Barua ya wazi
Kutoka kwa toleo la Oktober 1891 la jarida ya Sayansi ya Kikristo na E.E.E
Kwa siku kadha nimekuwa na hisia ya wasiwasi na hofu nisiingie katika makosa, na nisiweze kukua katika Ukweli, kwani nilikuwa na matumaini ya kufanya hivyo. Hii siku ilikuwa moja ya giza na mafadhaiko. Mwishowe nikaketi, mbali na kila mtu na nikakumbana na makosa hii. Nikasema, sijali vile makosa inasema, yote ni uongo. Mungu alisema ,”Usiogope, niko nawe mpaka mwisho wa dunia.” Hakuna kitu ambacho kinaweza kunitenganisha na Mungu.
Mara moja picha ikanijia kwa mawazo yangu, kama mmoja anayeniongelesha. Mtoto mdogo alikuwa na uoga wa kupitia kwenye ukumbi uliokuwa na giza kuenda kwenye chumba kingine. Baba yake na mama yake wakamhakikishia ya kwamba hakukuwa na kitu chochote cha kuhofia, na wakamuambia aende. Imani yake ya kitoto na ujasiri ukamuezesha kuweka kando hofu yake na kuenda, hivyo kuthibitisha ukweli wa maneno yao.
Sasa Mungu, Baba anayetupenda, ameniongelesha kupitia Bibilia na Sayansi na Afya, akiniambia niende mbele kwa ujasiri kupitia inayoonekana kama giza ya imani za kibinadamu , kwa sababu sio kitu. Si amesema “ Mimi ni Mungu, na hakuna mwingine?’’ “Kwa sababu umemfanya Bwana, ambaye ni kimbilio langu, aliye juu zaidi, makaazi yako; Hakuna uovu ambao utakupata, wala tauni yoyote kuja karibu na makazi yako.”
Basi je, sitakuwa wa kuamini kama mtoto mdogo, na kuamini {Kufahamu} yale Mungu ananiambia, na niende mbele nikijua Mungu ni yote? Hivyo niliomba kwa wakati, na hisia nzuri ya uwepo na nguvu za Mungu zikanijia.
Hali inayohusiana na tajiriba ilileta utambuzi wa Akili moja kwa nguvu zaidi kuliko mbeleni. Siku moja au mbili baadaye, nilipokea barua mbili kutoka kwa marafiki wawili wa karibu katika Ukweli wakipatiana mawazo yaleyale ya uhimizo yaliyonijia , katika umbo tofauti pekee.
Jinsi ambavyo masomo ya shule ya jumapili hufichua kuomba sanamu katika zama hii. Makanisa yanasoma masomo haya kwa urahisi kama kurejelea Israeli ya zamani. Kwa nini wasione ya kwamba wanaongelesha makosa leo, na kutuonyesha dhambi zetu. Wanaongea na sauti yenye maonyo. Kwa nini wote wasimrudie Bwana Mungu wao?