Uponyaji wa mda |

Uponyaji wa mda

Kate Buck


Anayetafuta uhuru, na anapata imecheleweshwa, anajaribio la kuuliza, mbona nachukua mda kupona? Nasoma na kutafiti kwa uaminifu, nafanya yote ambayo yanatarajiwa kutoka kwangu, ” naomba bila kusita,” lakini hali haibadiliki. Wengine wanapona haraka, bila ufahamu wote dhahiri au maarifa ya Sayansi, na kuonekana bila bidii yoyote kwao. Hii inaweza kuwa kweli; lakini ukweli unabaki ya kwamba kila mmoja lazima atembee kwa njia yake na ajifunze somo linalopatikana mle.

Uponyanji wangu mwenyewe katika Sayansi ya Kikristo ulikuwa polepole. Mantiki na nadharia za Sayansi ya Kikristo ilikuwa wazi kwangu kwa mwenzi moja ama miwili, lakini kuiamini na kuifanya iwe ya vitendo, ilichukua miaka.

Nawezaona sababu kadha za kupona kwa kuchelewa. Kwanza niliamini kabisa kwa uhalisi na nguvu za uovu ambao niliteseka nao. Basi pia nilitaka kuponywa juu ya yote, na hii kwa wakati mwingine ni mkasa. Nilisoma nakala na wazo la kupona akilini mwangu. Ningesoma kauli yenye nguvu na kufikiri, “Labda hii itaniponya.”

Ningependa kuonya wengine kwa dhati dhidi ya destruri kama ile. Nilifikiri wataalamu walikuwa wakipoteza mda wao wakiongea sana kuhusu Mungu,kwa sababu sikuwa natafuta dini. Nilikuwa natamani tu niwe huru kutokana na mateso. Kikwazo kingine kilikuwa ni kwamba nilijihurumia. Kujihurumia ni kama sumu. Inakaa wengine hupona haraka lakini sikuwa mmoja wao. Nashukuru sana kwa yote na kwa hatua zote njiani, ingawa vile ngumu ilionekana.

Ni muhimu sana kwa watu wengine kusukumwa kwa upweke, hakika ndio wapate na wajijue kama watoto wa Roho; ndio wajifahamishe na nafsi ya kweli ambayo hawajawai kukutana nayo.

Hii inachukua mda, utafiti, mawazo na kujitakasa; kuachilia polepole kwa imani za zamani na tabia, kutupilia makosa mengi, mengine ambayo yalifikiriwa kuwa ya maadili mema; kubadilisha kwa elimu ya uongo, na uchambuzi mpya wa nafsi kutokana na msingi mpya.

Wakati mwingine mtu atasema, ” sijali vile njia inachosha, kama nimepona. Lakini inakaa nikama sipati nafuu licha ya bidii ninayoweka.” Hii kamwe sivyo kwa sababu uhuru unapokuja, mtu atajipata ameendelea kwenye barabara kupita vile alivyoota angekuwa.

Kwa kuwafariji wasafiri wa aina ile Mama Eddy anaandika, ” Kama juhudi zako zimezungukwa na hali zinazotisha, na haupokei zawadi ya sasa, usirudi kwa uovu, au kuwa mvivu kwa mbio. Wakati moshi wa vita utaondoka, utashuhudia yale mema umefanya, na utapokea kulingana na vile unavyostahili. Upendo hauna haraka ya kutukomboa kotoka kwa majaribu, kwa sababu upendo unamaanisha ya kwamba tutajaribiwa na kusafishwa.” {S&H ukurasa wa 22}

Najua kwa tajiriba yangu haikuwa mpaka siku moja nikaweka nakala chini na kusema, ” Naam, iwe kama nitawai pona ama la, niko na uhakika nampata kumjua Mungu kuliko vile nilimjua hapo mbeleni.” Kisha hali nzuri zikaanza kudhihirika. Niligeukia Sayansi ya Kikristo na wazo la kumpata Mungu. Kisha mateso yakapungua na mwishowe kutoweka. Nilifikiri kidogo kuhusu mwili na kwa asili ikanisumbua kidogo.

Sio kwa njia isiyokuwa ya kawaida, na hisi huruma kwa kina kwa wale wanaoneka wakipokea uhuru wao polepole, kwa sababu najua changamoto za matumaini yaliyohairishwa, lakini lazima niongeze ya kwamba najua mengi, mengi kuhusu ushindi wake.

Basi na tuendelee kwa kustajimili; tuwekeni ujasiri na imani yetu kwa Mungu, mpaka kujapo kwa wakati wa furaha, ambapo tunaweza sema kama Paulo alivyosema, ” Nimepigana vita vizuri, nimemaliza mkondo wangu.”

Kujitahidi kwa dhati zaidi, kujitahidi, kushinda, siku kwa siku ndio kitu kimoja kinachohitajika kama “tunafikia alama;” lakini muumini hayuko pekee kwa sababu amejifunza ya kwamba Baba wetu wa mbinguni ako pamoja na yeye kwa kila hatua kwenye njia.