Fedha
Mkusanyiko wa maandishi na BICKNELL YOUNG
Unaona, ya kwamba kama uko na ufahamu wa kutofaulu, kutoweza, na umasikini, ni vingumu kubadili dhihirisho ya mambo haya kwa nje, kwani ufahamu utajionyesha wenyewe, haijalishi ufanye nini. Badilisha ufahamu.
Ni bure kujaribu kuwaza vitu na kuzifanya ziwepo. Fanya vile Yesu alivyofanya, wakati aliacha utendaji wa Akili kufanya kazi. Tunamuona Yesu akipitia hatua rahisi za udhihirisho. Aliinua macho yake juu mbinguni na akashukuru. Alikuwa tayari amepuuzilia mbali kuonekana, na alikuwa ameachilia mawazo ya vipi,lini, na wapi;hii ikiwa kabisa nje ya jimbo lake.
Tukizingatia hali za maisha, wakati mwingine tunaipata ikiwa ngumu kudhihirisha matamanio ya moyo. Lakini tunapo achilia ” mchakato wa mawazo” tunagundua ya kwamba nguvu za Mungu ni kuu kuliko chombo na vyombo vyovyote kupitia au kwa njia inayofanya kazi.
Kama uko chini ya Roho, hauko chini ya laana ya sheria tena. {Mungu – nguvu kabisa ako nje ya uchukuaji wa fikira.}
Kutokuwepo kwa mwili, na kuwepo na Bwana, inakuwa sheria inayobadilika, ambayo inafanya kazi kwa njia Chanya na ya ajabu. Inatuliza moyo mara moja, kujua kwamba nguvu ni kuu kuliko chombo cha himisho.
Baba ndiye utukufu wa binadamu, ya “MIMI.” Hekalu ni umbo la utukufu, mahali ulimwengu unakuwa wa kuonekana.
Wakati kitu kinakoma kuwa na uhai katika ufahamu wako, hakiwezi kuwa na mwili au umbo.
Yesu hangefanya kitu chochote mwenyewe; hata wewe huwezi. Utasisitiza utaweza, na kuendelea kung’ang’ana na kupigana na udhihirisho, ukitumaini kubadilisha kitu? Ukiwa na ufahamu wa kitu chochote, ni ya milele katika mbingu, na inaweza fanyika tena, tena na tena. Lakini kitu kinachotolewa , kiko katika msimamo wa kutawanyika. Kinyume cha kufikiria kimeleta matokeo ya binadamu kuabudu kitu, badala ya kuangalia ufahamu ambao unakihifadhi; “Nikaribie,na nitakukaribia.” Toa macho yako kwa mwonekano, na uweke “juu yangu,” ukitaka kuona jangwa ikijaa maua kama waridi.
Fahari ya “udhihirisho” itapita, ikiwa asili kwa Mungu kufunuliwa, badala ya kuonyeshwa. Unaweza shangaa, kama maombi yako yangejibiwa? Mpaka iwe asili na kawaida, hakuna tokeo kuu linaweza fanyika.
Ni shukrani na utambuzi zilizozalisha mikate na samaki kwa wale elfu tano. Kidogo unachouliza, ndio vigumu inavyokuwa kupata, kwa sababu ya utajiri wake mkubwa. Maono yako mbaya ya yale ambayo ni yako, inakufanya usiwe na wingi wa Roho. Mtu aliye na ufahamu uliyo jaa matatizo, atayapata, pahali popote aendapo. Bila ufahamu wa dutu, hauwezi hifadhi ishara.
Nia ya shukrani, ndio kipimo kinacho hesabika. Shukrani, ambayo inaleta ubora mwingi katika udhihirisho, inafanyika katika furaha ya uwepo, kama una kitu chochote au la. Iwe umekuwa mpotovu, inajalisha vitu ndogo? Zitakuja kwa hali yake kiautomatiki. Haziwezi sita. “Mimi, nikiinuliwa nitawavuta watu wote kwangu,” ni sheria ya hesabu. Ni ajabu, kufurahi, sio kwa sababu ya ushindi au vitu,lakini kwa sababu ya uwepo. Kama furaha yako bado iko nje, ukitafuta ishara, bado uko tupu, hakuna shukrani.
“ Nitageuza, geuza, geuza…”na kwa hivyo kila kitu kitageuzwa, mpaka upate ndani yako yale Yesu alipata ndani yake: Chanzo cha yote.
Msalaba wako ni ufahamu wako wa uovu, hakuna kingine; na ni katika msalaba huu umejipigilia miaka hii yote. Unajisulubisha , na wakati ule ule unaitana utolewe kutoka kwenye msalaba. Ni juu yako. Vile Yesu alisimama mbele ya mashahidi elfu tano juu ya ukosefu, inatupatia wazo la ujasiri ambao umezaliwa juu ya utambulizi ya utendaji asili wa Mungu. Aliinua macho yake mbinguni, na akashukuru; nini hatua yako? Tazama.
Ukishika wazo, hakuna kitu ngumu kwangu, ufahamu wa Kristo. Kila kitu ni ngumu kwangu John Smith. Kama lazima uvurute maiti ya John Smith; historia ya magonjwa, na dhambi, na kikomo ndani yako, hauwezi ingia kwenye ufalme. Lakini wewe ni kiumbe kipya katika ulimwengu mpya; sio kiumbe cha zamani kilicho fanyiwa marekebisho.
Ni wakati upi utaacha kujaribu kupata vitu, na kuona uwepo wa Mungu? Roho wa ufahamu wa uwepo wa Mungu, ndio chanzo cha ugavi wote; sio ugavi mwingine: Ugavi wote. Ukijua haya hautajaribu kuwinda ugavi, au kazi, kwa sababu itawepo katika eneo moja kama lingine.Itakuwa mahali ulipo, na chochote unahitaji. Utapata uwepo wa yote.Mahali hakuna kitu kilicho kosekana. Vitu hizi zote zitaongezwa kwa yule ambaye hana uoga. Kuna sasa moja: Kwa nini uwe na hofu ya kukubali wema hapa na sasa, badala ya kungojea mavuno?
Ukifahamu wazo ya kwamba haujaribu kubadilisha nje, haujaribu kujifanisi, haujaribu kutafuta kazi, utaona wakati uko na vitu hivi katika ufahamu wako, wakati unakubali katika akili yako uwezekano wa udhihirisho, katika wakati ule ndio udhihirisho, uasili wa maumbile ya Neno, inakuwa mwili. Badala ya kupoteza wakati ukijaribu kudhihirisha ujana na nguvu mpya, kwa hatua tutaona, ya kwamba kuona kwa usahihi kanuni hii ya Kristo, ambayo ilikuwa kabla ya Ibrahimu, ni Uhai wa milele. Ya kale yamepita. Hayatakumbukwa, wala kuja katika mawazo.
Katika hali iliyoendelea ya ufahamu wa Kristo, ni vigumu kutafuta chochote kutoka chanzo kingine ila Mungu. Mara tu Roho au Akili imedhibitishwa kama ukweli pekee, dhihirisho itajishughulisha yenyewe. Wakati uko tayari kuachilia hisia iliyo na kikomo ya utu, ambayo umejitambulisha nayo, utaniona mimi, Mungu. Achilia wazo ya kwamba unajaribu kufanya udhihirisho na kuzama katika kina.
Kutambua uwepo kwaweza onekana kuwa kazi kubwa, kwa sababu akili ya kibinadamu inataka kujaribu; lakini ufunuo umepatianwa, ambapo Yesu Kristo ni rahisi. Lazima ieleweke kwa mtoto, au haitakuwa na faida kwako. Ni utambuzi, alafu kutumia.
Unafamu kuacha tatizo la kimwili, haitafaidi kitu? Kama iko ndani ya ufahamu wako, utaizalisha hata kama umeenda nchi ya mbali, kwa sababu umeenda nayo.
Ilikuwa ngumu kwa Yesu, mwanadamu, kuzalisha dutu, kama itakavyo kuwa kwako. Ni Kristo aliyefanya haya. Katika ufahamu mpya, ambao uko ndani ya kila mwanadamu, ukingojea utambuzi, kuna kuachilia papo hapo, kama unavyo tambua uwepo. Mipango mingi bila mwisho na kujaribu kupanga vitu ghafla huisha. Serikali itakuwa juu ya mabega yake, serikali ya uhai wako, na yote ni sawa. Usiwe na hofu, ni mimi.
Tazama, mashamba ni meupe. Vuna, wewe ambaye unasoma ukurasa huu; vuna ujao wa uhai kila mahali. Wakati utakuja tambua utambuzi wa uhai kila mahali ukiwemo, hakuna kitu hata kimoja kitafichwa kwako, na hakutakuwa na mahali pa dhambi, magonjwa, au kifo, na utapata kitu kipya kikifanya kazi katika washirika wako ambayo itakuwa juu ya yote afya na magonjwa; ufahamu mpya ambao sio matokeo ya kushindwa kwa uovu, lakini ni wingi wa Roho, ambayo ni ya macho safi kuona dhambi. Mwanadamu aliyepona labda ni bora kuliko aliye mgonjwa, lakini bado anayumbayumba kati ya kitu na kutokuwa na kitu.Itabidi amehamia mahali pa utambuzi, na palekuishi kwa hali ya furaha isiyo badilika. Uwezo wake hautakuwa kudhihirisha Neno, lakini kuleta uwepo wenye uhai kwenye kuonekana. Hii ndio nguvu yako, uwezo wa kukubali mema yaliyo tayarishwa juu yako. Fungua mishipi ya viatu vya sandali zako. Achilia fikira za kibinadamu; achana na kwa nini, lini, wapi. Ukipoteza ubinafsi, wacha umezwe katika “ NI MIMI.” Alafu utapoteza sheria zote za kibinadamu. Haitakuwa shida au shughuli yako, kwa sababu haitakuwepo tena. Kuwa mtulivu kwa nje na unene kwa sauti na furaha ndani, mpaka ivunje nyuta za gereza lako. “Niko na vitu mingi zilizofichwa ningetaka kuwaonyesha, wakati mnaweza tulia.” Mahali upo ni patakatifu.