Marekani
Kutoka kwa mkusanyiko wa maandishi na BICKNELL YOUNG
Mungu anatawala ulimwengu wake wakati wote na anatawala kwa usahihi. Hakuna kitu tunachokifahamu ambacho hakiji chini ya sheria ya nguvu za Kimungu, na yale ambayo yanahitajika kwetu, inasemekana katika ile sura katika maandishi yaliyokusanywa kuhusu “Uaminifu:” Kuwa mwaminifu.
Tukio lolote, ambalo ni dhihirisho na umilele, au la Akili moja ya milele, haliwezi jirudia, kwa sababu Mungu hafanyi jambo zaidi ya mara moja. Yale anafanya mara moja hatawai fanya tena. Atafanya jambo lingine, kwa sababu Bibilia inasema, “Tazama, “nayafanya mambo yote upya.” {Ufunuo 21:5}, na Mama Eddy anasema, “Uumbaji unaonekana kila wakati, na ni lazima uendelee kuonekana kutoka kwa asili yake ya chanzo kisichoisha.” {Sayansi na Afya 507:28}
Sababu yote na lengo na kusudi la Marekani ni Sayansi ya Kikristo. Hii ndio sababu imetengwa, na haiwezi tambuliwa kwa yale yanajulikana kama mataifa. Mwanadamu anajitawala, na hakuna serikali ingine. Katika Sayansi na Afya ukurasa 125:16, tunasoma: “Akiangaza serikali ya Mungu, mwanadamu anajitawala.” Hii ni Sayansi ya Kikristo. Kwa hivyo nchi yetu, ikisimama vile imesimama kwa binadamu akijitawala, inasimama kama kanuni. Hii ndio inaifanya iwe vile ilivyo. Kwa nini tena tuko kila mtu akitengeneza sheria kwa watu wengine? Matokeo ni hakuna anaye jitawala, ila asisitize kuwa vile.
Wakati huu kuna umuhimu wa umaakini kwa sehemu ya yale yanayo onekana kama kila mmoja anayejitawala na aliye taja jina la Sayansi ya Kikristo. Maeneo maarufu ya zamani yanatoweka. Yanatoweka kwa haraka. Katika nchi yetu, hali ya siasa imechukua mwelekeo ambao haijawai chukua tena. Tumeendelea na vikundi kadhaa, wanachama wa Republican na Democrats, tumegawanyika kwa vikundi za walio na utambulisho wa kiofisi na wasio. Iwe tutafanya au la. Ilifanyika hivyo tu. Sasa tutafanya nini kuhusu haya? Tatizo na hatari kuhusu haya, ni kwamba unayaona kimakosa. Mmoja atasema chama cha Republican au Democratic kimekaribia kuwa sahihi na kitaenda kwa njia ya zamani. Sasa ni nini unatakiwa kufanya? Kazi yetu inakuja mbele ya uchaguzi, au kujiandikisha na hatuwezi sema kabisa ya kwamba ilikuwa ni ukosefu wa udhihirisho ambao uliwezesha mkatoloki mkali kuchaguliwa na moja ya vyama hizi. Hatuwezi sema kuna ukosefu wa udhihirisho. Najua kitu kimoja, ya kwamba Mungu anatawala ulimwengu, haijalishi vile Republicans au Democrats wanafanya, na sijaona pande zote mbili kufanya yale ambayo yanafanana na Mungu. Sasa yale tunafanya, au hatufanyi, ni udhihirisho wetu wa kibinafsi, sina budi kusema, ya kwamba mkutano uliokuwa Houston unatakiwa kuamsha kila mtu. Hakutakiwi kuwa na shaka ni nini nia ya kanisa la Katoliki la Roma, kupata uongozi rasmi katika nchi yetu, na kutawala kabisa, lakini hatutaishughulikia, kama tutaanza mfumo wa upinzani, kwa sababu njia ya kushughulikia uovu sio kipigana nao, lakini kufanya kujua kwa njia kubwa kutoka kwa msimamo wa mwenye nguvu zote. Msimamo ambapo tunashughulikia uovu, ni msimamo wa Kanuni, msimamo mmoja wa Kimungu.
“Bwana Mungu mwenye nguvu zote anatawala.” {Ufunuo 18:6} “ Mimi ni Mungu aliye karibu…..na sio Mungu aliye mbali?” {Yeremia 23:23} Mimi ni Akili iliyo karibu? Mimi ni Kanuni iliyo karibu? Mimi ni ufahamu ulio karibu? Nguvu iliyo karibu? Sasa swali ni, ufahamu wa Sayansi ya Kikristo kwa upande wa mwanasayansi ya Kikristo ni haya, au ni kuongea tu kuhusu haya? Ni gani? Ni gani Sayansi: kuongea juu ya Upendo, au kuwa Upendo? Kuongea kuhusu mawazo ya Akili, au kuwa mawazo ya Akili, ili kwamba hakuna kitu kingine kinacho endelea ila Akili.
Sasa, haina faida yoyote kusema, ni hali muhimu sana iliyokabili nchi yetu, na kuachia hapo. Ni kama kusema ya kwamba mtu ako na ugonjwa mbaya, na kuachia hapo. Kusema haya ni hali muhimu ambayo ishawai Kabili nchi yetu hata kuzingatia vita vya uasi, na kuachia hapo, ni mbaya zaidi kuliko kitu chochote. Hakuna kitu kinachoweza fanyika ambacho ni tisho, tukijua nchi yetu ni nini, na ni nini inaitawala. Kuna Akili moja, ufahamu mmoja. Ufahamu huu ndio tu kitu kinachoendelea.
Ni yapi unafanya kuhusu haya? Mtu akifikiria ya kwamba mambo haya yote yako chini ya mabadiliko ya ghafla na sheria ya mabadiliko, basi haina haja awe na nchi. Kama anajua ya kwamba nchi yake ni yale anayo fikiria kwa usahihi, yale anayopenda kutoka kwa msimamo wa Upendo, yale ambayo anaheshimu, na kudumisha, na kuunga mkono, kwa sababu ya Kanuni, na ya kwamba serikali kwa kweli ni serikali ya Mungu, au Kristo, na hakuna mwingine, basi anajua kitu; na akiendelea kujua, atakabiliana na shida, atakabiliana na hatari, atashinda tishio lolote, na kuimarisha nguvu za Kimungu kwa niaba ya nchi yake. Atakuwa mzalendo zaidi ya vile angeota kuwa, kwa sababu anafanyisha kazi nguvu za Mungu kudumisha chochote ambacho kinalingana na Kanuni, katika utawala, au katika sheria ya nchi yake, na kabisa kuidumisha, kuiendeleza kwa faida ya wanadamu.
Kila wazo sahihi liko na uwepo wake katika Mungu,na kwa hivyo linadumishwa na Mungu, Kanuni, Upendo na linafanya kazi kwa niaba ya wanadamu na Sayansi ya Kikristo iko hapa kama nguvu hii kubwa.
Ile ambayo milele ni, ile ambayo ina umuhimu, ni kujua Mungu tayari amefanya mambo yote vizuri, na huu ndio msimamo wa Sayansi ya Kikristo. Kisha lazima tujue, kisha tunaweza jua, kisha tunajua, na kujua yale ni, nakujua umilele wa sheria ambayo haya masuala yanaendelezwa, tunasema: Nchi yangu, serikali ya Kanuni ya Kimungu: serikali yangu, serikali ya Mungu, sasa imeimarishwa na sheria yake haijaguzwa na mkusanyiko wa hali au tukio, na nguvu zake, na usalama wake, unadumishwa. Hakuna muungano wa vipengele vya vita , ule ujulikanao kama wa kisiasa au kifedha, unaweza kuiguza. Hakuna muungano wa siasa, au wanasiasa, hakuna kitu kinachoweza kutungwa kwa njia ya athari, kijamii,kidini, kisiasa,kifedha,ambao unaweza guza wazo la Kimungu, na haiwezekani ya kwamba nchi yangu, au serikali ya nchi yangu, kamwe inaweza anguka kwa mikono ya mfumo wa viwango kwani kila mfumo ni kosa, na hatima yake ni kuangamizwa, na kamwe haiwezi pata kuinuka katika nchi yangu, ambayo inatawaliwa na Mungu.
“Ufalme wako umekuja; Daima uko hapa.” {S&A 16:31}