Siku
Kutoka Kwa Maandiko Yaliyokusanywa Iliyoandikwa Na Bicknell Young, Ukurasa Wa 79
Ukiamka asubuhi ,tambua na urudie kwa ufahamu mara moja, ” Kuna Akili moja tu.” Na wakati huo, kabla ya mvuto wa siku umechukuliwa, imarisha ukweli juu ya siku. {tazama kamusi} Jua kuwa imani ya wakati haina utawala juu yako na juu ya wengine; uko na utawala juu yake. Imarisha siku zako katika ufahamu na ufumbuzi. Siku haina utaratibu. Ukiamka jua uko na wakati na nafasi kufanya yale yote unahitaji kufanya leo. Tangaza, ya kwamba kuna Akili moja, ya kwamba mambo yote yashafanyika ndani ya Mungu na hauna la kufanya ila uwe kwa ufahamu safi, ili kwamba Mungu aweze kufichuka. Ukishikilia haya, utakuwa na wakati mwingi na nafasi nyingi za kufanya yale yote unayohitaji kufanya. Jua asubuhi , siku ni ufunguo wa mpango wake, mhamazisho, ambayo haijui kuanza wala kumaliza. Matukio yote ya Mungu yashapangwa.
Ni nini unatakiwa kufanya leo? Uko na jambo moja la kufanya na hilo ni kujua Ukweli. Ukipatana na kazi ya masaa kumi na sita, jua Ukweli kama jambo la kwanza. Usianze na imani ya kuwa uko na mambo fulani ya kufanya. Ukianza vile, umevutika tayari. Lazima ujue haya kabla ya kuanza ama utakua umeshachelewa. Kufichuka kwa Kimungu hakuanzi kamwe, haina mwisho na haikatishwi kwa muda wowote, na unapotangaza ufumbuzi huu wa milele wa mpango wa siku wa Mungu, na kusudi, hii ni uponyaji kwa leo.
Upendo usio na mwisho haujui kikomo, haiwezi kuzuiliwa kwa mafanikio, na sheria zake hasiwezi kubadilishwa na hasiwezi kuingiliwa. Siku hii haianzi wala kuisha; haikupeleki wewe au mimi au mtu yeyote karibu na kaburi, kwa imani wala kabisa. Siku hii inachukua wewe na uumbaji wote karibu na maisha ya milele. Siku hii ni kitendo cha aliye na ujasiri wote. Siku hii ina agizo la Kimungu, na yaja kisayansi. Mahitaji ya siku hii yameimarishwa, na hayahitaji wakati. Siku hii ni roho, sio mwili, na usiache mambo ya kimwili yaseme, ” Mimi ni” kwa tukio lolote la uumbaji. Siku hii ni ufumbuo na udhibitisho wa maisha bila mwisho. Haina usiku, ni mwangaza wa milele, mionzi ya Roho, Mungu.
Hakuna shida ambayo inaweza ingia siku ya Mungu. Akili haihusiki na matatizo. Akili inafumbua mawazo yake bila kikomo. Iko na mchanganyiko wote, ubunifu na wingi. Haina mwisho na dhihirisho zake ni kamili, ni nzima na zimeridhika, kwa kuwa binadamu ni hali ya kukamilika kwa Mungu na kuridhika kwa ukuu.
Afya inamaanisha ukamilifu. Mtu hahitajiki kuonekana kama kitu kingine ila ukamilifu. Maana asili ya afya ni hiyo tu, kuwa umekamilika tu. Hakuna chochote kinachohitajika ,kinachokosekana, na lazima tuwe na afya. Ni asili ya Kimungu. Kila mtu lazima awe nayo kwa kuidai. Inawezapatikana kwa Sayansi ya Kikristo, kwa sababu Sayansi ya Kikristo inafunua sheria na sayansi ya uhai katika Kristo. Inatakiwa kua, na inaweza kua imedhibitishwa. Unaweza idhibitisha. Jaribu kuifanya na saidia wengine kuifanya siku hii. Kazi hii ya kila siku itafanya mengi ambayo hauwezi dhamini mara moja. Ufahamu wa kweli wa siku unainua mzigo wa imani ya kimwili na inatumika kufukuza kuchangnyikiwa kwa sasa kwa akili za kimwili Pamoja na kukulinda kutoka kwa madai yake.