Mungu na Mwanadamu |

Mungu na Mwanadamu

Kutoka Kwa Mafunzo na hotuba kuhusu Sayansi ya Kikristo

iliyoandikwa na Edward Kimball

Hotuba fupi iliyotolewa mwakani 1900


Mungu kwa kikamilifu ni mambo na vitu zote, sasa, na Mungu ni mwema; kwa hvyo ni ukweli usiyopingika na usiyobadilika kabisa ya kwamba hakuna kitu kingine ulimwenguni ila Mungu na athari yake kamilifu.

Huyu Mungu ni Akili, milele akiwa na ufahamu wa nafsi yake mwenyewe, kamwe hajawai na hatawai kuwa na ufahamu wa kitu kingine chochote. Akili ni moja milele,na hii Moja inajumuisha wote.

Inajumuisha wote ambao kwa uwezekano wowote wanaweza hitajika kwa Akili kamilifu.

Akili inajitawala. Inafahamu sasa na hata milele juu ya uhimili wa Kimungu, Upendo. Inahamasishwa na, kujazwa nguvu na, kukumbushwa na, na milele kusonga kulingana na hii moja na ya kipekee , uhimili, Upendo.

Kwa sababu hii,Akili – Akili pekee – ni tulivu, inaaminika,ni pole, na ni jasiri milele; kwa sababu kwa urahisi inashuhudia nguvu za maumbile yake, Upendo. Kwa hivyo hakuna uwezekano au nafasi katika ufalme usiokuwa na upungufu ambao ni wa Akili wa kupata hofu. Hakuna kitu katika Upendo cha kuleta hofu, hakuna katika Akili cha kuifahamu, hakuna katika wema cha kuidumisha, hakuna nafasi katika ulimwengu wa Upendo kwa kitu kama hicho.

Akili – kamilifu, kujifahamu – kujijua kama Moja, na ikijitawala milele, inaunda msingi wa maumbile yake kamilifu,Upendo na ni uhai wa milele. Hii inamaanisha – kwa ajili kila kitu ambacho Akili inashikilia katika ufahamu ni dhahiri – dhihirisho – lake. Na yenyewe ni dutu, Akili kwa urahisi inagundua ya kwamba inashuhudia uhai wa milele.

Wazo zote katika ulimwengu, papa hapa ni kauli ya Akili hii Moja; kwa hivyo zinawekwa, kuhifadhiwa ,kukuzwa, kutawaliwa na kuelekezwa na yenyewe, Wema.

Mawazo haya huunda Neno la Mungu, ambalo – kulingana na agano lake – itatimiza yale ambayo wametumwa.

Akili hii, ikijaza anga yote, haiachi nafasi kwa akili nyingine yoyote; ikiwa na yote ambayo kwa uwezekano wowote itahitajika kwa uhai, kitendo au nguvu, haiachi kipande kingine chochote cha kuunda akili nyingine; na kuwa na ufahamu wa kutenda kama sababu isiyo na mwisho, haiachi chanzo au kipemgele ya sababu kwa akili nyingine yoyote.

Hii Akili yenye ufahamu, ikiwa na ufahamu wa ukamilifu, ya kuridhika, ya kujua kwa milele, inaifanya kutowezekana kabisa ya kwamba kunaweza kuwa , kushawai kuwa au kutawai kuwa , akili nyingine.

Akili hii moja, ikijumuisha wote na kuwa wote, haiwezi jua, kutana au kuwa na upinzani. Hakuna kitu cha kupinga, kupinga kwa, kupingia, hakuna mbinu ya utaratibu ,hakuna kiunganishi, na hakuna lengo, hatua, au nguvu ya kitu chochote kama kile, kwa sababu Mungu ni yote na hawezijipinga mwenyewe.

Akiwa Yote, Mungu anaufahamu kamili wa mamlaka yake ya Kimungu, kwa urahisi anajua ukamilifu wa serikali yake, anatambua udhibiti wake usio na mwisho, ako na ushahidi – uthibitisho – wa utawala wake usio na upinzani.

Ako na ufahamu wa kufanya chochote anataka, na mapenzi yake ni mema. Akili, kwa hivyo ni serikali yote, sheria na utendaji wa sheria ambao upo, na hii sheria haipingiki, haina mipaka kwa upeo na nguvu.

Mwanadamu milele amezingirwa ndani ya ufahamu kamilifu wa wema. Hawezi kukwepa, hata kidogo, kutoka kwa ulinzi, upendo, anaehamasisha, anaedumisha, aonae kote, anaedhibiti usafi wa Upendo.

Hana shaka, hana jukumu, hakuna kitu cha kupanga, kukamilisha, kupata, kutamani, kwa sababu kwa urahisi ako na mambo yote mazuri.

Hakuna mustakabali katika sasa ya milele kwa Akili isiyo na mwisho. Kwa hivyo hakuna mustakabali wa kujua Ukweli au kumjua Mungu au kufikia ukamilifu na hakuna kudhihirisha, kwa sababu dhihirisho pekee la kufanya, daima imekuwa ifanywe, au daima itakuwa , ni ya Mungu, na hiyo inafanywa sasa, na binadamu ni ufahamu wa ukweli huu. Kwa urahisi anajua, bila tashwishi yoyote, ukweli wa milele wa uwepo katika Wema.

Yeye binadamu, ana ufahamu wa kiroho, uthibitisho kamili wa wema, anamjua Mungu kuwa mmoja katika serikali, mmoja katika nguvu, mmoja katika utendaji, mmoja katika uwepo wa milele, ufahamu moja, mmoja kweli, hali halisi ya uwepo. Kile alicho daima, ni ufahamu wa Wema, utambuzi wa kiroho wa Ukweli, ufahamu wa Akili moja. Yeye ni hali moja ya usafi, asili, ufahamu usiyo na wingu, ukitenda, ukisonga, ukiwa na uwepo uliokamilika katika Upendo wa Mungu usiobadilika.

Hawezi anguka kutoka kwa hali yake ya mamlaka. Utawala wake hauwezi ondolewa. Hawezi poteza ufahamu alioupata kutoka kwa Mungu. Hawezi potoshwa, kuongozwa vibaya, kudanganywa, kwani anachokijua ni Akili, Mungu.