Hungekuwa na hofu juu ya kitu chochote
Kutoka kwa Hotuba na makala ya EDWARD KIMBALL
Hisia yetu juu ya Kristo Yesu na kazi yake ni kwamba hakuja kuangusha au kubadili kitu kuu ambayo ilikuwa na haki ya kuwa. Sio kabisa. Alikuja kumbomoa ile ambayo haikuwa na haki ya kuishi. Kwa kweli sio mantiki kudhani ya kwamba kuja kwa Kristo kutenda mapenzi ya Mungu kungekatisha kitu chochote ambacho Mungu aliteua; ya kwamba angezima kitu ambacho kina msingi wake katika maisha ya milele na ilikuwa na uhai wa milele. Hio kwa uhakika haingekuwa mantiki au ya busara; mafundisho yetu ni kwamba kazi yake inatakiwa kudhibitisha kwa wanadamu na kuvuta umaakini kwa ukweli kwamba magonjwa na dhambi na wazimu na hofu na hizi vitu zote zikiwa famiia moja ambazo zinasumbua wanadamu zote sio halali, sio kawaida, hazina haki, hazina sheria na sio muhimu. Kazi ya Kristo ni dhibitisho kwa kadirio letu la asili ya uharibifu ya aina tofauti za uovu zinazosumbua wanadamu.
Wakati Kristo yesu alimaliza kazi yake alifanya tangazo la ajabu. Ilikuwa hii: “Kuweni na furaha, nimeshinda ulimwengu.” “Nendeni namfanye vivyo hivyo.” Tambua adhimisho ya tangazo lile. Hakuwa amefanya kitu cha ajabu, kitu ambacho kilikuwa cha dhamani kwa kikundi kidogo tu cha watu, ilikuwa ni huduma kwa binadamu kwa wakati wote, kama dhibitisho la asili isiyo na mwisho ya kusudi la Kimungu. “Nendeni na mfanye vivyo hivyo.” “Mambo haya mtayafanya na mengine makuu.” “Mimi ndimi njia.” “Nifuateni” “Mtaujua ukweli na ukweli utawaweka huru.” Huru kutokana na nini? Kufuata njia yake, kufanya alivyofanya, – yote inamaanisha nini? Kwa nini, inatakiwa kumaanisha uko na haki ya kusoma njia yako, kugundua njia yako, kutenda njia ambayo itakukomboa kutokana na mifumo ile ile ya uovu; na hii ndio moja ya pointi ya kimsingi ya mafundisho ya Sayansi ya Kikristo. Mungu alimpa mwanadamu utawala juu ya dunia yote; hiyo kwa kweli inamaanisha utawala juu ya mwili wake, hali yake, mazingira yake, na hali zilizo mzingira. Inamaanisha utawala juu ya kila adui, juu ya kila kikwazo, juu ya kila kitu kinachojiinua dhidi ya maisha yake.Shida tulionayo ni kwamba tuna hofu na kila mtu na kila kitu kwa sababu hatujui, kamwe hatukujua , ya kwamba kwa msingi Mungu alitupatia utawala. Hungekuwa na hofu juu ya kitu chochote ungelijua uko na utawala juu yake; na kila mtu anayesoma Bibilia ako na fursa ya kupata kwa kurasa zake za kwanza ya kwamba hio ndio Mungu ametupatia, na sisi wote tumeikosa mpaka siku ya leo.
Tumekuwa, kama ilivyo, kama povu juu ya bahari ya hatima ya bahati mbaya, na tayari kuamini ya kwamba hali ovu ya uhai inaweza tushinda, na kuondoa uhai, na kutufanya wagonjwa, na kutuua wakati wowote. Tunaelimishwa kupatanishwa na hatima yetu mbaya, laana yetu na hakuna mtu aliye elimishwa kufikiri ya kwamba ako na haki ya kukataa, au kwa kikamilifu kupigana na adui yake.
Katika hatua hii Sayansi ya Kikristo inasisimua tumaini ya kwamba uko na haki kupigana na kushinda. Uko na haki ya kuwa bwana wa hatima yako. Uko na haki ya kufanikiwa katika kila kitu ambacho ni sahihi kwako kufanya. Uko na haki ya kujifunza kuzuia magonjwa;Uko na haki ya kujifunza kutibu umasikini; na mvutano muovu wa wanadamu dhidi yao wenyewe. Sisi leo hatuna mwelekeo, kulingana na kukiri kwetu; Ilhali milele kuna mlio katika masikio ya Ukristo jambo hili moja, katika Kristo na mafundisho yake na njia yake na utawala wake tuko na haki ya wokovu, na itatufanya huru.