Hakuna kitu kinaendelea ila Wema
Kutoka kwa Darasa la Msingi la 1936 na BICKNELL YOUNG
Ukurasa 70
Uovu wa kinyama sio kitu cha kuogopwa. Sayansi ya Akili haimo katika zile vitu inavyovishughulikia. Ukweli haupo katika kosa unalolishughulikia.
Vita ni uovu wa kinyama. Kiangazi sio ukosefu wa mvua, ni uovu wa kinyama. Unaweza tibu hadi mpaka upate rangi ya samawati katika uso wako kama kiangazi na usiende mahali popote; ichukulie kama uovu wa kinyama na utaitibu. Hali ya anga ni kitu ambacho tunaweza shughulikia kama tunaweza. Ikiwa akili ya kimwili inasema hali ya anga inatisha, inuka juu ya haya. Nani anasema vile? Hii ni nini kwa Mungu, kwa Upendo usio na mwisho, wa Kimungu, uliopo milele, ulio na nguvu zote, ujuae yote? Hali pekee iliopo ya anga ni hali ya anga ya Kimungu. Unaweza kuwa hauwezi ifikiria, lakini unaijua. Hali ya anga ni kitu ambacho Wanasayansi wanaweza fanya kitu kuihusu. Kila kitu kiovu ni imani ya mvuto, uovu wa kinyama. Tambua ya kwamba hakuna kitu kinachoendelea ila wema.