Bonde litajaa maji
Iliyoandikwa na Gilbert Carpenter
Mama Eddy aliniambia juu ya dhihirisho wakati kanisa la kwanza lilipokua linawekwa paa. Haikunyesha kwa mda wa siku kama sitini. Hatimaye mlezi wa maziwa akaacha ujumbe hapo Pleasant View ya kwamba hataweza kuleta maziwa ingine kwa sababu hakukuwa na maji ya kutosha katika kisima chake ambacho alikitumia kuwapa mifugo wake kwa sababu ilikuwa inakauka. Keshoye hata hivyo kama kawaida alikuja na maziwa akisema kulikuwa na futi mbili ama tatu za maji katika kisima chake licha ya kuwa hakukuwa kumenyesha. Aliwauliza wanafunzi ambao alikutana nao kama walikuwa wachawi au manabii.
Baada ya kusema dhihirisho hii Mama Eddy alisema, ” Si Mungu ni mwema? Oh Bwana Carpenter, amini Mungu huyu mpendwa na mwema.”
Katika Wafalme wa pili 3:17 tunasoma, “Kwa maana anasema Bwana, hautaona upepo, wala hautaona mvua; ila ile bonde itajaa maji, ili muweze kunywa , nyinyi na mifugo wenyu na wanyama wenyu.” Inaonekana dhihirisho la Mama Eddy kwa tukio hili ilikuwa ni timizo la leo la unabii wa maandiko ya Bibilia.