Mazungumzo juu ya ugavi
Na EDWARD KIMBALL
Nahisi kwamba, ingawa haufuati pesa kwa maana ya kawaida ya neno, kuna sababu ya kutosha kujua ya kwamba uko na haki ya kupata ugavi wa kutosha. Kila kitu kinachohusika na ambacho watu wanaita ugavi,ni kitu cha mawazo. Yale tunatakiwa kufanya, ni kufikia kwenye mawazo yasiyo na kikomo, kwa mtazamo huu. Kibinadamu, itakuwa asili kufikiria vile, ilhali ukiwa katika utendaji wa Sayansi ya Kikristo, ugavi wako utakuja kupitia utendaji; lakini ona vile ni wazo lililo na kikomo! Kama ilivyo ugavi ni wa milele, na kwa kweli ni dhihirisho la milele, ni huzuni aje wazo ambalo hupuuza milele na kuweka kikomo kwa ugavi na kuuweka kwa mkondo mwembamba.
Kwa upande mwingine, fikiria hivi: Ugavi uko kila mahali na hauna kikomo, na uko mahali upo kila wakati, na kile unachokitaka. Utajionyesha kwa mamilioni ya njia. Kwa hivyo, fungua njia zote na uwache uingie ndani. Jiweke katika hali ya kutoshangaa. Pata mtazamo wa akili ambao hakuna kitu kwa njia ya ugavi kitakushangaza, hata ukipata vipande vya fedha katika mdomo wa samaki. Wewe sio mwadhiriwa wa hali yoyote; wewe ni mtoto wa Mungu. Uko na ugavi usio na kikomo, Jifahamishe na ukubwa wa mawazo yako yakidhihirisha umilele wa uwepo. Hakuna hisia ya mwanamume au mwanamke, au imani yoyote ya tukio, au janga lisilo eleweka, au imani ingine yoyote, inaweza kukutenga na uponyaji wako, ambao ni uwepo na nguvu za Mungu aliye pekee.
Milele imekamilika kabisa. Uhai umeimarishwa, na sheria yote na nguvu zimeimarishwa. Ukweli, au Akili ya Kimungu, inajumuisha ukamilifu. Uwezekano wote wa uwepo ni wako; na hakutakuwa na mwingine kamwe. Hauhitaji kungojea ukombozi; leo ni wako. Unaweza onyesha utawala kama unangoja. Tangaza kila kitu kizuri kwako. Tarajia kila kitu kizuri sasa.