Nafsi moja
Iliyoandikwa na BICKNEL YOUNG
Kwa mtazamo wa ukweli ya kwamba kitabu chetu cha maandiko kinatangaza kwa usafi ya kwamba kuna Nafsi moja, hakutakiwi kuwa na shaka juu ya haya. Nafsi moja. Hakuna nafsi katika mwanadamu yeyote au katika mnyama yeyote. Usiogope kuona hivyo. Na ninasema kwenu, kila mtu anatakiwa kuondoa hii dhana ya zamani ya kwamba uko na nafsi ndani ya mwili wako ambayo inaweza toroka. Hakuna kitu cha aina ile kinachoendelea. Kuna nafsi moja tu – Mungu. Hio ndio Nafsi tu mtu yeyote ako nayo.
Nafsi ndio thamani, kudumu, ipo kila wakati, iko mzima kila wakati, iko hai kila wakati, iko na ushirikisho kila wakati kiini cha uumbaji wote, kiini chako, kiini cha yale yote uko nayo. Nafsi inaashiria kitu kingine, Kama inavyotumika kibinadamu, jina Nafsi iko na maana zaidi kidogo juu ya jina Roho. Kila kitu ambacho ni kizuri kinasemekana kimetengenezwa na Nafsi. Ni, ukipenda, ile uwezo maalum wa milele kujieleza kwa uzuri wa milele katika uumbaji wote. Kila kitu ambacho ni kizuri ambacho tunajua jambo lolote kukihusu,kiko na asili yake katika Nafsi, Akili ya Kimungu. Hio ndio sababu ya kwamba ndio tuweze kuonyesha uzuri, mtu lazima awe kitu kando ya mtu mwenye maarifa. Kuna maelfu ya watu ambao hawawezi kuonyesha kitu chochote kwa asili ya uzuri, kwa sababu hawana Nafsi. Oh ndio, wako na Nafsi bila shaka, lakini hawajaamka kwenye Nafsi. Watu wengine huionyesha kwa urahisi mkubwa kwa njia moja na wanaikosa kwa njia zingine zote.
Wengine wanaweza imba, wengine wanaweza chora. Ikionyeshwa kwa njia moja, tunaiita asili ya usanii. Lakini haitakiwi kuwa ya upande mmoja. Kuelewa Nafsi bora zaidi, hatupotezi kitu chochote ambacho ni halali au sahihi kwa njia ya kuonyesha lakini tunakuwa na ufanisi zaidi na zaidi na usaidizi zaidi kwa dunia. Wakati mmoja nilikuwa muimbaji mtaalamu na nilikuwa kiongozi mwimbaji katika kanisa la kwanza Chicago wakati ibada zilikuwa zinafanywa katika ukumbi wa micheza wa zamani. Nilipata kwamba kuchagua nyimbo zangu na kuzitafsiri ndio kufurahisha wote ilikuwa kazi ya kukera na ngumu. Alafu siku moja, nilipokuwa nikiingia kwenye ukumbi, iliniijia ya kwamba kama kuna kitu cha ukweli kuhusu uimbaji, basi kila mtu alikuwa anaimba. Hii ililainisha kila kitu, kwa sababu tulikuwa tunaimba sisi wote pamoja. Hio ndio asili ya Mungu.
Uzuri hauwezi tekelezwa na imani yeyote, kwa sababu ina uwepo wake katika Mungu. Yote ni sawa, milele, moja na umilele wake na ukamilifu. Haiwezi athirika au kudhoofika kwa njia yoyote, kwa sababu hakuna nguvu nyingine au uwepo. Hakuna njia yoyote inayowezekana ambayo inawezajeruhiwa, kwa sababu hakuna kitu cha kuwaza juu ya jeraha. Uzuri na utukufu wake wa ukamilifu, unawazwa na Mungu pekee kama mawazo ya Mungu. Uzuri, bila kujali kutafuta kwa kimwili, ni wa kiroho. Kama Ukweli, ni wa milele. Kwa hivyo usimkashifu mtu yeyote kwa kujaribu kuwa mzuri!
Tutakuwa wazuri mbinguni, unaweza kuwa na uhakika!
Njia ya Sayansi ni njia ya elimu sahihi, na inatupilia imani ya zamani kwamba kuna Nafsi katika mwili ambayo lazima itoroke. Inaonyesha kwamba Mungu ni Nafsi, na umilele hauwezi ingia ndani ya kitu chochote. Uzuri wote upo kama ubora wa Mungu, Nafsi. Sio ya kimwili. Tunasema, “Haweki Nafsi yoyote katika uimbaji wake, au kuchora, au kuandika.” Alafu tunasema haina nafsi. Na hio ni sahihi. Nafsi ndio chanzo cha yote tunayojua kuhusu uzuri, ukuu, yote ambayo inafanya maisha kuwa ya kustahimili.
Katika kazi ya kuponya, Nafsi ni muhimu kama Akili. Inatuinua kutoka kwa mashimo ya kurudia maneno, na inatuonyesha kwamba hamasa ni zaidi ya mbinu. Na sisi wote tuangalie vizuri tuwezavyo! Ni halali kabisa kwa mtu yeyote kujaribu kuwa mzuri. Hatuwezi fika mbinguni bila uzuri! Ufalme wa Mbinguni ni ufalme wa uzuri.
Nafsi ndio mfano wa kujua, na inaashiria furaha, umoja, amani, na kadhalika, na wakati mtu anadhihirisha Nafsi, uzuri wa Nafsi utaonekana kwa mazingira yake. Nafsi ndio kiini cha uzuri wote, kanuni na shughuli na sheria ya yote ambayo
ni nzuri na yenye uwiano. Tunaweza shirikisha kimwili na uzuri, lakini uzuri ni wa milele, inainua, ni kuu na tukufu. Kwa hivyo hatuhitaji kufikiria kwamba tunaweza puuza uzuri wa ijulikanayo kama dunia ya kiasili. Umilele wa uzuri utaonekana kwa kipimo ambacho tutaacha kushirikisha kimwili na utu na uzuri.
Kama mtu ameondoa uoga wake na hisia zake za kibinadamu zinakombolewa kupitia Nafsi, atakuwa mwenye hisia za kuelewa na kuwa na maono safi ambayo yatakuwa ya kutosha kuponya kesi haraka – mahali ubora uliopungukiwa kiupendo na uliopungukiwa kwa uzuri ungeshindwa kuona yale mema na ya kweli. Mara nyingine watu wenye “hisia” Wako zaidi kisayansi kuliko waliotulia. Hisia za kibinadamu kwa jumla sio za kutengwa. Kama unaendelea kwenye Sayansi ya Nafsi, utaona uzuri mahali ambapo hukuona mbeleni.