Mungu hutawala Mataifa |

Mungu hutawala Mataifa

Iliyoandikwa na Peter V. Ross


Katika nyakati hizi ngumu kila mtu anaweza fanya jambo la kusaidia kutatua hali hii. Anaweza sisitiza ya kwamba Bwana Mungu mwenye nguvu zote anatawala. Hii ni njia ingine ya kusema ya kwamba Kanuni inatawala dunia na mataifa, inatawala biashara na viwanda, inatawala binadamu na masuala yake, ikitengua nguvu zisizokuwa na kanuni ambazo hugadhabisha jamii, kuharibu biashara, anzisha vita, au kwingineko kuingilia uzima wa binadamu. Ni wakati wa kukabiliana na mwingiliano huu wenye uharibifu, sio kwa hofu, lakini kwa uhakika ya kwamba hauna nguvu za kushinda mpango wa Kimungu kuhusu hatima ya binadamu. Katikati mwa kelele kali za leo, kila mmoja, kwa msaada wa Sayansi ya Kikristo. anaweza tembea duniani kwa heshima na ujasiri.

Katika hafla tofauti, Yesu alipita bila kuonekana katikati mwa vikundi vya watu vilivyotisha; akaingia kwenye vyumba bila kufungua milango; akawalisha watu wengi na mikate michache na samaki, mipaka ya binadamu ilifanywa bure na huyu mwanamume wa Galilee. Na haya yanaweza dhibitishwa na mtu yeyote anayefahamu , kama Yesu, ya kwamba binadamu na ulimwengu ni za kiroho.

Kwa mtu huyu, kuta hutoweka; umbali husonga nyuma; ukosefu unamezwa na wingi; hatari inapitwa na usalama. Katika ulimwengu wa kiroho ambao ni wa kweli, hakuna vizuizi, hakuna vikwazo, hakuna kifo, vizingiti, hatari, ukosefu upo katika hisia za kiasili. Na zitapotea kama akili ya binadamu inatoa nafasi kwa Akili ya Kimungu, na hisia za kiasili zinapatia nafasi hisia za kiroho. Kwa binadamu wa maumbile ya Mungu, usalama na amani ni kawaida, na anatembea duniani katika amani.