Tukisema, “Nataka”
iliyoandikwa na BICKNELL YOUNG
Agosti 17, 1935
Tukisema, ” Nataka,” tunazuia “Ni mimi.” Mimi pekee haiwezi taka. Mwanadamu ni hali ya umiliki, sio ya kutamani. Tunapoweka kando ” Nataka,” basi “Ni Mimi” yupo. Kama kuna kitu chochote unataka, fikiri kwanza; hio ndio sababu hauna.
Ukiona kila kitu na kila mtu anatawaliwa na Mungu, hio ndio safina, na kuna usalama. Ukitafuta udhihirisho, wewe ni utengano. Mwanasayansi wa Kikristo ni wa dhamani kama tu anafanya tathmini.
Petero alikuwa sawa na akidhihirisha mpaka wakati hofu ilimjia, alafu akazama. Hatutafuti maisha; kuishi ni uwepo, na uwepo ni Mungu, na Mungu ni kuishi.
Wakati unashughulikia hofu, ishughulikie; usiwe hofu. Usiweke hofu yako kwa tiba ya hofu. Roho ndio kitu dhahiri; Udhahiri ni dutu, na dutu ni Roho.
Mtu akasema, “Inaonekana kwangu, madai kila wakati ni, hatuwezi ona Roho.” Jibu ilikuwa, “Mpendwa, hauwezi ona kitu kingine chochote, Ila Roho; Itakuwa vigumu, hata ukijaribu.”