Mahojiano na mchungaji Mary Baker Glover |

Mahojiano na mchungaji Mary Baker Glover

Kutoka kwa Mlinzi wa Sayansi ya Kikristo JUNI 17 1905 Na SIBYL WILBUR


Mahojiano ya juzi ya mda mfupi na Sibyl Wilbur wa Boston Herald yalikuwa yenye kupendeza. Nitatubu ya kwamba nilienda kwa kusita kukumbana na juhudu za kunyamazisha makelele ya umma, nikiendelea kuionyesha kwa njia yangu na kimbilio langu la tumaini. Lakini ni wito mkubwa uliotulia ambao ulikuwa wake, ulichukua mda mdogo vipi kuongea naye wakati nilipoguswa na ukweli wa kusudi la kweli! Kwa kupunguza mazungumzo na kuhisi zaidi tuliachana kama tumebarikiwa. Mama Wilbur atapokea shukurani zangu kwa ukarimu wake, kwa kuniacha na masaa ya kutosha ya kuunganisha fikira zangu na zake katika hazina ya milele, na kwa kupata riba kutokana na amana iliyopatikana kutokana na dakika, mpaka tupokee akaunti kuu ambapo Mungu ndiye kuiweka? Kwa sababu ya wema wake, na apanukiwe utumishi wake; nami, nifanye kazi kupanua yangu kuwa njia za amani; mpaka mzigo na joto ya siku zimeisha, mawimbi ya jioni yamepita, na ndege na kuchanuka kwa maua kuamke katika mwangaza wa jua.

Mary Baker Eddy,

Pleasant View, Concord, N. H., Mei 24, 1905

Nimemuona mama Mary Baker G. Eddy. Nimeongea naye na kupata majibu yake kuhusu maswala kadha juu ya Sayansi ya Kikristo. Nimeukumbatia mkono wake, nikahisi kuguswa kwa mawazo yake, nikisikiza baraka zake za wema na kupokea kutoka kwa mdomo wake ujumbe kwa dunia.

Mama Eddy yuko hai na salama, yuko katika udhibiti wa akili na nguvu zake za mwili. Hana ulemavu wowote wa mwili; ako na uzuri wa kimo na mwenye mavazi ya kuridhisha na mwenye umri. Akili yake ni safi na yenye nguvu, iko chonjo na yenye nguvu na iliyo na ufahamu. Macho yake yameng’aa, sauti yake kama kengele. Katika neno, mama Eddy anakaa kuwa amefikia marekebisho kati ya nguvu zake za kimwili na za kiroho ambayo inaahidi kubeba uhai wake katika miaka mingi ijayo.

Siri ambayo dunia imekuwa ikijaribu kutoka kwa nyumba iliyolindwa sana ya Pleasant View, siri ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikifasiriwa kwa shaka kumaanisha ugonjwa, kuporomoka kwa kimwili au kiakili, na hata wapinzani wenye msimamo mkali wa akili za kidunia, kuvunjika kamili kwa Mama Eddy na mabadiliko katika mahali pake pa wakilishi – hii siri imejulikana na kujulikana kwake ni kashfa kwa tuhuma za utoto ambazo zimewekelewa dhidi ya maisha isiyokuwa na hatia.

Siri ya Pleasant View sio siri hata kidogo. Ni ukweli wa wazi na kwa urahisi, ambao akili yoyote inaweza tayari kuwa ikipanga bila umuhimu wa kuingiliwa kwa uchungu juu ya kutengwa aliopata kwa mwanamke aliyepatiana kipimo kamili cha huduma yake kwa wanadamu kabla ya kustaafu kutokana na ukumbi wa shughuli za kibinadamu.

Hapo Pleasant View, Concord, N. H., kunaishi mwanamke wa ajabu, mwenye zaidi ya miaka themanini, ambaye anapitia mchakato wa polepole wa kumalizia kubadilisha kuwa wa kiroho uwezo wake. Anafanya muujiza wa uhai wa mwanadamu ambao unaweza shuhudiwa katika boma yoyote anapoishi baba mzee ama mama. Anafanya muujiza ambao kama mtakatifu Leo, marehemu baba wa kanisa la Katoliki, alitenda wakati alirefusha uhai wake kwa umri mkubwa kwa kujitenga na dunia, wakati alikuwa na nafasi ya kugeuza maisha yake kuwa ya kiroho kwa kusoma, maombi, na kutafakari, akinena kila mwaka waraka wa kitume ulio na bidi na wa kiroho.

Hakuna mahali pakuu Pleasant View, kama palipo Vatican, Roma; hakuna nyumba iliyo na baraza mia na mia za nyumba, milango ikifunguka juu ya milango, kila ukilindwa na askari, ili kuzingatia kimya na utakatifu kutokana na uvamizi; hakuna Bustani yenye ukuta iliyo enea kwa maili mingi ambayo mtu anaweza tembea peke yake akiwa na mazingira na Mungu, akiwa amehifadhiwa kutokana na macho yenye kuchunguza ya udadisi wa kidhalili. Kuna nyumba tu ndogo iliyoko katika ekari ndogo zenye ukuta mfupi. Kupiga kengele mlangoni inamaanisha ya kwamba kila mshirika katika nyumba amesumbuliwa, na kuingia kwa mgeni katika sembuleni mwa nyumba kunamaanisha uvamizi juu ya familia ambayo mshirika mkuu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa anayeishi duniani leo.

Kuvunjwa na ukweli.

Mwandishi sio mwanasayansi ya Kikristo. Ni muhimu kukiri kutoka mwanzo ya kwamba mahojiano na Mama Eddy yalikuwa yamehitajika, kwa sababu Mama Eddy alikuwa amekuwa chombo cha kuchunguzwa kwa kina kwa waandishi wa habari za umma wa America. Kila gazeti kuu nchini imefanya bidii katika miaka michache iliyopita kupata nafasi na kiongozi wa kanisa la Sayansi ya Kikristo na kushindwa katika kiulimwengu, wamejenga ofisi ambayo ni kubwa kama ilivyo ya kijinga inapoguswa na kiloweshi cha ukweli.

Hadithi ambayo imetengenezwa polepole kutoka Mama Eddy astaafu kutokana na maisha yenye shughuli, zaidi ya miaka kumi iliyopita, imekuwa ya kwamba kanisa la Sayansi ya Kikristo ilianzishwa katika mafundisho ya uhai wa milele katika dunia; ya kwamba imetangaza kifo kitashindwa; ya kwamba haina ujasiri wa kukumbana na kumalizika kwa kimwili kwa mwanzilishi wake. Kwa hivyo, kwa sababu dunia haikuwa na fursa ya kumuona Mama Eddy, ilikuwa inawezekana, sio, inaweza fanyika, ya kwamba Mama Eddy alikuwa ameingia kwenye ulemavu wa kimwili, au alikuwa mwenye mnyonge wa akili, kama hakuwa ameaga.

Kulikuwa na hadithi nyingine ya kwamba Mama Eddy alikuwa hai, lakini alikuwa anatibiwa na wakandaji misuli na madaktari wa urembo; ya kwamba heshima ya miaka ilikuwa imepotoshwa kwa kejeli juu ya utu wake; katika neno alilaghaiwa kwa kutumia njia bandia ili kuweka picha ya ujana kwa kujigamba yasiyowezekana juu ya mafundisho yasiyowezekana ya kimo cha kuwa mchanga milele. Hisia za mwanamke kwa kiasili zilifanya pointi hii ya kuvutia na kando, niliazimia kuwa na uwezo kuupa ulimwengu ukweli wenyewe.

Ya kwamba kanisa la Sayansi ya Kikristo halitawekwa katika hali ngumu kwa sababu ya mafundisho yake ya kifilosofia katika kifo cha kiongozi wake, imefanywa wazi kwa maelezo ya mafundisho ya mafundisho ya kweli ya Sayansi ya Kikristo juu ya maada hii ya uhai wa milele, ambayo imepatiwa mwandishi kupitia taarifa yenye mamlaka kutoka kwa mshiriki wa kamati ya uchapishaji. Taarifa hii inaonyesha upumbavu wa dhana potovu wa mafundisho haya.

“ Hatufanyi madai,” alisema mwanasayansi ya Kikriso huyu, “ Ya kwamba inawezekama mtu kuishi katika mwili milele. Tunakubali unabii wa maandiko ya kwamba hatimaye wanadamu watakuwa wamefikia kwa kiwango kikuu cha kiroho ya kwamba kifo kitaacha kuwa jambo la tajiriba ya kibinadamu. Lakini karne zinawezapita kabla ya hali hii iliyoinuka kupatikana na binadamu yeyote. Wanasayansi ya Kikristo wanaamini, hata hivyo, ya kwamba urefu wa maisha umeongezeka kupitia mafundisho ya kidini, na itaendelea kuongezeka katika kila kizazi.”

Maelezo haya yanajibu kwa ufanisi mkosoaji aliyefurahia kwa kufikiria ya kwamba wanasayansi ya kikristo walikuwa wamejiweka kwenye kona; na kwa kauli ya mzaha juu ya ubandia wa umbo la Mama Eddy, kuna uwezekano mwandishi kuwahakikishia wafuasi wapendwa wa Mama Eddy, ya kwamba hakuna mambo ya kudhalilisha ambayo imetekelezwa dhidi ya kiongozi wao; ya kwamba amezungukwa na marafiki na waliojitolea na wanaompenda; ya kwamba yeye ni kiongozi wa nyumba yake kwa njia isiyoweza kukanushwa; ya kwamba anazeeka kwa urembo kama mwanamke mwingine yeyote ashawai.

Na baada ya kukutana naye na familia yake, naamini ya kwamba, katika ukamilifu wa wakati, pazia ya uhai wa milele inainuliwa juu zaidi, dunia itajua, na ya kwamba ataaga kwa ukuu zaidi na ushindi wa imani ya Ukristo, na Wakristo duniani kote watakua tayari kutambua ya kwamba maisha yenye manufaa imefungwa kama midundo ya mziki, kama vile waja msimu wa baridi baada ya kipindi kirefu cha majira ya vuli ikikaribia uvunaji wa mwaka. Hakutakuwa na miujiza zaidi iliyotetea kwa niaba yake na mamilioni ya wafuasi wake kuliko muujiza mmoja mkubwa wa maisha mazuri ambayo huja kwa kila mwanadamu kutoka kwa tumbo la uzazi la wakati.

Kupata wakati wa mahojiano na Mama Eddy

Mahojiano na Mama Eddy haikuwa imepatikana bila kuchelewa, bila mda mrefu wa majibizano na washirika wa bodi ya uongozi ya kanisa , bila hatimaye kushinda upingamizi wa meneja wa kamati ya uchapishaji, Alfred Farlow, ambaye ofisi zake ziko Huntington Chambers, Boston. Jaribio la kupata mahojiano na Mama Eddy ilianza Februari na gazeti la Boston Herald, na ikafikia kilele kwa ufanisi Jumapili Mei 21.

Pingamizi ambalo Bwana Farrow alitoa juu ya kupatiana barua ya utangulizi kwa Mama Eddy, au makarani wake hapo Pleasant View, ilikuwa ya kiasili kabisa. Alisema ya kwamba hakuwa na mamlaka yakufanya madai kwa wakati wa Mama Eddy, na kwamba hakupendelea kumsumbua na maombi ambayo alikuwa amekataa kuzingatia mara nyingi. Alisema kwamba siku zake zilikuwa zimejaa shughuli, na ilikuwa ni jukumu lake kumkinga kutokana na kuingiliwa. Hata hivyo, Bwana Farrow hatimaye alikubali kurejesha maombi ya gazeti la Herald kwa Mama Eddy, na kufanya jitihada kupata ruhusa ya ziara ile.

Ofisi ya Bwana Farrow ilipata barua kutoka kwa Mama Eddy kwa msimamizi wa gazeti la Herald. Barua ilikuwa imeandikwa kwa karatasi ya barua, chini ya mhuri, kauli mbiu ambayo ni “Vincere aut Mori.” Tarehe ilikuwa Machi 25, na barua ilisoma:-

“ Bi wangu mpendwa – Je unaweza kuniruhusu, kwa ajili lazima niweke msimamo dhabiti kwa makataa ya maombi ninayopata kutoka kwa waandishi wa magazeti. Sayansi ya Kikristo haiwezi enezwa kwa njia za kiulimwengu. Kubali shukrani zangu na kitabu hiki. Tafadhali soma ukurasa 464, aya ya 1. Wako kwa dhati, Mary Baker Eddy.”

Barua ilikuwa imeandikwa kwa tapureta, lakini idhini ilikuwa kwa maandishi safi ya Mama Eddy. Ni ukweli unaoonekana ya kwamba ni kwa mtindo wa kisasa, na kwa namna ya kushangaza kwa utulivu kwa mmoja wa kimo chake. Barua iliambatanishwa na nakala ya kitabu cha Mama Eddy, “Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko,” na aya iliyoonyeshwa ilisomwa kama ifwatavyo:-

“Imesemwa kwa mwandishi: “Dunia inafaidika kutokana nawe, lakini inahisi ushawishi wako bila kukuona. Kwa nini usijifanye ujulikane na watu wengi zaidi? Marafiki wake wangejua mda aliokua nao mdogo kufanya ajulikane kwa nje, isipokuwa kupitia machapisho yake yenye kazi mingi, na wakati na kazi ambayo bado inahitajika kudhibitisha shughuli za Sayansi ya Kikristo, – wangeelewa kwa nini amejitenga. Wengine hawangechukua nafasi yake, hata kama wako tayari kufanya vile. Kwa hivyo amebaki kutoonekana kwenye kituo chake, akifanya kazi kwa vizazi vijazo, asitazamie zawadi ya sasa.”

Habari ile ilikuwa yenye heshima nyingi, lakini makataa yalikaa kamili. Lakini bado gazeti la Herald halikuwa tayari kukata tamaa juu ya kusudi lake la kupata Habari ya muhimu juu ya Mama Eddy.

Kwa hivyo pendekezo lilifanywa kwa Bwana Farlow ya kwamba msimamizi wa gazeti la Herald aruhusiwe atembee Pleasant View chini ya muongozo wa mmoja wa makarani, aingie kwenye nyumba na maeneo inayozingira wakati Mama Eddy yupo katika ziara yake, na kama inawezekana, aweze kumuona kwa haraka Mama Eddy kama anaingia kwenye gari lake.

Wakati wote wa mwezi wa Aprili, ombi hili lilisitishwa, na mwishowe likakataliwa. Wakati haukufaa, makarani walitangaza, na kama wakati mwingine ukipatikana baadaye, ombi linaweza kukubaliwa. Sio mpaka mwisho wa Mei ndio swala likawasilishwa tena, wakati mtazamo mpya juu ya ripoti kadha za Mama Eddy na maelezo ambayo haikuwa kamili na ya kutosheleza juu yake ilikuwa imetokea katika magazeti, ukafanya upya hatima kwa pendekezo la mahojiano na gazeti la Herald kwa sehemu ya kamati ya uchapishaji, wakati pia iliongeza juhudi zangu kwa swala lile.

Wakati msimamizi wa Herald alisisitiza kusudi la kuenda Concord, na kutafuta habari ambayo ingepatikana, akipata ukaribisho ambao ungepatikana, meneja wa kamati ya uchapishaji aliandika barua kwa makarani wa Pleasant View, na akapatia mwaandishi hadithi hii barua ya utangulizi, akiomba heshima za nyumba na wakati wote ambao unawezapatikana, lakini si kujumuisha ombi la mahojiano na Mama Eddy. Kwa haya mwandishi lazima angetosheka.

Nimesema maelezo kamili ya shughuli hii kuonyesha uangalifu ambao wasimamizi wa Mama Eddy wanavyolinda kujitenga kwake, na sasa nahisi uangalifu huu uko na sababu, na kwamba, hata katika kutoelewana na shutuma za uongo, wasimamizi hawa wanafanya vyema kufanya wajibu wao na kusimama wima, kama ilivyo, mbele ya tuhuma za nia zisizofaa. Maisha ya Mama Eddy ni ya thamani kubwa kwa kanisa la Sayansi ya Kikristo.

Majengo na mazingira ya Pleasant View.

Safari ya kuenda Concord, N. H., kutoka Boston ni ya kuridhisha. Safari ile ya masaa mawili katika bonde la mto Merrimac, kupitia vilima vya chini ambavyo ndio kama vilima vidogo vya milima ya White Mountains, inapitisha mtu katika eneo la kilimo lenye ardhi ngumu na miji yenye viwanda mpaka kwenye mji mkuu, ulio na miti mipana yenye kivuli, nyumba za mtindo wa zamani, na kanisa nyingi. Jiji lipo, kama ilivyokuwa, kwenye beseni, ukingo wake ukiwa ni milima iliyozingira. Miti ya zamani inatengeneza paa za Kijani kibichi juu ya mitaa, na kuna mazingira ya kusinzia katika jiji.

Majengo ya umma yamewekwa katika kikundi kimoja Katikati mwa jiji, jengo la bunge, maktaba ya umma, ofisi ya posta, na jengo la jiji, na kanisa sita ama nane zikiweko pamoja kama zimezingira. Majengo mengi ni ya graniti ya New Hampshire, na hakuna iliyo na urembo zaidi kuliko la kanisa la Sayansi ya Kikristo, ambayo ilikuwa ni zawadi ya Mama Eddy kwa wafuasi wake Concord. Huu mjengo umejengwa kwa jiwe changa la machimbo, na ni ya rangi nyeupe kama marumaru. Iko na mnara mrefu, ambao ni ya sura nne na nzuri, na ambayo inapanda ikianza na msingi mpana mpaka wembamba wa juu, ambako kumewekwa kengele za duara ambako nyimbo za sifa za zamani zinasikika kwa mji wote kila Jumapili asubuhi.

Nilifika mjini Jumamosi alasiri, na ni kapelekwa mara moja kwenye mtaa wa Pleasant, kupitia hifadhi la jimbo, na mazingira yake mazuri, kupitia nyumba ya wazee, na kupitia majumba mazuri ya kibinafsi, mpaka, labda maili moja kutoka Katikati mwa jiji, nikafika maeneo ya Pleasant View.

Mahali pale pako kusini, na Magharibi mwa jiji. Kwenye mteremko wa ekari mia moja kutoka kwa Barabara ya mlima mpaka mto wa Blue River. Kuna ukingo mdogo wa graniti kando ya Barabara juu yake kukiwa na ua la chuma. Eneo limepangiliwa kwa maakini kama Bustani kwa usanifu wa mandhari ya Bustani. Kuna eneo la nyasi, Katikati ambako kunasimama nyumba ya ghorofa tatu, na baraza zake, na athari za mnara, ikipatiana mitazamo mikubwa ya dirisha kwenye vyumba.

Kuna chemichemi ya mapambo katika sehemu ya mbele na kiendeshi cha mviringo inafika mpaka mlangoni kutoka kwa kibarabara cha graniti, ambako kumewekwa lango ndogo la chuma. Mbele ya nyumba nyasi yateremka mpaka mtoni, na katika sehemu kadha za maeneo kuna maua ya mtakawa, maua ya pansy, hayasinthi. Kutoka kwa bustani kuna shamba la miti ya matunda, ambayo ilikuwa kwenye msimu wa maua wakati wa ziara.

Kutoka kwa nyumba njia inaelekea kwenye ziwa ndogo, ambako kumejengwa nyumba ya mashua ya kurembesha, na hapa ndio kumewekwa mashua ndogo ambayo Mama Eddy alipenda kuiendesha kwenye ziwa lile ndogo kwa wakati mwingine. Mtazamo ng’ambo ya mto ni mzuri kutoka kwa madirisha ya chumba cha Mama Eddy na kwa kweli, kutoka kwa vyumba vyote vya upande huo. Mlima wa zambarao waonyesha sura yake kwa umbali wa maili kadha, moja kwa moja mkabala kuna milima ambayo ni mahali pa kuzaliwa pa Mama Eddy.

Bwana Frye, Karani wa kwanza

Niliachilia gari langu la farasi kwenye lango na kutembea kwenye njia yenye mawe madogo mpaka kwenye mlango wa kuingia, ambako kuna dirisha zenye vioo vyenye rangi, ambazo zinapatiana picha ya urembo yenye kung’aa katika rangi ya Kijani iliyo kwenye nyumba. Kubisha kwangu kulijibiwa na mama mwenye kimo, aliyenisalimia kwa tabasamu, na kuchukua kadi yangu na barua ya utangulizi kwa Calvin A. Frye, ambaye ni karani wa kwanza wa Mama Eddy. Akanikaribisha na kunielekeza kwenye chumba cha mapokezi, ambako aliniacha.

Nimeongeo juu ya vipimo vya wastani vya nyumba, lakini vyumba viwili vya mapokezi ambavyo viko katika magharibi mwa nyumba ya chini, zimepangwa kuonyesha adhari ya utukufu. Zimetundikwa kwa brokedi ya ua la waridi, na mkeka mweupe, na pazia nyepesi dirishani. Zimejaa mwanga wa jua, na ziko na picha nzuri za kuchorwa, moja wapo ikiwa picha ya Mama Eddy, ikisimamia kama amesima kwenye madhabahu ya kanisa lake la Boston.

Nilikuwa tu na wakati mdogo wa kutazama uzuri wa vyumba vile, wakati bwana Frye alishuka kwenye ngazi na kunikaribisha kwenye maktaba, upande wa pili wa ukumbi. Hiki ni chumba kidogo cha mraba, kilichojaa vitabu vilivyofungiwa na milango ya vioo, ikiwa na michongo mizuri ya chuma ikiwa juu ya visanduku vile. Samani ni ya Ngozi, na ni ya starehe, inayofaa kuishi, yenye mtindo wa zamani. Bwana Frye akaketi mkabala nami, na kuniangalia kwa mawazo kwa mda bila kuongea. Alafu akasema: –

Sitaki kuonekana asiyekuwa na ukarimu kwako baada ya kufanya safari ya kuja Concord, lakini siwezi fanya zaidi ya kukubalisha kuona sebule zetu, na kuongea nawe kwa mda mfupi. Niko na shughuli kila siku na kazi muhimu tukiwa na Mama Eddy, na yeye, bila shaka, hawezi sumbuliwa.

Nilimwangalia Bwana Frye kwa upande wake, na pia nikabaki kimya kwa mda kidogo. Ni mtu aliyeonekana kuwa mtu wa ofisi, na nywele yake ikiwa nyeupe kidogo. Alikuwa amesumbuka, na kukasirika kidogo kwa ziara yangu. Alikuwa anakaa kuiharibu kazi ya miezi mitatu kwa kutoa makataa yake juu ya ndoto yangu.

“ Nataka kuona nyumba na maeneo, kwa uhakika; mahali popote kwenye nyumba yako ambako unaweza nionyesha,’’ nikajibu. “Lakini pia nataka kumuona Mama Eddy.”

“ Sina uwezo wa kuamrisha wakati wa Mama Eddy. Nimemjulisha kuhusu maombi yako, na hajaona ikiwa sawa kuonana nawe,’’ akasema Bwana Frye. “ Ako na shughuli, na hataki kusumbuliwa.’’

“ Shughuli yake ni ya kanisa la Sayansi ya Kikristo?”

“ Kwa wakati huu anashughulika na mambo ya kibinafsi, na makarani wake wako kazini kumsaidia.”

“ Haikua kusidi langu kuuliza asili halisi kuhusu biashara yake kwa wakati huu,” nikaelezea. Nilitaka kupendekeza shughuli niliyokuja nayo ni ya umuhimu. Niko tayari kungoja Concord mpaka wakati ule Mama Eddy ataweza kuniona. Kama Mama Eddy ni mgonjwa, sitangoja; Kama Mama Eddy sio mgonjwa, nitangoja kwa subira ambayo nitaipata, nikijua hatimaye utaelewa kuwa shughuli yangu ni muhimu.”

Bwana Frye akawaza. Kwa sasa akasema: “ Kama nilivyokuambia, siwezi mshawishi Mama Eddy kufanya kitu chochote ambacho hataki kukifanya. Nitamwambia ulivyosema. Kwa sasa nitaagiza uonyeshwe mahali hapa, na nitatumana ili ujulishwe vile Mama Eddy ameamua. Natumai habari itakuwa ya kuridhisha.”

Kwa wakati huu kengele ya stima ikalia katika chumba kilicho juu, na kukaja mtu aliyemuita bwana Frye. Nilisikia sauti ya kupendeza ikiongea naye, alafu milango ikafungwa, na nikawachwa peke yangu kukagua maktaba kama nilitaka.

Baada ya kuangalia picha mbili ambazo zilikuwa za kuvutia zaidi, mojapo ya “Christ au Diana?” ingine “ Danieli katika pango la simba,” mwanamke mwingine akaja kwangu, mwanamke ambaye nilikuja kujua baadaye kwamba alikuwa Mama Laura E. Sargent. Alikuwa na uso wa kupendeza, na akaniangalia kwa tabasamu kidogo lililokuwa na swali, ni kama alikuwa kwa hali ya hisia kunichokoza juu ya uvumilivu wa waandishi wote wa Habari. Lakini akasema: –

“Kama utanifuata nitakujulisha kwa msimamizi, na atakuonyesha eneo nje ya nyumba na zizi.”

Tulipita kwenye chumba cha mankuli na jikoni, ikinipatia nafasi kuona kwamba, mpaka kona zote za nyumba, mpangilio urahisi na ufahari mdogo uliendelea. Mhudumu, August Mann, alikuwa anatungoja na akakuwa msimamizi.

“ Muonyeshe kila mahali, na kila kitu anachotaka kuona,” akasema Mama Sargent, kwa fadhili, na Bwana Mann akataabasamu kwa njia kubwa, na iliyokamilika, – tabasamu la kutoa tashwishi la Thomas kwa sababu yuko na sura ya urafiki.

Ziara kufanywa Pamoja na msimamizi

Zizi zajumuisha nyumba ya gari la farasi, zizi na mabanda ya ng’ombe. Kwanza nilionyeshwa magari ya farasi. Gari la Mama Eddy lilikuwa limeoshwa baada ya ziara yake ya kila siku, na nilipatiwa ruhusa kuketi ndani yake ili nione vile iko na starehe. Ni gari lenye milango miwili iliyo na springi za kufanya urahisi kuendesha gari. Ilikuwa imewekwa kitambaa cha Kijani kibichi, na taa za fedha na iko na alama ya herufi ya Mama Eddy kwenye mlango.

Mwavuli wa Mama Eddy na kitambaa chepesi zilikuwa bado kwenye kiti. Mlikuwa na kipochi cha vitambaa cha harri ya rangi ya lavenda kilichokuwa kinaning’inia toka kwa kasha la kadi mbele ya gari, na saa iliyokuwa ndogo iliyokuwa katikati mwa kasha hili na chupa mbili za kristali zilizokuwa katika mfuko wa ukuta. Hizi chupa ndogo zilikuwa zimekusudiwa na watengenezaji wa gari kama chumvi ya kunusia, manukato, au vitu vidogo vitamu lakini nilipoziona zilikuwa wazi, na zilionekana vifaa vya kurembesha tu.

Kiti cha gari kilikuwa chenye starehe, kikiwa kimepambwa na mito yenye hewa, ikiwa mahali pazuri pa kupumzisha mgongo.

“ Unafikiria unaweza furahia starehe ya aina ile kwa safari ndefu?” akauliza Bwana Mann.

Mlikuwa na magari mengine ya kukokotwa katika vyumba tofauti, gari moja la zamani lililotumiwa kwa musimu wa baridi, lakini ambalo bado ni nzuri; lingine ambalo ni nene na linatumiwa na familia, lingine ndogo la safari ndogo, na lingine lililo na paa.

Kwenye mlango unaoelekea kwenye zizi kuna kichapisho: “ Kwa wakati wowote ongelesha farasi kabla ya kuingia kwenye zizi.”

Tuliingia kwenye zizi na Bwana Mann akaongelesha kila mnyama, akiwaita kwa majina. Dolly na Princess ni farasi wa gari la Mama Eddy. Ni Wanyama wakubwa waliowazuri walio na rangi ya kahawia, lakini sio wa ukoo maalum wa kidamu. Kuna farasi wengine wawili, – Jerry na Bess, ninaamini, – wanyama wa kawaida waliolishwa vizuri.

Lakini katika zizi la Ngombe tuliwaona Ngombe wawili wadogo waliokula nyasi nyepesi. Zilikaa kama swara wadogo kwa rangi na umbo, na kwa urembo wa macho, na wakaja kwa wito wa msimamizi ni kama walikuwa wa kufugwa wenye thamani.

Baada ya kugusagusa mapua yenye unyevu ya ng’ombe wale wadogo tulienda kwenye banda la mimea, na kutazama mimea ambayo inatayarishwa kupelekwa kwenye shamba, tukatazama vituo vya kuzalisha na baadaye tukapitia kwenye nyasi ambayo ilikuwa na ulaini, kuchunguza mmea wa karne, ukiwa na matawi yake marefu yenye ya samawati yenye maumbile ya upanga.

Wanaume wawili au watatu walikuwa kazini wakichukua maua ya dandelion kutoka kwa nyasi, na kukatakata kwenye ukingo mwa njia. Nilikuwa nimewaona wanaume wawili kwenye zizi, na kwa kutazama mlikuwa na wanaume wahudumu kadha ambao walikuwa wameajiriwa. Uhifadhi wake wa maakini wa kupalilia na kuchunga mimea ulionekana, kwani kila mahali kulikuwa kumehifadhiwa kwa kupendeza. Katika nyumba ndogo ya msimu wa njua tulisimama, na msimamizi akanikaribisha kuchukua maua ya pansy ambayo nilitaka. Bwana Frye alikuja kwangu pale, na akaambia msimamizi kutuma gari la kukokotwa kwenye mlango kunipeleka kwenye hoteli.

“ Mama Eddy atatumana kesho juu ya wakati ambao unaweza kuja kumuona,” akasema, na akatikisa mkono wangu kwa uchangamfu.

Ujumbe kutoka kwa Mama Eddy

Jumapili asubuhi nilihudhuria ibada katika kanisa la kwanza la Kristo, mwanasayansi, katika Concord, na baada ya ibada, ambayo huwa fupi kwa yule ambaye amezoea ibada refu yenye matambiko, nilienda kwa matembezi, kama bado sijapokea ujumbe wowote.

Nilikuwa natembea kwenye njia nikielekea upande mmoja kwa jumla kwa upande wa Pleasant View, wakati nilipomuona Bwana Mann akiendesha gari lake akija upande wangu. Akasimama kwenye ukingo mwa barabara na akasema alikuwa amekuja kunichukua. Mama Eddy alikuwa ameamua kuniona kwa dakika chache saa saba. Tulienda Pamoja kwenye gari kuelekea kwenye nyumba, na wakati huu, nilipokuwa natembea kwenye njia ya kuingia, nikasikia piano, ambayo kuna mtu alikuwa anaicheza kwa upole, na kabla yangu kubonyeza kengele, kicheko.

Hofu yote ya ujinga kuhusu siri kuu katika Pleasant View ikashuka mara moja kama vazi la chuki. Nikaona uzuri wa maisha mazuri ya nyumbani, yakiwa ya kiasili na kwa makubaliano hapa katika mpangilio huu mzuri kwa boma hii ya mashambani.

Msimamizi wa nyumba akajibu kupiga kwangu kwa kengele kwa hafla hii, na akasema angepeleka kadi yangu kwa Mama Eddy. Nikaenda sebuleni na hapo nikakutana na Mama Sargent tena, na Kijana mdogo, karani mdogo, aliyekuja Pleasant View maajuzi, ni yeye aliyekuwa akicheza piano.

Mhudumu akaja kunichukua na akasema: “Mama Eddy atakuona sasa.”

“Tunaenda nawe, sio?” nikauliza Mama Sargent.

“Nitatembea nawe mpaka kwa mlango, kama unapenda,” akajibu. “ Lakini Mama Eddy angependa kukuona peke yako.”

“ Nawezaongea naye?”

“ Bila shaka. Hii ndio maana uko hapa,” akataabasamu Mama Sargent tena, akiwa na ucheshi wa swali.

Tukaenda juu kwa ngorofa mpaka kwa chumba cha masomo cha Mama Eddy ambacho kiko katika chumba cha mnara na sebule kwa upande wa dirisha. Mama Sargent akaniacha kwa mlango, na kwa kushangaa kwangu, akaufunga mlango baada ya kuondoka. Nikamuona mama aliyekuwa na nywele nyeupe akiwa amesimama kwenye dirisha akiwa amenipa mgongo. Akasimama pale kimya kwa sekunde kadha, alafu akagheuka akaja kwangu. Akanyoosha mkono wake kwangu na kutaja jina langu.

Alikuwa anafanana na picha iliyokuwa chumba cha chini ambayo niliitazama kwa karibu, na kila kipengele kilikuwa ni mfano wa picha ambayo dunia inajua kama mwanzilishi wa Sayansi ya Kikristo. Alivaa gauni ya hariri ya rangi nyeusi ikiwa na lace adimu ikipangwa kwa mtindo wa fichu kwenye shingo. Nywele yake ilikuwa nyeupe kabisa na imepangwa vizuri mbali na uso. Ngozi yake ilikuwa na ulaini wa mwanamke mzee, na hata kama ilikuwa sawa na iliyokaribia kuwa kama kioo, haikuwa imeguzwa kwa njia bandia. Mkono alionipa kwa salamu ulikuwa mdogo na ulioumbika vizuri. Kwa maumbile lazima alikuwa kama futi tano na inchi tano.

“ Vurugu hii yote kuja kuniona masikini mimi,” akasema Mama Eddy, akiniangalia kwa macho yaliyong’aa, akitabasamu kwa wema.

“ Nahisi kubahatika na kuheshimika kwa nafasi uliyonipa.”

“ Lakini mbona, mtoto wangu mpendwa? Ni kwa nini watu wengi wanataka kuniona?”

Sikuweza kujibu. Nilihisi kuzidiwa.

“ Yote ambayo nauliza kutoka kwa ulimwengu sasa,” akaendelea Mama Eddy, kwa sauti iliyokuwa na utamu wa kengele ya fedha, “ ni unipatie wakati, wakati wa kujiingiza ndani ya Mungu.”

Tena nikawa kimya, kwa sababu mlikuwa na nguvu na maamuzi katika kila neno ambalo lilitajwa kwa upole. Nguvu ilikuwa kama amri kutoka kwa akili iliyokuwa imezoea kutiiwa.

“ Umetosheka ya kwamba umekutana nami, na kwa kuwa nimekubali maombi yako yote?”

“ Nimetosheka,” nikajibu.

“ Ningependa kutosheleza kila ambaye angependa kuniona,” akaendelea Mama Eddy. “ Ningependa kuwakaribisha wote , niwachukue kwa moyo wangu. Lakini siwezi, naweza sema tu kwao ambao wanathamini azma hii, “ Tazama Ukweli na sahau utu wangu.” Yote ambayo nauliza ulimwengu ni wakati.”

Nikainua mkono wa Mama Eddy kwenye mdomo wangu, na nikainama kwa mapenzi yake ya kusitisha mahojiano. Akagusa paji langu la uso kwa vidole vyake, na akainua mkono wake kama aliyetaka kunibariki nilipokuwa natoka chumbani. Mtazamo wangu wa mwisho ulikuwa kama anasimama pale, akiwa kama kijana, akiwa anatawala kwa mtazamo, na kwa upole, kama maua, na kwa mapenzi. Kitendo chake cha mwisho kilikuwa kupunga kwa mkono aliouinua.

Hazina katika nyumba

Bwana Frye alikuwa ananingoja kwenye ukumbi na akanipeleka sebuleni. Pale niliwapata familia imekusanyika, Mama Pamelia J. Leonard, wa New York, Mama Sargent, na karani msaidizi. Mama Eddy alikuwa amewaambia wanionyeshe hazina kadha zilizokuwa kwenye nyumba, na walikuwa wananingonja kutimiza matakwa yake.

Kati yake mlikuwa hati ya kukunjwa ya dhahabu ambapo kulikuwa kumeandikwa ukaribisho kutoka kwa kanisa la Mother church Boston kwa Mama Eddy wa kutembea na kukubali jengo kama ukumbusho kutoka kwa mikono ya washirika elfu nne. Hati hii iko katika kijisanduku juu ya meza ambayo imetandazwa kitambaa cha hariri kilicho na maua, kilicholetwa kutoka Pekin na Mama Conger, mke wa aliyekuwa waziri Uchina, ambaye, kawa anavyojulikana vizuri, ni mfuasi mwaminifu wa Sayansi ya Kikristo, na ambaye alifuata imani yake kati ya wafungwa waliojaa hofu katika uzingiraji wa Pekin wakati wa uasi wa mabondia.

Chini ya meza hii kuna mkeka wa mbuni uliotumwa kutoka kusini mwa Amerika. Kwenye meza ingine mlikuwa na nakala ya “ Bohemia,” iliyotengenezwa kwa Ngozi, iliyochapishwa vizuri na kuangaziwa, ikiwa ndio toleo la pili la toleo kuu la nakala hamsini za kazi hii, nambari hii ikichapishwa juu ya Mama Eddy. Kuna picha kubwa ya kushonwa kwa ukuta mmoja, ya Yesu kama mchungaji mwema, ikiwa na maandishi, “ Bendera yake juu yangu ni Upendo.” Picha ingine ambayo imethaminiwa na Mama Eddy, aliyokuwa amepatiwa na mwanafunzi, ni “ Malaika wa Ufufuo.”

Kwenye meza katika sebule ya nyuma mlikuwa na miiko miwili ya fedha ambayo ilitumiwa kuweka mawe ya msingi ya makanisa ya Concord na Boston. Mwiko wa mwashi wa Concord ulipatiwa Mama Eddy na Bi Victoria Murray, binti ya Bwana Dunmore.

Katika maktaba mna kikombe kilichopatianwa na washirika wakuu wa kanisa la Boston. Hiki ni chungu kizuri chenye nakshi iliyoinuka cha fedha, chenye ukingo wake kuna lulu wakubwa kumi na wawili. Kuna wengine wadogo katika chumba hiki walio wa thamana na wazuri. Kuna picha za mfalme Edward na Malkia Alexandria wa Uingereza, na picha ya “The Madonna and child,” na “ The Holy Family,” iliyochorwa na mwanafunzi wa Raphael, na kupatiwa Mama Eddy na Bwana Abinger. Kilele chake kiko nyuma mwa fremu, na chini yake kuna maandishi, “ Kutoka kwa Abinger, mwenye kuvutiwa, kwa Mchunganji Mary Baker Eddy.”

Kwenye ukuta kuna mkeka ulio tengenezwa kuwa wa malkia, na ambao thamana yake ni $5000; lakini hakuna ambaye angepatiana historia yake. Mkeka ule ulikuwa umeshonwa kwa mikono, na ulikuwa unahitaji miaka kumi na nane kuutengeneza. Mlikuwa na Bibilia mzee ambayo ilichapishwa mwakani 1551, na saa ya zamani ambayo ilikaa kuwa na historia ambayo imefichika. Pia kuna saa mzee nzuri iliyokuwa kwenye ukuta, ambayo mlio wake wa kifedha kwa kila robo saa. Ilipatianwa na kanisa lake. Kwa aina yake ziko chache ambazo zinapatikana.

Maisha ya kila siku katika “ Pleasant View.”

Tulitembea kwa dakika chache baraza ya nyuma, ikiwa Mama Sargent akishuhudia kitu kuhusu maisha ya kila siku katika “ Pleasant View.”

“ Mama Eddy huamka mapema,’’ akasema. “ Yeye hukula chakula chake kwa masaa inayotakikana bila kuchelewa, akija kwenye chumba cha chini kwa mamkuli. Hali kwa mitindo kuhusu chakula chake kwa njia yoyote, hajawaiacha kukula nyama, wala kwa njia yoyote haonyeshi sifa ya kipekee kuhusu lishe, ila, bila shaka, amekuwa wa wastani juu ya hamu ya chakula. Angependa kufanya mazoezi zaidi kuliko anavyofanya, lakini hakuna uwezo wa kutosha wa kujitenga katika boma hii, kama unavyoona. Anaweza tembea hapa kwenye baraza, na anaenda kwenye safari zake za kila siku ambazo ni za lisaa limoja kwa urefu.

“ Anapenda mpangilio na uzoefu kuliko kila kitu, na anapenda kuona shughuli za nyumbani zikiendelea kwa utaratibu. Pia anapenda kuwa na familia karibu, kama unavyoona. Saa zingine hutupilia kazi zingine zote na kuziweka kando ili kutunga na kuandika mashairi. Uandishi wake ni bora sana, na anaweka alama za uandishi kwa uangalifu mkuu.

Anatia uangalifu wa kibinafsi katika barua za kila siku, ambazo ni nyingi. Yeye hujibu barua nyingi kwa mwandiko wake, akiandika kwa haraka bila kutumia nguvu yoyote; lakini zingine nyingi zinajibiwa na karani wake kwa kuamrishwa.

Yeye husimamia biashara zote zinazofanyika hapa, akisimamia biashara za karani wake. Saa zigine anatumia mda mrefu katika tafakari na anapenda kutazama upande mwingine wa mto kwenye mlima wa Bow Hill, pahali alipozaliwa. Aliambia mmoja wa walio katika nyumba siku nyingine juzi ya kwamba alijua kila mahali katika eneo lile, na ya kwamba angeona kaunti saba kutoka kwa dirisha lake.

“ Maisha yetu hapa ni rahisi sana ingawa yenye shughuli mingi. Lakini ni maisha yaliyotengwa kwa Mungu, na kila siku hukaa kuleta baraka mpya kwa uhusiano na maisha haya mazuri ya Mama Eddy. Yeye kila wakati ni mtulivu, mnyenyekevu, na haja yake ni kuishi maisha matakatifu. Sisi ambao tunatumia siku zetu katika “ Pleasant View’ tuko na nafasi ya kukua kwa namna ya ajabu katika kanuni za imani ya Sayansi ya Kikristo.”

Gari lililetwa kwenye mlango tena, na nikapelekwa hotelini. Mahojiano ya kibinafsi na Mama Eddy yameelezewa kwa uaminifu. Niliwaachia makarini wake muhtasari wa mahojiano na Mama Eddy tuliokubaliana ataangalia kwa wakati wake, na kuamrisha majibu yake. Hii ilijumuisha maswali ambayo itahusisha mazungumzo marefu ambayo itafanyika kwa wakati mmoja. Maswali baadaye yalizingatiwa, na kupatianwa kwa gazeti la Herald na maoni ya Mama Eddy kama yafuatavyo:-

Maswali yaliyojibiwa na Mama Eddy.

Sayansi ya Kikristo ni dini mpya? Ndio, dini mpya na ya zamani na Ukristo.

Iko na msimo kuhusiana na Ukristo kama vile Ukristo ulikuwa na Uyahudi? Kwa kiasi Fulani.

Wewe kama Mama Eddy ni mtafsiri wa mafundisho ya Yesu, au umepatiana yale ambayo ni mpya katika mafundisho yake? Mimi ni mtafsiri.

kitabu cha Sayansi ya Kikristo ni moja na Neno la Mungu kwa hisia moja na Bibilia? Ukweli wote ni wa Mungu, na Sayansi ya Kikristo ni ukweli wa milele, unaodhibitishwa, kulingana na kanuni inayostawi na sheria zinazoweza kudhibitishwa.

“ Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko” ni utimilifu wa agano jipya wa ufunuo wa siku za usoni.” Ndio.

Sayansi ya Kikristo inazozana na sayansi ya kiasili? La sio kwa sayansi ya kiasili ya kiroho. Hakuna sayansi ya maada.

Inakataza kusoma kwake { Sayansi ya Kikristo} au sehemu yoyote yake? Inapokewa kwa kusoma na usahihi.

Sayansi ya Kikristo inakataza masomo ya mwili, fiziologia, na usafi? Sio kwa usafi wa kiroho

Sayansi ya Kikristo inakana uhai wa viini vya ugonjwa, au inasisitiza ubora wa binadamu juu ya nguvu zile? Inakana kuwepo kwake.

Ni sahihi kwa mwana Sayansi ya Kikristo kutozingatia sheria za usafi au kuzitupilia wakati hali ni muhimu? Kupuuza haya yote inakana ukamilifu wa Mungu, Roho, na sheria zake.

Mwana Sayansi ya Kikristo na atumie utamaduni wa kiasili, atumie lishe bora, au atumie hewa safi kama tiba na kama msaada wa uzima wa mwili? La, si lazima.

Kwa hali inayowezekana, Mwana sayansi ya Kikristo anaweza tumia upasuaji? Ndio, na la.

Kwa uwezekano wa ugonjwa wa kuambukizwa mwana sayansi ya Kikristo anaweza jipatiana kwa matibabu ya kutengwa na matumizi ya madawa ili kuua viini vya ugonjwa? Kama Sheria inadai, ndio.

Sayansi ya kikristo inachukulia umasikini kama udhihirisho wa ugonjwa? Hapana

Umasikini ni ugonjwa wa mtu binafsi au jamii? Zote mbili.

Mtu binafsi anaweza shinda kushindwa na mambo ya dunia akitumia Sayansi ya Kikristo? Ndio

Kuna mafundisho katika Sayansi ya Kikristo kwamba uovu unaweza pendekezwa dhidi ya mwingine kama wema? Haya mafundisho ni udanganyifu. Sayansi ya Kikristo inaweza toa adhari nzuri pekee.

Akili ya uovu iko na nguvu dhidi ya maisha ya kiroho? Uovu unafanya kazi dhidi ya wema wote, kama unafanya kazi yoyote.

Unachukulia kifo kama hofu kubwa ua dunia ambayo wanadamu wanauelekeza kwao wenyewe? Ndio

Kama Dunia itaachana na masomo ya magonjwa na uhalifu, na kujitweka katika kusoma juu ya utajiri, afya, na upendo, wahalifu, viwete, na umasikini zinaweza isha? Ndio zinawezaisha.

Sayansi ya Kikristo inatetea kumalizwa kwa taasisi za hisani na pia mahospitali? La

Jamii inawezaishi bila magereza na nyumba za masikini? Sio kwa sasa.