Kadi
Kiongezo Kilichoongezwa Kwa Toleo La Julai 1891
LA Jarida la Sayansi ya Kikristo iliyoandikwa na Mary Baker Eddy
Kuona umaakini wangu ulivutiwa na makala ya jarida la mwezi Mei,nafikiria ingekuwa hekima kutoandaa USHIRIKIANO WA JUMUIA WA KUTOA KAZI ZA MAANDISHI YA SAYANSI YA KIKRISTO.
- Sababu siamini huduma ya shirika lililo enea kwa upana.Iinawezesha kukuza mashirika ya kibinafsi,sheria za darasa na nia isio ,ya ukristo kwa kazi ya ukristo.
- Ninawaona wanafunzi wangu wakiwa na uwezo, ubinafsi, wa kuchagua kazi za kusoma wao wenyewe na kuzisambaza, kama vile kamati ingekuwa ile imechaguliwa kwa kusudi hii.
Sitakuwa na jambo lingine la kusema kuhusu maada hii, lakini natumai hitimisho la wanafunzi wangu itachukuliwa kwa busara, na itakuwa ya kukuza maslahi ya wale wako nje, na pia wale wako ndani ya shirika hili.
MARY B. G. EDDY
TANGAZO
Kuamka kwa ukweli ni kuwa mbinu na njia za kimwili haziwezi kuingizwa katika onyesho la vitendo na kazi ya sayansi ya Kimungu na hasa kwa kusambaza maandishi ya Sayansi ya Kikristo, nakumbuka ombi lililofanywa kwa jarida la Mei, kwa jina ” kwamba wanasayansi wajiandae kwa uenezaji kwa utaratibu wa maandishi ya Sayansi ya Kikristo,” na kutangaza muungano wa jumla wa kutoa maandishi ya Sayansi ya Kikristo isiyo na mpangilio kutoka tarehe ile.
CAROL NORTON,
Katibu mkuu
New York, June 26, 1891