Mungu ni ufahamu wa mtu binafsi
Imeandikwa na BICKNELL YOUNG
Mungu ni ufahamu wa mtu binafsi. Ufahamu wa Mungu ni ufahamu wa mtu binafsi wakati hofu au chuki au upendo wa uovu umeshindwa. Kwa kiwango tunatambua ya kwamba Mungu anafunuka kama tajiriba ya kila siku kwa umbo la milele na aina na kazi, tutafurahia kwa nje maisha yenye baraka tele, afya, uwiano, amani, furaha, mafanikio – bila kuwaza.
Kamwe hauwezi mpata Mungu, kwa sababu ile inayohusika kumtafuta Mungu, ni Mungu, mwenyewe. Natukumbuke bila kujali jina au asili ya madai yote ya kimwili, madai yenyewe kwa wakati wote ni sawa. Kuna madai tu moja ambayo tunatakiwa kuikabili, na hii ni pendekezo la hofu la ubinafsi kando na Mungu. Wakati wowote hisia ya mgawanyiko inajitokeza kwako, kutana nayo haraka kwa ufahamu ya kwamba ni pendekezo, ya kuwa ni imani ya ulimwengu inayowasilishwa kwako kukubaliwa au kukataliwa. Na kwa sababu umepatiwa utawala, na kwa sababu uko na utawala wa Mungu, iko katika uwezo wako kukataza kuingia kwenye mawazo kwa pendekezo lolote kwa ubinafsi kando na Mungu, au hali yoyote ambayo sio sehemu ya uwepo wa kiroho na wa milele wa Mungu.
Lazima tuendelee mbele. Na kuendelea mbele namaanisha haya: Sasa hivi uko katika ufalme wa Mungu kama utakavyo kuwa wakati mwingine wowote. Hakuna kitu ambacho kinaweza ongezwa kwako, na hakuna kitu ambacho kinaweza tolewa kwako. Alafu inaweza onekana ya kwamba yote ambayo ni muhimu kwa kutimiza haya ni utayari wa kupumzika na kukubali, “ Baba, yale yote ambayo yanakujumuisha, pia mimi niko vile.” Hakuna kitu cha kutimiza, hakuna kitu cha kupata, hakuna kitu cha kuwa. “ Yote ambayo yanakujumuisha, mimi pia niko vile.” Na upumzike katika huu Ukweli. Pumzika katika uwepo huu wa kiroho wa Mimi ni. Haya sio magumu sana. Sio magumu hata kidogo. Inaonekana vile mwanzoni. Lakini polepole kama tunavyo chukua mtazamo huu katika maisha, kama tunachukua utambulisho huu, inakuwa ukweli pekee wa uwepo wetu.
Kitu cha muhimu kukumbuka ni kwamba unafunguka kutoka ndani; hautakiwi kushikanisha na tajiriba kutoka nje. Kwa kinyume, kuendelea kwako na ufunguo wa ndani ni wa kukuweka huru kutokana na kushughulika na yale ambayo yanaonekana kama dunia ya nje. Hii haimanishi ya kwamba hatutakuwa na uwiano, amani, furaha, wingi, matunda kwa yale yanayoonekana kama dunia ya nje. Inamaanisha hata hivyo, kama tunajipata tukiishi katika hisia ya uwepo wa ndani, huu ufunguo wa ndani unajitokeza kama uwiano wa dunia ya nje. Yale ambayo tunapata na kugundua katika ufahamu wetu, tunapata kama muonekano wa nje, lakini tunaweka mawazo yetu yote katika kuendelea, ufunuo, na utambuzi wa yale yote yanayojumuisha ufahamu. Alafu, tunapata ufahamu huu ukionekana kwa nje kama uwiano katika ijulikanayo kama shughuli za kibinadamu. Ufahamu wa Kristo ni ufahamu wako. Wakati watu na vitu katika ijulikanayo kama dunia ya nje hazikusumbui tena, hazitufanyi kuwa na chuki, hofu, au upendo, basi tunakaribia hisia ya ulimwengu ya Upendo na Uhai na Ukweli, ambayo hujumuisha ufahamu wa Kristo.
Kwa wakati huu tunashika maada ya kwamba Mungu, ufahamu wa kimungu, ni ufahamu wa kibinafsi, ufahamu wangu na wako, na wake, alafu tunaanza kufahamu maneno ya mshairi: “ Mungu yuko karibu kuliko kupumua, karibu kuliko mikono na nyayo.” {Mwandishi hajulikani} Mungu ni ufahamu wetu na kwa hivyo usaidizi wa karibu. Kwa kweli, ni uwepo wa kimungu wenyewe ndio mimi. Iwe tuwe tumekuwa na ufahamu wake au la, tumekuwa “ufahamu ukifunguka” kutoka mwanzo wa nyakati. Chochote ambacho sisi ni katika itwayo tajiriba ya kibinadamu, sisi ni matokeo ya moja kwa moja ya yale yote tushawai kuwa tangu “ mbele ya Abrahamu.” Ukiamka na utambuzi wako wa kufunuliwa kwa Mungu, kutangaza, kujifunua mwenyewe kama ufahamu wa kibinafsi, unaingizwa katika ufunuo wa juu wa Ukweli na kama Ukweli huu unaingia kwenye ufahamu, utaonekana kama kiwango kikuu cha ufahamu uliofunuliwa. Kwa kweli, ufahamu hauna mwisho, lakini hii haibadilishi ukweli kwamba tunaonyesha umilele ule kwa kiwango pekee ambacho tunaweza tambua na kuiga.
Vivyo ndivyo ilivyo na uponyaji. Uponyaji kwa kweli sio kushinda magonjwa, au kubadilisha hali ya mwili. Uponyaji , badala yake inajumuisha kufungua ufahamu wetu kwa kuingia kwa Ukweli wa kiroho, na kama Ukweli huu unajaa kwenye ufahamu wetu, unajionyesha kama mwili ulio bora zaidi, kama hali iliyo bora, kama afya bora.
Wakati Yesu alituliza mawimbi, maneno yake pekee yalikuwa “….Amani, kuwa mtulivu.” Inakuwa muhimu kwetu kutambua: Amani, kuwa mtulivu” kwa kila mkwazo, kwa kila wazo sumbufu, na kwa hivyo, kwa hali zote za nje za sitofahamu na ukosefu wa uwiano. Wakati Yesu alisema, “Amani, kuwa mtulivu,” hakuwa anaelekeza mawazo yake kwa mawimbi yenye kupiga au kwa Dhoruba. Hakuwa anashughulikia mawazo yaliyo taabika, akili iliyo taabika ya wafuasi wake, ya wale waliokuwa ndani ya mashua. Wala hakuwa anashughulikia kama watu, lakini kwa imani ya kiulimwengu ya wazo sumbufu, kwa imani ya kiulimwengu ya akili kando na Mungu. Kwa imani ya kiulimwengu ya hali zisizokuwa na uwiano za nje na ndani, alikuwa anatangaza: AMANI, KUWA MTULIVU!”
Ni kupitia ufahamu wetu wa Ukweli wa uwepo ambapo tunamilikiwa utawala wetu. Kwa maneno mengine, kupitia ufahamu wetu wa Ukweli wa uwepo, tunaona ya kwamba nguvu sio kitu ambacho kiko “nje” kama mtu, mahali, au kitu au hali, lakini ya kwamba nguvu zote ziko katika ufahamu wetu, katika ufahamu ya yale yanayoonekana kwetu. Usiamini ya kwamba utawala uko katika wanadamu. Usiamini ya kwamba nguvu iko kando na ufahamu na iko mahali “nje.” Kama mtu au hali. Inua wazo juu ya imani kama zile na utambue kuwa Mungu pekee- ufahamu wa kimungu wa milele, ambao ni ufahamu wa kibinafsi – ni mamlaka yote, ni nguvu zote, na kupitia utambuzi huu, uwiano unaonekana. Kumbuka ya kwamba utawala ni wa Mungu, ukifanya kazi kama ufahamu wa kibinafsi. Sio utawala wa mtu binafsi. Ni utawala wa Mungu, ukifanya kazi kama ufahamu wa kibinafsi.
Kwa njia ile ile tuchukulie ya kwamba kuna kiungo cha mwili ambacho kiko na shida, hapa tena tunajigeukia ndani na kujiuliza; “Afya ni kazi, nguvu, katika kiungo chochote au kazi ya mwili? Au mwili kwa kikamilifu ni Athari ya ufahamu? Na si ufahamu ndio unatawala na kuthibiti? Na si ufahamu ni -Mungu? Alafu, si Mungu ako na uthibiti wote juu ya ile inayo onekana kwetu kama mtu, mahali, kitu, kiungo au kazi?” Wakati unatambua Ukweli ule, unahakikisha utawala juu ya utendaji uliogonjeka au ulio na mgongano.
Nguvu zote ziko ndani ya Mungu, ambayo ndiyo ufahamu wa kibinafsi; kwa hivyo, tajiriba yangu, iwe ni tajiriba ya afya yangu, nyumbani, mwandani, biashara, ugavi, yote ni hali yangu ya ufahamu ikifunuka. Kama nimepewa nguvu zote, nguvu zote zinapatikana katika msimamo wa Mungu. Nikikaribisha huu Ukweli katika ufahamu, huu ufahamu unajionyesha kama mtu bora zaidi, mahali, kitu au hali. Hakuna tajiriba ambayo inaweza nijia ila ufunuo wa ufahamu wangu. Wakati nilitambua ya kwamba yote ni Mungu akiibuka na kujitangaza, alafu tajiriba ninayovutia iko katika kiwango cha huu utambuzi. Hakuna haja ya kulaumu watu kwa kosa lolote katika tajiriba yangu; hakuna haja ya kulaumu hali yoyote, au kufikiria ya kwamba ni kitu ambacho sikuwa na uthibiti wake. Lawama ya kweli ni katika mlango wa kutojua huu Ukweli; kwa hivyo hakuna samahani kuendelea mwaka na mwingine kukubalisha utawala wa mtu, mahali au kitu.
Kila kitu ambacho kinafanyika katika tajiriba yetu ni matokeo ya moja kwa moja ya ufahamu wetu. Tunapojisikia “hatuko sawa ama tumepotoka,” hatuleti uwiano kwa mtu yeyote, lakini tukiwa na hisia ya UMOJA, sisi ni sheria ya afya na amani kwa kila mmoja anayekaribia ufahamu wetu. Tujifunze kutolaumu mtu mwingine kwa matatizo yetu. Yale ambayo yanaendelea katika ufahamu lazima yaonekane kwa nje. Yale yanaonekana kama kazi ya ufahamu, huonekana kama uwiano kwa nje. Kazi yetu imefanyika wakati tumepata hali yetu ya UMOJA na Mungu.
Leo ni siku ya UFAHAMU WA UMOJA NA MUNGU, na maisha yetu yote yanaweza anza upya kutoka wakati huu. Natuichukulie siku ya leo kama siku yetu. Umri hauna uhusiano wowote; tajiriba; ukosefu; – haya yote hayana uhusiano wowote nayo. Natuache leo iwe siku ya “Umoja wa ufahamu na Mungu.” Jiulize: “Namjua Mungu kama Ufahamu wa uwepo wa kibinafsi?”
Ni kupitia utambuzi huu wa Mungu kama Ufahamu wa uwepo wa kibinafsi ambao tunaweza waamsha wengine. Hatutakiwi kamwe kujaribu kumshawishi mtu mwingine juu ya Ukweli, kwa sababu hakuna himizo kwa maarifa ya binadamu inaweza kueleza Ukweli. Kanuni yetu ni kwamba Mungu ndiye Akili, nafsi, ufahamu na dutu ya uwepo wa kibinafsi. Huu ni Ukweli wa kiulimwengu, na kama tunaishi katika Ukweli huu, wale wote wanaoingia katika mazingira ya mawazo yetu watavutiwa kwa kiroho nao. Natuache Ukweli uwaguse wote waliotayari kuupokea. Haja yetu ni haya kama Ukweli wa Kiulimwengu na kama tunaukumbatia kama vile uko, wale ambao watakutana nasi wanapona. Alafu, shukrani zetu sio kwa uponyaji, lakini furaha yetu ni juu ya KANUNI inavyoonekana.
Siri yote ya kuishi katika uwiano iko ndani ya utambuzi wa Mungu kama ufahamu wa mtu binafsi. Tutapata “kufika nyumbani” wakati tutatambua asili ya Mungu kama ufahamu wa mtu binafsi. Wakati kwa kweli tunafahamu haya, basi tunaona tunaweza amini kila wazo katika serikali ya ufahamu huu mmoja – tunaweza “ waachilia na kuacha waende” kwa kusema.
Kwa faida ya wale wanaotaka kusaidia wengine, tafadhali jifunze kuwaachilia. Usiwachukue kwa mawazo yako hata kamwe. Lakini geuka na kutambua ya kwamba unafanya kazi na kanuni – Kanuni ambayo itaponya au kuokoa au kugeuza yeyote. Kama utamwachilia yule mtu binafsi kutoka kwa mawazo yako na kutambua kanuni hii, ya kwamba Mungu ndiye Sababu, sheria na athari ya yote mwachilie yule mtu kwa Ukweli.
Sasa, kuhusu kufungua kwa ufahamu kwa wema ambao unaonekana kutakikana: Kama swali ni la ugavi tunageuka mbali na onyesho, lakini tunalichukulia swala la ugavi. Tunawezafikiria Mungu kama ufahamu wa mtu na kwamba, ufahamu ule ndio ugavi. Kama ni swala la ugonjwa tunageuka mbali na mtu au hali na kumgeukia Mungu. Tunatambua ya kwamba Mungu ndio ufahamu wa mtu binafsi, ni dutu ya mwili, ya viungo na kwa hivyo uwiano lazima uwe sheria iliyo karibu kila wakati. Kama ni swala la utengano, tena lazima tugeuke mbali na onyesho na kutambua Mungu kama UMOJA. Uwepo wote ukiwa katika Mungu, tunamaliza imani ile ya utengano.
Kwa hivyo tunaona tunafungua ufahamu katika maelekeo maalum katika kutafakari kwetu, lakini kumbuka hatufundishi mfumo ambao utaleta wema kwa njia ya miujiza kwa mtu binafsi, kando na ulimwengu kwa jumla. Tamanio letu ni katika Kanuni na katika kuonyesha Kanuni ile. Tukubali hii Kanuni, ya kwamba Mungu ni Uhai, Nafsi, Akili, dutu na umbo la kila kiumbe binafsi. Tukubali na kutambua haya – ya kwamba wakati tunasema “Mungu” tunaongea kuhusu ufahamu wa mtu binafsi.
Alafu, huyu Mungu, ufahamu huu, ni sheria kwa mwili, uwiano, afya, utajiri na furaha ya wote. Hii lazima ikubalike kama “Kanuni.” Wakati tunakubali haya kama Kanuni ya kweli, basi tunarudi kwa kanuni ile wakati tunakabiliana na picha au madai yoyote yenye makosa. Ni hapo tunaweza kumbuka hatuna haja na madai. Haja yetu ni katika Kanuni.
Kumbuka ya kwamba wale watu ambao wanauliza usaidizi sio uzingatiaji wetu. Wao ndio ambao watapata faida. Biashara yetu ni, ni kanuni gani inayohusika hapa? Na kama tuko na uhakika wa kutosha ya kuwa kanuni hii ni nini, watapona wale ambao wataikujia.
Matibabu
Wakati kuna imani ya makosa, ni mvuto na sio kitu kingine. Ikatae kutoka kwa msimamo wa ukamilifu. Makataa yetu ni juu ya nguvu zake badala ya uhai wake. Binadamu sio pointi katika ulimwengu; yeye ni ufahamu unaojumuisha – anajua, yeye ndiye “kujua.” Huyu ndiye mwanadamu wa kimungu; pia ni, kadri unavyo husika, Kristo anaye ponya. Katika Sayansi ya Kikristo, Kristo ndiye pekee ambaye ako na kitu kuhusiana na mwanadamu. Ufahamu wetu wa Sayansi ya Kikristo ndio Kristo anayeponya.
Binadamu ndiye ushahidi wa uwepo wa kimungu. Simama hapo! Tusimame katika mlima wa ufunuo! Na tuwe mlima ule. Hali ile ya asili ya uwepo yaja kwa utambuzi. Chukua haki zote na haki za kipekee za Akili ya kimungu. Fikiria kama mwanadamu, alafu utakuwa “mwanadamu.” Huyu ndiye Kristo anayeponya; hili ndilo lengo la “NI MIMI.” …Niko uhai milele…”{Ufunuo 1:18} Simama kama mwangaza wa ulimwemgu! “Shangilia, mwana wa Mungu.” Yale yote yanayohitajika ni mwana wa Mungu, au Sayansi ya Uwepo. Endelea “Kuona” Mwana wa Mungu, sisitiza ya kwamba yupo hapa, haijalishi ushahidi wa hisia.
Matibabu: Jua hakuna magonjwa- huu ugonjwa ujulikanao hauko kwa dutu – hakuna dutu ambayo ugonjwa unaweza onekana au kupatikana.
Akili. Isiyo na mwisho na yenye nguvu zote – daima ipo – ya Kimungu – aliyeko hai kwa nafsi yake – Ufahamu, Ukweli, mwenye maarifa yote, mwenye nguvu zote, mwenye uwepo wote wa uhai, uwepo, Kanuni, Upendo, Sababu pekee – uwepo au utendaji pekee – shughuli zote, muonekano na utekelezaji wa sheria yote; Mungu aliye mmoja na asiye na mwisho – ufahamu pekee.
Jua hakuna dai lolote la uongo ulimwengu wote usio na mwisho. Hakuna ugonjwa na hakuna sababu ya {jina la ugonjwa}, hakuna hisia kwake, hakuna dutu mahali inaonekana au kushahidiwa, hakuna Akili ambayo imetoka kwake, hakuna nguvu, hakuna utendaji, au sheria , hakuna mahali, nafasi au uwepo wake. Hakuna anayeifikiria au aliyeifikiria, hakuna kitu ama mtu kupitia kwake ambao inaweza jionyesha au kuonekana. Hii inayojulikana kama “ugonjwa” ni uongo, au imani ya uongo ili kwamba hakuna ukweli ndani yake kabisa.
Lazima ujue ukamilifu wa Mungu na mwanadamu. Mungu ni nguvu, binadamu ni Ushahidi wa hii wazo la milele ambayo ni moja na Kanuni. Hana magonjwa, hapatikani na yoyote, hawezi jua vile; hakuna uhai anayeweza kupata au kuonekana kuonyesha ugonjwa.
Binadamu yuko salama na sio mgonjwa na ukweli wa kimungu unaonekana kupitia matibabu, na kupitia tiba hii , na ushahidi wake ni kamili na haina lawama. Thibitisha Ukweli, thibitisha ya kwamba Mungu ndiye pekee na makosa sio. Akili ya Kimungu ndiyo pekee na bila shaka mimi na wewe tunajua la kufanya – na tunalifanya. Tangaza ukamilifu wa uwepo – Mungu mkamilifu, mwanadamu mkamilifu, kazi kamili kwa kila jambo.
Jua: Hofu haina athari, hofu haiwezi leta uovu wowote, wala hakuwezi kuwa na adhabu yoyote, imani au dutu, au sheria: na bila uwezekano wa athari au adhabu kwa ijulikanayo kama imani ya ushawishi. Usisite kufunika ardhi ndio uweze kujua hofu iliyozingira haina athari kwa kesi. Haina tofauti yoyote akili ya kimwili ikisema ni watu wangapi wapo, Yale UNAJUA yanatupilia madai ya hofu na iitwayo matokeo yake.
Jua: Hakuna mahali, sheria, ambayo {jina la ugonjwa} milele inaweza kuzwa, au kuanzishwa, au kuwa na mahali au kuendelea. Ni uongo, na matibabu yangu ni sheria ya kutozwa nje na kutengwa kwake. MUNGU PAMOJA NASI – inafanya kazi ya uponyaji. Fanya kazi na ujasiri wote wa Akili. Shighulikia kama Mungu ameshuka kutoka mbinguni na kusema, “Nitaponya kesi hii,” – ukitambua haki zako na kutimiza kazi yako. “ Aliyeshuka ni sawa na aliyepanda…” {Waefeso 4: 10} Yale unajua ni makuu kuliko hofu. Uwepo {Imani} ya hofu kama madai haitupatii sababu yoyote ya ugonjwa. Wala hofu, wala ugonjwa kufanya kurudi hali ya awali. Tazama kwamba Ukweli unamaliza makosa. Kama kuna madai ya chuki, unajua haiwezi fanya kitu kwa mgonjwa. Vunja nguvu zake. Jua haiwezi fanya kitu. Theologia ya zamani haiwezi fanya binadamu kuwa mgonjwa na haiwezi mzuia kupona katika Sayansi ya Kikristo.
Akili ya kimwili haina sheria. Haiwezi sababisha athari yoyote kwa kuwa sio sababu. Hasira au chuki haiwezi mfanya mwanadamu kuwa mgonjwa, kwa kuwa MUNGU ALIMUUMBA VIZURI! Tuko na utawala wa Mungu. Akili ya Kimungu inathibiti hali. Inabadilisha hali. Ni Kristo anayekuja kwa mwili na hivyo anaacha ufahamu huru kuakisi Sayansi. Ukamilifu wa mwanadamu ni usalama wake. Kufanya jambo nzuri kwa njia inayofaa ni Kanuni. Ni ukamilifu. Uko na haki yake. Idai, na ni yako. Iko kwa pande zote, juu, kuzunguka na kila mahali. Weka ulinzi mzuri. Usikiri ya kwamba uko na mengi “ya kufanya” kama vile Wanasayansi ya Kikristo wanapenda kusema, hauna kitu cha kufanya ila Mungu, Na kwa uvumi, na udadisi, jua hakuna kitu kama hicho.Hakuma akili ya kimwili, ila akili ya kimwili hudai iko na uwepo, utu na uvumi. Utawala ndio uhuru mkamilifu wa Akili isiyo na mwisho. Hakuna kitu cha kuzuia utawala wako. Kuna Akili moja tu.
Sheria ni amri ya Akili. “…amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote,” [Wafilipi 4:7} Uhakikisho mtiifu katika ufalme wa Akili. Mungu ni Kanuni, na binadamu huishi Kanuni hii. Utawala wa binadamu ni kumjua Mungu. Kutosheleka, furaha ya uumbaji wa Mungu. Hakuna kitu nje ya Mungu kuleta shida yoyote. Hakuna uwezekano wa uumbaji wake kusumbuliwa na kitu chochote kinyume na asili yake, wala pendekezo la uovu katika uumbaji wa Mungu. Moja katika uwepo. Moja katika sheria, moja katika mpango, moja katika kusudi. Moja katika utendaji, dutu na katika Sayansi. Jua ya kwamba binadamu anafanya kitu kilicho sahihi, kwa wakati wote, na katika hali zote, na yupo katika mahali panapofaa. Athari za uovu ziko na sababu katika imani pekee. Hakuna mawazo yanayoweza kuingia, ama kufanya kitu chochote kilicho na uharibifu. Ufahamu wa Kimungu ni ufahamu wa mwanadamu. Hakuna kitu ila ukweli wa milele Akili kamilifu isiyo na mwisho ambayo inadhihirisha mawazo kamilifu isiyo na mwisho. Kuendelea kwa mwanasayansi ya Kikristo ni furaha isiyo na mwisho – kupaa kunakoendelea kupitia milele yote, kukua katika ufahamu wa Mungu, wema.
Kama Wanasayansi ya Kikristo tujitenge na Mungu na kusimama kama “mnara mrefu” wa Ukweli usiobadilika, ambapo wale wanaohitaji uponyaji na ufahamu wanaweza kuja, lakini hatuwezi shuka au kutingizwa. Katika nakala yetu tunasoma “Hakuna magonjwa.” {S&A 421:18] Na wakati wowote ugonjwa unaonekana, ni hisia za uongo za kimwili. Ile pia ni kweli juu ya dhambi, uovu, huzuni, hitaji, shida, vita na kifo. Hizi zote ziitwazo tajiriba za kibinadamu ni haramu na zisizo za kweli. Hazina sababu za kisayansi za kuwa, na katika mwangaza wa wazo safi ambayo hushikamana na ufunuo, hakuna kanuni au ukweli ndani yake au juu yake na hakuna sheria ambayo zinaweza kuonekana kufanya kazi, kuendelea au kuishi. Ni muhimu kudumisha ufahamu wa uwepo wa kweli na sheria yake;- kwa kufanya hivyo, picha ya uongo ya binadamu kuvutwa na dhambi, au kuathirika na magonjwa, inashindwa. Nakala yetu pia inasema, “Ni undanganyifu wa kiakili kufanya magonjwa kuwa ya kweli – kuifanya kitu kinacho onekana na kuhisiwa – na kujaribu tiba yake kupitia Akili.” {S&A 395: 21 -23}
Kwa njia ile ile kuona mwanamume, mwanamke, mtoto, mtu yeyote au kitu chochote kama mgonjwa akihitaji uponyaji pia ni “undanganyifu wa kiakili.” Kama tunavyoelewa ya kwamba ile inayoonekana kama mwanadamu ni Mwana wa Mungu, wa kimungu katika uwepo, na wa kimungu katika sifa zake zote, kwa hivyo lazima tuone chochote kinachoonekana kuwa mgonjwa au ugonjwa ni uongo ambao unaficha ukweli wa kimungu – ukweli ukiwa mwili wa kimungu, utambulisho wa mwanadamu wa kweli.