Neno mtu
Iliyoandikwa na Bicknell Young
Matibabu ya Sayansi ya Kikristo sio mimi nikifikiria juu yako, au kwa niamba yako – au kukuponya kutokana na kitu. Ni Ukweli wa kile ulicho kwa kweli SASA na milele, na huu ukweli unasafisha pendekezo ambayo inadai kuwa wewe na inaisafisha milele.
Neno “mtu” linajumuisha wote waitwao “wanadamu,” mtu inamaanisha watu wote na kila kiumbe binafsi. Mungu ni Uhai – Ukweli – Akili – Upendo; Mtu anaishi ndani na kama Uhai, wenyewe; Upendo, wenyewe; Ukweli, wenyewe; na Akili, yenyewe.
Mtu ni dhihirisho la uwepo, na imisho na utendaji – ikijumuisha wote – mtu hataki kitu cha kurembesha, kutukuza, au kusafisha uhai wake. Kuwepo kwa pamoja na Mungu, yeye ni uwepo wa maisha ya milele na kiini kisichoweza kuharibiwa. Akiishi kama dhihirisho la uwepo na imisho la Baba, binadamu ni hali ya umiliki ulio kamilika wa Akili isiyo na mwisho ikijumuisha ndani yake mawazo yote.
Sifa za binadamu ni Upendo, uwiano, utawala, mafanikio, ufahamu wazi, na utendaji sahihi uliokamilika kwa kila akifikiriacho au akitendacho. Mwanadamu na shughuli zake ni uwepo na imisho kamili na ya kawaida ya Kanuni isiyo na mwisho – isiyoweza hata kwa tofauti kidogo kutoka kwa ukamilifu kamili. Binadamu akiwa uwepo na imisho la Akili isiyo na mwisho, mwanadamu ndani yake ako na yale yote ambayo yanasababisha ukamilifu na uwepo wa umoja – hatamani – ako na umiliki.