoja kufurahia heshima yake kwa amani na kuwacha wengine kufanya kazi, lakini alilenga kazi yake, yeye mwenyewe na mara moja! Soma Mwanzo 41:45 – “ Na Yusufu akaenda kwa nchi yote ya Misri.” Alafu soma kifungu kifuatacho – “ Na Yusufu akatoka kwa Farao na kutembea katika nchi ya Misri.” Mara alipopata cheo, alijipatiana kwa kazi yake, yeye mwenyewe akikagua nchi yote! Wengi wamechoshwa na kazi za kupata mamlaka mpaka hawana nguvu iliyobaki ya kutimiza jukumu zao. Wanapopata mamlaka mapya, uzingatio wao wa kwanza ni vile watatumia faida. Wanaowinda mamlaka hawajitayarishi kwa nafasi, lakini wanatamani cheo wawe tayari au laa! Wengi, wakati wanapata cheo, wako na maarifa ya kuonyesha vile hawataweza kufanya kulingana na jukumu na cheo kile – wanaingia kwenye ofisi na kupatiana kazi yao kwa karani anayefuata, na yeye kwa mwingine, ili hakuna kitu kinachotimizwa! Kuchelewesha kazi ndio kikomo cha biashara, na kuchelewa ndio mwizi wa wakati. Wanatenda yaliyo kidogo sana kupata fedha, kwa nadharia ya kwamba ukiwa na bidi sana kazi yako itakuwa bei nafuu.
Yusufu, hata hivyo hakuwa wa aina ile, kwa sababu mara tu alipofanywa kamishna mkuu wa Misri, ndio alianza kujenga maghala na kukusanya nafaka ya kuijaza. Kupitia sera yake nzuri ya kiuchumi, akakidhi mahitaji ya watu katika wakati wa ukame, na kupitia haya nguvu za Farao zikaongezeka zaidi. Bwana alikuwa naye – kwa hivyo hakufikiria heshima ambayo alikuwa amepata madaraka yake, lakini kwa wajibu uliokuwa juu yake – na akajipatiana kwa kazi yake kuu. Hii ndiyo mimi nawe lazima tufanye kama tutapatiana utendanji wa kuonekana ya kwamba Mungu yunasi! Lakini tazama tena, Mungu alikuwa na Yusufu na hiyo ilimfanya kuwa mpole na mwenye huruma. Watu wengine wasiochelewa biasharani ni wagumu – lakini sio Yusufu! Upole wake unamtenganisha. Amejawa na upendo wa uzingatiaji. Alipokuwa na wafungwa chini yake, hakuwadhulumu lakini kwa uzingatiaji. Alitazama afya yao, na kuuliza shida zao na alikuwa tayari kufanya awezalo kuwasaidia. Hii ndiyo ilikuwa siri moja ya ufanisi maishani mwake- alikuwa rafiki ya kila mtu. Yule ambaye ni tayari kuwa mtumishi wa wote, yeye ndiye atakaekuwa mkubwa wa wote. Mungu alikuwa na Yusufu na akamfunza upendo, kwa kuwa Mungu, mwenyewe, ana huruma kwa wale walio katika mateso. Labda utapinga haya, ya kwamba Yusufu alikaa, kwa mda, kutesa na kuwachezea ndugu zake. Sio hata kidogo! Alikuwa anatafuta wema wao. Upendo aliokuwa nao juu yao ulikuwa wa Hekima na wa maakini. Mungu, aliye na upendo mwingi kuliko Yusufu, hutuumiza mara nyingi ili tutubu na kutuponya kutokana na maovu mengi. Yusufu alitumai kuwaleta ndugu zake kwa hali sahihi ya moyo na alifanikiwa, ila mchakato ule ulikuwa wa uchungu kwake kuliko kwao!
Mwishowe hangejizuia, lakini alibubujika kwa machozi mbele yao wote, kwa sababu kulikuwa na moyo mkubwa wa upendo chini ya nguo ya Misri ya Yusufu! Alipenda na nafsi yake yote kama vile kila mtu aliye na Mungu kwa kuwa “Mungu ni Upendo.” Kama haupendi, Mungu hayuko nawe. Ukiishi duniani kwa kujipenda na chuki, kushuku, na kuwa mgumu – shetani yunawe! Mungu hayupo kwa sababu mahali Mungu yupo anapanua roho wake! Anatufanya kupenda wanadamu wote kwa upendo wa wema na anatufanya kukubali wema wa undugu wa Israeli, ndio tunafurahia kufanya wema kwa wale wote ambao wako kwa nyumba ya imani. Hii ilikuwa alama kwamba Mungu alikuwa na Yusufu. Alama ingine ya uwepo wa Mungu katika Yusufu ilikuwa Hekima yake kubwa. Alifanya kila kitu kulingana na vile kilifaa kufanywa. Ni vugumu kubadilisha kitu chochote katika maisha ya Yusufu kuiboresha na ninafikiria kama nikipenda Hekima yake kwa kitu kimoja kuliko kingine ni kwa kimya chake kizuri. Ni rahisi kuongea, rahisi kuongea vizuri, lakini kuwa kimya ndiyo ngumu! Hakusema kitu ambacho ninaweza soma, kuhusu mke wa Potifa. Ilionekana kuwa muhimu kujitetea, lakini hakumshtaki mwanamke yule. Aliacha hukumu kuendelea na kumuacha kwa nafsi yake na uzingatiaji mpole wa bwanaye. Hii ilionyesha nguvu kubwa. Ni vigumu kwa mtu kushikanisha mdomo wake, asiseme kitu, wakati maisha yake iko hatarini. Alikuwa Hodari wa maneno katika kimya chake mpaka hakuna neno la malalamishi katika maisha yake.
Hatuwezi sema ya kwamba kuwa watakatifu wote wa Bibilia, kwa kuwa wengi walilalamika kwa uchungu! Kwa kweli, tuko na kitabu cha malalamiko! Hatuwahukumu waliolalamika, lakini tunawaenzi wale, kama kondoo mbele ya wanyoaji nywele, walikuwa kimya. Chuma iliingia nafsi yake, lakini hatuambii vile – Tunatazama Zaburi kwa taarifa hii. Alibeba kwa utulivu mapenzi ya Babake. Wakati ndugu zake walisimama mbele yake – watu wakatili waliomuuza – hakuwakashifu. Kwa kweli aliwafariji, akisema, “Sasa msiwe na shaka, au wenye hasira kwenu wenyewe, ya kwamba mliniuza hapa: kwa Mungu alinituma mbele yenyu kuokoa maisha yenyu.” Akiwafanyia msamaha mwema kwao, akasema, “ Na Mungu alinituma mbele yenyu kuhifadhi ufanisi katika dunia kwenu, na kuwaokoa kwa ukombozi mkubwa. Kwa hivyo sio nyinyi mlionituma hapa, lakini Mungu.” Ni tofauti aje kwa roho ya wale watu wanaochunguza, wakijaribu kupata makosa, na wakati makosa inapatikana, wanalia, “ Tazama! Uliona haya? Nilikuambia! Hawa watu wazuri sio wema kuliko vile wanavyostahili.” Ndio, kunaweza kuwa kuna madoadoa katika jua, lakini kuna madoadoa makuu katika macho yako au ungeweza kuona mwangaza zaidi wa Mungu! Wale ambao huona makosa tayari wako na mengi yao. Kama mtu yule aliyeiba bidhaa na akakimbia, wanajaribu kugeuza harufu kwa kuita, “ Mwizi, mwizi,” kwa wengine! Na Mungu atufanye vipofu kwa makosa ya watu wake hivi karibuni , na sio kutufanya kuwa na jicho la chui kwa makosa yao na kitengo cha nia mbaya juu yao! Natamani kwa Hekima tuwe kimya kama vile Yusufu alikuwa. Tunaweza kutubu juu ya maongezi, lakini nadra kufikiria juu ya kimya. Unaweza lalamika na kupata haki kwa malalamishi, lakini utapata makuu zaidi usipolalamika.
Kwani ni nini ilichokuwapo kwa Yusufu kulalamika, kwani Bwana alikuwa naye? Alikuwa gerezani -hicho ni kitu cha kulalamikia. Ndio, lakini kama bwana alikuwa naye, gereza haikuwa ya kuhofia! Ninaweza kuenda gerezani siku yoyote kama bwana atakuwa nami! Nani hawezi? Lakini Yusufu alikuwa mbali na babake mpenzi na kukimbiakimbia kwa ile miguu ndogo ambayo alikuwa anapenda kusikia – miguu ya ndugu yake mdogo Benjamin. Niko na uhakika Yusufu alimkosa mtoto mwingine pekee wa mama yake, nduguye. Ilikuwa hofu kubwa kwake kuwa mbali na nyumbani, lakini alikuwa kimya, mtulivu na menye furaha. Mungu yu pamoja naye, kama Benjamin hayuko! Kama baba Yakobo hayuko, Mungu yuko! Na kwa hivyo haoni haja ya malalamiko ya uchungu, lakini sababu ya kukubali kazi yake na kufanya aliwezalo kwa kila hali. “ Mungu alikuwa naye” na huu ndio ushahidi wa mwisho ambao napatiana – ya kwamba alikuwa mwaminifu kwa agano, mwaminifu kwa Israeli na Mungu wa Israeli mpaka mwisho. Farao akampatia, katika ndoa, binti wa kasisi. Na kasisi walikuwa wa cheo kikuu kote Misri – na kwa hivyo Yusufu akapatiwa Madaraka juu ya ndoa, na pia kuwa mkubwa wa wakubwa wote ofisini. Walilia mbele yake, “Piga magoti,” na kila mmoja alimheshimu katika nchi yote ya Misri. Ila hangekuwa MMisri – alikuwa muIsraeli, na babake , alipokuja Misri, alimpata mmoja wa familia kwa moyo na nafsi! Baraka ya babake ilikuwa ya thamana kwa Yusufu, na aliipokea kwa ajili yake na wana wake.
Ninatazama kwa uchungu maprofesa wengi wanao fanikiwa duniani hawana Mungu ndani yao, kwa sababu wanageuka kuwa wa Misri- hawajui, sasa, kujali ibada ya watu wa Mungu – wanatafuta kitu chenye maonyesho na cha kuheshimika! Wanahitaji jamii kwa hivyo wanatafuta kanisa lenye mtindo na kumeza kanuni zao! Wanawawekelea watoto wao, kwani nani anatarajia mabinti na vijana kuhudhuria mkutano wa kawaida ambapo watu wa kiwango cha chini huenda? Kwa ajili ya vijana, lazima watachanganyika na jamii, na kwa hivyo wanaacha kanuni zao, watu wao na Mungu wao! Wanakuwa wa Misri! Kwa kweli, wengine wao wangekuwa wafuasi wa shetani ili kupata Madaraka na cheo! Ndio hao, wanaenda Misri, wakiwa vikundi! Nimeiona na nitaiona tena. Wengine wenu wakipata kuwa matajiri, nisema mtakuwa hivyo – inakaa kuwa njia ya binadamu – mara tu profesa anapata ufanisi duniani, anapata aibu kwa ukweli wa Mungu ambaye alimpenda mwanzoni. Waasi wa aina hii wataipata kazi ngumu kufa. Kweli nasema kwenu, badala kupata aibu juu yetu, tuko na sababu nzuri ya kupata aibu juu yao, kwa sababu ni juu ya aibu hawawezi tosheka kujihusisha na watu wateule wa Mungu kwa sababu ni masikini, na labda hawajasoma! Yusufu alikaa na watu wake na Mungu wao – ingawa lazima aishi Misri, hatakuwa Mmisri! Hata hatuwacha maiti yake katika kaburi la Misri! WaMisri walijenga kaburi la dhamana kubwa la Yusufu – inasimama mpaka leo, lakini mwili wake haupo. “Nawahimiza,” alisema, “chukua mifupa yangu, kwa sababu mimi si wa Misri. Mahali pangu ni katika nchi ya agano.” “Alitoa amri juu ya mifupa yake.”
Acha wengine wafanye wapendavyo, kwangu bahati yangu imechaguliwa kwa wale wanaomfuata Bwana kikamilifu. Ndio, Bwana wangu, pahali unapoishi, nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako Mungu wangu, na Watoto wangu wawe wako mpaka kizazi cha mwisho. Kama Bwana yunawe, hivyo ndivyo utakavyosema, lakini kama hayuko nawe na upate ufanisi duniani, na uongezeke katika utajiri, utamgeuka Kristo na watu wake – na itabidi tuseme, kama Paulo alivyosema, “ Demas ameniacha, na kuupenda ulimwengu.”
3. Tatu, tutazame MATOKEO YA MUNGU KUWA NA YUSUFU. Matokeo yalikuwa kwamba, “ Alikuwa mtu mwenye ufanisi.” Lakini tazama kwamba ingawa Mungu alikuwa na Yusufu, haikumtenga kando na chuki, “ Mungu alikuwa naye lakini ndugu zake walimchukia. “ Ndio, na kama Mungu anapenda mtu, dunia itamchukia. Tunajua sisi ni wana wa Mungu kwa sababu maadui wa Mungu ni maadui wetu! Zaidi ya hayo, “Mungu alikuwa na Yusufu,” lakini haikumtenga kutokana na majaribu mabaya – Haikuzuia mke wa mkubwa wake kumtamani. Watu wazuri wanaweza jaribiwa kwa majaribio mabaya zaidi. Uwepo wa Mungu haukumtenga kando na uvumi – mke wa nyumba alimshtaki kwa ukatili mkuu na Mungu akamruhusu Potifa kumuamini. Mimi na wewe tungesema, “ Kama Mungu yunasi, uovu kama huu unaweza tufanyikiaje?” Lakini Bwana alikuwa naye na bado alikuwa mtu aliyefitiniwa! Hapana, uwepo wa Kimungu haukumtenga kutokana na uchungu. Alikaa gerezani mpaka kama amevaa nyororo mpaka chuma kikaingia moyoni na bado, “Bwana alikuwa naye.” Uwepo ule haukumuokoa kutokana na kuvunjika moyo. Alisema kwa mlinzi wa gereza, “Nifikirie mambo yako yakienda vyema…lakini mlinzi alimsahau. Kila kitu kinaweza kaa kuenda kinyume kwako, na bado Mungu anaweza kuwa nawe. Mungu haahidi ya kwamba utakuwa na ambacho kinakaa ufanisi, lakini utakuwa na ufanisi wa kweli.
Sasa, ilisaidia nini Mungu kuwa na Yusufu? Kwanza ilimuokoa kutokana na dhambi mbaya. Anatoroka, anafunga masikio yake – anatoroka na kushinda -kwa kuwa Mungu yuko naye! Rafiki mchanga, kama Mungu yuko nawe wakati wa majaribu, hutahitaji kitu kingine, hakuna matokeo mengine makuu ila kubakia kikamilifu ukiwa msafi kwa nguo zisizochafuliwa na mwili! Mungu alikuwa naye na matokeo yaliyofuata alimsaidia Kutenda makuu. Mahali popote yuko, anafanya jambo linalo faa na kwa ukuu. Kama ni mtumwa, mkubwa wake anapata kuwa hajawahi kuwa na mtumwa kama yeye! Kama yuko gerezani, mashimo yale haikufurahishwa na Malaika mhudumu kama yeye! Kama ameinuliwa kuwa na Farao, Farao hakuwa amepata mhifadhi wa fedha za Misri- na hakuna wakati fedha za Misri zilikuwa na ufanisi kama sasa! Kwa njia ile ndio Mungu alimsaidia Yusufu akaweza kutimiza hatima yake kuu, kwa ajili kama Nuhu alikuwa baba wa pili duniani, tutasemaje kumhusu Yusufu, ila alikuwa muuguzi mlezi wake? Wanadamu wangekufa njaa kama maono ya Yusufu haingepatikana, kwenye magala, mazao ya miaka ya wingi, kwani kulikuwa na ukame juu ya nchi zote!
Hekima ya Yusufu ikalisha wanandamu! Haikuwa cheo kidogo kwa yule kijana wa Kiyahudi – Kuwa Meneja wa kamisheni wa dunia yote! Kama Mungu yunasi, tutatimiza hatima ya kuheshimika pia. Inaweza kosa kujulikana kwa mapana, sio kwa macho kibinadamu, lakini maisha inaheshimika kwa uwepo wa Mungu! Pia ilimpa Yusufu maisha yenye furaha sana, kuchukua maisha ya Yusufu, mpaka mwisho, ni ya kutamanika. Hakuna ambaye angefikiria kumweka Pamoja na wenye mateso. Kama tungefanya uchaguzi wa watu walio na huzuni, hatuwezi fikiria juu ya Yusufu! Hapana, ilkiwa maisha mema na yenye furaha – na yako itakuwa vile kama Mungu yunawe.
Na, kumalizia, Mungu aliwapa Yusufu na familia yake baraka maradufu Israeli, ambayo haikufanyika kwa wana 12 wa Yakobo. Yakobo akasema, “ Na sasa wana wako wawili, Ephraim na Manasseh, waliozaliwa kwako katika nchi ya Misri kabla nije kwako Misri ni wangu; Kama Reuben na Simeoni, watakuwa wangu,” basi kuwafanya kila mmoja wao kabila. Ephraim na Manasseh kila mmoja alisimama mbele ya kabila ni kama walikuwa wana wa Yakobo. Levi anatolewa kwa wale 12 na wanapata kuwa watumishi wa Mungu. Alafu Ephraim na Manasseh wanawekwa ndani, ndio nyumba ya Yusufu inaongezeka mara dufu kati ya makabila 12! Kuna Yusufu wawili katika Israeli lakini Judah ni mmoja! Yusufu ako na baraka mara dufu ya ufalme! Wale ambao wanaanza mapema na Mungu, wanasimama imara mpaka mwisho na kushikilia Mungu katka dhiki na kwenye mafanikio, wataona uzao wao ukija kwa Bwana – na katika wana wao watapata mara dufu – ndio, Bwana atawapa mara dufu kwa yale yote watakayopoteza kwa ajili ya jina lake. Inaweza kuwa wataishi kuona mkono wa Bwana juu ya watoto wao na watoto wa watoto wao! Na kwao itatimika neno la Mungu, “Kwako Israeli itabariki, ikisema, Mungu alikufanya kama Ephraimu na kama Manasseh.” Natutafute kipande mara dufu na watu wa Mungu kwa kuwa nao kimoyo. Nani yutayari kuteseka nao ili apate kutawala nao? Nani yutayari kutupilia utajiri wa Misri nyuma ili akapate maradufu katika nchi ya agano, nchi ambayo inatiririka kwa maziwa na asali?
Nafikiri nasikia wengine wenu mkisema, “Niko hapa, bwana. Nitafurahi kushiriki na watu wa Mungu, liwe liwalo.” Kuubeba msalaba wa Kristo na utavaa taji la Kristo! Enda naye katika matope, na utakuwa naye katika jumba la ufalme! Utashiriki naye katika kipande mara dufu katika siku ya kuonekana. Hii inaweza kuwa kwa sababu Bwana yunawe – hiyo lazima iwe ndio mwanzo na mwisho wake! “ Bwana alikuwa na Yusufu” – Ewe Bwana, kuwa nasi! Ewe ambaye jina lake ni Imanueli, Mungu Pamoja nasi, kuwa nasi kutoka sasa mpaka milele! Amina na Amina!