Ibada ya Jumapili
Iliyoandikwa na GILBERT CARPENTER
Mtu hupati kipengele cha furaha kikikosekana katika thiologia ya zamani; hii inaifanya kuwa muhimu kwa wahusika wake kuijia dini kutoka kwa hisia ya jukumu badala ya matamanio. Alafu ili kulazimisha hili jukumu kwa ,binadamu, theologia ya zamani imebidi kuunda adhabu kwa kushindwa kuifuata. Haiwezekani kudumisha njia hii ya kumsukuma binadamu kumuabudu Mungu, kama theologia ya zamani haikufundisha hofu ya adhabu kama kiboko kumlazimisha kuunda inayochukuliwa kama jitihada sahihi kupata wokovu na mbinguni. Hivyo theologia ya zamani imewezesha dhana kwamba kanisa ni shule ya Mungu kwa watoto watukutu na kwa vile wengi ni watukutu chini ya kanuni hii, sio ajabu kuna furaha kidogo sana,Ni furaha kiasi gani ambayo unaweza pata darasani pahali wengi wa watoto wanatambua upungufu wao na walikuwa wanangonja adhabu inayohakikishwa?
Sayansi ya Kikristo imeondoa mafundisho haya ya kidini ya zamani ya moto wa kuzimu na laana kwa kufanya utafutaji wa mbinguni wa binadamu ujae furaha, ya kwamba hakuna haja ya kutumia hofu ya adhabu ili kumuinua. Katika kumuadhibu mtoto inatosha kumnyima ruhusa ya kuenda mahali, kama mahali pale ni pazuri bila adhabu ingine.
Ibada ya Sayansi ya Kikristo inaweza tafsiriwa kama uwanja wa ndege ambao mshiriki wa kanisa huja kwa kusudi la kufanya safari ya ndege ya kiroho. Hakuna mshiriki anayetakiwa kutosheka kwa kubaki katika uwanja huu wa ndege, wakati anapatiwa kila nafasi ya kuchukua safari ya kiroho ambayo inachangia sehemu muhimu katika ukombozi wa binadamu. Roho yote ya uwanja wa ndege ni safari na hatakiwi kuendelea katika hali ya kutoendelea au ukosefu wa utendaji unaojipenda na kujihisi ametosheka. Katika ibada kutapatikana maagizo muhimu ya safari hii ya kiroho, ikionyesha mizigo ambayo lazima iachwe nyuma, na vifaa ambavyo ni muhimu, na kadhalika.
Mafundisho ya dini ya zamani inatazamia ibada ya jumapili kama kazi muhimu na mahali panapo stahili pa mapumziko pa mawazo, ambapo wajibu mkuu wa mwanadamu ni kuja kusikiliza. Katika Sayansi ya Kikristo ibada ya kanisa ni mahali mwanadamu huja kuanzisha mawazo yake na kuingia kwenye utendaji wa kiroho,ambayo inatakiwa kuendelea wiki yote, ikionyesha ibada kuwa chanzo cha hekima. Ibada inaweza chambuliwa kama ikiwa na majukumu dhahiri saba, ikiambatana na siku saba za uumbaji ikifikia kilele cha siku ya mapumziko ambayo wakati “ Mungu aliona kila kitu alichoumba na tazama ilikuwa mzuri sana.”
-
MUZIKI. Jukumu la kwanza katika ibada yetu ya jumapili huja kupitia nyimbo za kuabudu na muziki ni wito wa furaha ambao inapakikana kufungua akili ya washirika kwa tumaini la kiroho. Ni agizo la “kupiga kelele ya furaha kwa Bwana.” Inashikamana na siku ya kwanza ya uumbaji wakati Mungu alisema, “ Na kuwe na mwangaza; na kukawa na mwangaza.” Kama mtu angekuwa kwa giza la hofu na mtu akaleta mwangaza ambao ulionyesha ya kwamba kwa kweli alikuwa katika nyumba ya baba yake ambapo hakuwa na kitu cha kuhofia, si hiyo inaweza leta furaha?
-
CHAGUO LA SOMO LA BIBILIA. Ikiwa msingi wa jengo letu la ibada ni furaha, Bibilia ndio jiwe la msingi. Ni la muhimu ya kwamba ufunuo wa Mama Eddy ushikanishwe na Bibilia na kuonyeshwa hauwezi tenganishwa nayo. Ikiwa mtu anataka kujenga nyumba ambayo itasimama ataijenga juu ya mwamba, kulingana na mafundisho ya Yesu.
Ukweli wa kiroho wa agano jipya ambayo Yesu, Kristo, alikuwa mfunuaji na mtafsiri, ni mwamba ambao Mama Eddy alianzisha Sayansi ya Kikristo. Kwa hivyo tunaweza unganisha Sayansi ya Kikristo na Bibilia na kuweka katika akili ya dunia yote umoja huu, alafu Sayansi ya Kikristo itaimarishwa kwenye ukweli wa milele ambao hakuna mafuriko ambayo inaweza fagia kamwe.
Siku ya pili ya uumbaji inaleta anga, amabayo Mama Eddy anafafanua kama ufahamu wa kiroho. Wakati fedha inapochimbwa hupatikana na shaba na lazima hizi mbili zitenganishwe kabla yoyote ile iwe na thamani yoyote. Kwa hivyo Bibilia ina ufahamu wa Mungu na utendaji wake wa vitendo. Hata hivyo kwa sababu binadamu ameshindwa kutenganisha hizi mbili, Bibilia imekuwa na thamana ndogo. Kwa hivyo chaguo la maandiko linawakilisha anga au ufahamu wa kiroho ambao huwezesha mwanadamu kutenganisha kati ya Ukweli na dhihirisho la utendaji, kati ya Mungu kama Kanuni na kama inaakisiwa na binadamu ambayo ni dhihirisho muhimu la awali.
-
SALA YA BWANA NA UFAFANUZI WAKE WA KIROHO. Katika thiologia ya zamani sala ya Bwana, ikiwa haijaeleweka kwa sehemu kubwa, inakuwa jukumu linalo timizwa kwa haraka iwezekanavyo. Katika huduma ya Sayansi ya Kikristo, mara moja ni kumbusho kwa mwanasayansi wa Kikristo juu ya sababu yake kuwa katika huduma na ni lipi lazima afanye. Sio wito wa kazi ya mda mfupi wala huduma yote kuwa wito wa kazi ya akili ya lisa limoja. Sala ya bwana ni hotuba kuu ya majukumu saba yanayowakilishwa na huduma, ambayo huendelea katika siku saba za wiki.
Ibada yetu ya jumapili kwa ukweli inamaanisha huduma. Ni somo katika kazi ya mawazo, ufunuo wa kiroho na ukolezi wa kiroho. Hivyo sala ya Bwana ni taarifa kwa mshirika wa kanisa juu ya kazi ya kiakili. Sio mwaliko lakini hitaji. Ni wajibu na umuhimu ambao ushirika katika kanisa la Sayansi ya Kikristo inahusisha. Katika shughuli na haraka za asubuhi ya Jumapili katika matayarisho ya kuhudhuria ibada na kuwa pale katika mda ufaao, wazo linaamshwa. Baada ya wazo kuwa na fursa ya kuwa tulivu na tayari, laja hili dai pole. Ombi lililokimya huamsha mawazo ya mfanyikazi kwenye sababu ya kuhudhuria ibada na kumuonyesha umuhimu wa kufuata utaratibu wa sheria ndani ya mwongozo unaohusiana na maombi ya washirika. Katika uwezekano wa kusahau yaja ukumbusho wa jukumu letu kwa Mungu, kwa kiongozi wetu na kwa wanadamu.
Katika siku ya tatu ya uumbaji tunasoma juu ya “mmea unaotoa mbegu, na mti wenye matunda ukizaa matunda.” Maombi ya Sayansi ya Kikristo ni jitihada la kupanda mbegu ya ufahamu wa kiroho katika roho za wanadamu ili iweze kukua na kuzaa matunda.
Mwongozo unapatiana Sala ya Bwana na ufafanuzi wake wa kiroho kama somo tatu za kwanza katika shule ya jumapili, hizo zingine mbili zikiwa amri kumi na heri. Hizi somo tatu zinakaa kuambatana na tafsiri la sayansi la akili ya kimwili ambayo inapatikana katika ukurasa wa 115 wa Sayansi na Afya. Kupitia amri watoto wanafundishwa sifa za kibinadamu za akili za kimwili ambazo lazima ziondolewe. Heri zimeandaa sifa hizi bora za mawazo ambazo lazima zistawishwe ili kutayarisha katika mapokezi ya Ukweli. Alafu Sala ya Bwana na ufafanuzi wake wa kiroho unaandaa kauli kamili ya ukweli ambayo inatangaza ukamilifu , ukuu wa Mungu, na uhusiano wa binadamu kwake kama imisho lake. Katika tafsiri lake la kawaida Sala ya Bwana inapatikana kuwa kamilifu kama ombi la uthibitisho. Hivyo, katika ukweli inajumuisha majibishano ya kisayansi ambayo hutumiwa kuponya wagonjwa, na ambayo hutangaza uwepo wa milele na ukweli wa wema wote sasa na haizingatii ubinadamu kwa njia yoyote. Hivyo watoto wanafundishwa yale ambayo wanatakiwa kutoa kwa mawazo yao, na yale wanayostahili kuweka na kuendeleza , na pia tangazo la ukweli la kutumia katika utendaji. Hivyo ndivyo akili iliyo tayari kupokea funuo za juu za ukweli ambazo zinafunuliwa kupitia Somo la mahubiri kwa wanafunzi walio komaa zaidi, na waliofanywa kuwa tayari kuchukua majukumu ya ushirika wa kanisa kwa wakati ujao.
4.MATANGAZO. Matangazo yanatoa zaidi kuliko yale yanayo onekana kwenye uso. Yanawakilisha matumizi ya ufahamu wa kiroho kwa ile inayoonekana kama biashara ya kibinadamu. Ni sehemu ya elimu ya kiroho kusoma kutumia ukweli kwa ile inaitwa biashara ya kibinadamu na kwa kitu kingine chochote. Kama sehemu ya ibada, matangazo haiwakilishi biashara ya kibinadamu kama nafasi zilizopatianwa kwa washiriki kutumia ufahamu wao kwa shughuli za kibinadamu. Ikiwa haya yangeeleweka, hakungekuwa na kitu chochote katika shirika la Sayansi ya Kikristo ambayo haikuonekana kuwa kama madai ya udhihirisho. Hakuna nafasi za kibinadamu ambazo ziko na thamani yoyote kwa Mwanasayansi ya Kikristo ila kwa matumizi ya kiroho. Katika sherehe yetu ya kiroho ya Jumapili waja wito wa matumizi ya hisia za udhihirisho kwa shughuli za kibinadamu. Kutoka kwa matangazo tunasoma hatuwezi kaa katika hisia ya utu ya kuinuka kiakili na kiroho wakati wote, kwa sababu huu ni wito wa kuweka kwenye matumizi ya ufahamu wetu wa Sayansi ya Kikristo kusaidia wanadamu wenye kuteseka, kuhubiri injili na kuponya wagonjwa.
Katika thiologia ya zamani matangazo yanaweka wazi umuhimu wa muundo wa kiasili na shirika ambapo kunapatikana katika msingi wake mfumo wa kiroho na umuhimu wa kudumisha umbo hili na shirika. Ikiwa dhana hii ya kimakosa itakubalika katika Sayansi ya Kikristo basi bodi ya wamiliki wa hifadhi na ofisa watachaguliwa kulingana na msingi ya kwamba ni tu kupitia bidii ya kibinadamu na ufahamu wa kina wa biashara ndio sifa zinazohitajika kwa wagombea bila kujali ufahamu wa kiroho.
Isipokuwa kama msingi wa utendaji na maamuzi ni udhihirisho wa kiroho, kitendo lazima chanzo chake ni akili ya kimwili na kwa hivyo sio kizuri.
Katika shule wanafunzi wanafudishwa sheria alafu wanapatiwa nafasi kupitia mifano kama jaribio la ufahamu wao. Kwa njia ile ile biashara imeunganishwa na kuendesha kanisa la Sayansi ya Kikristo itakuwa sehemu ya Sayansi ya Kikristo tu kama tunaitumia kama nafasi ya kuondoa maoni ya kibinadamu zote mbili kutoka ndani na nje na Kutenda ufahamu wetu wa Mungu na uwezo wa mwanadamu wa kuakisi hekima ya Kimungu.
Katika siku ya nne ya uumbaji tunasoma juu ya taa kubwa, taa kubwa na ndogo. Katika njia ya kisayansi ya kipekee ya udhihirisho ya kuimarisha umoja wa binadamu na Mungu tunatumia mwangaza mkubwa, wakati ambapo mwangaza mdogo unasimamia matumizi ya kibinadamu ya sayansi, ambayo hupatikana katika shughuli zote za biashara na kazi za kanisa na washirika wake. Huu mwangaza unaitwa mdogo kwa sababu unatoa mwangaza mdogo wa kiroho; lakini uko na umuhimu kwa sababu unafundisha akili ya kibinadamu ya kwamba wakati wowote inaegemea juu yake yenyewe iko na makosa au gizani. Hivyo wakati tu inaegemea kwenye hekima ya Kimungu ndio mwangaza wa kweli na inaangazia kila mwanadamu.
Kutokana na haya tunaweza soma somo linalosaidia linalohusiana na mikutano yetu ya biashara. Katika Sura ya kwanza ya Mariko tunasoma juu ya uponyaji wa mkoma ambaye Yesu alishauri asiseme kitu chochote kwa mtu yeyote. Lakini yule mtu akachapisha kwa kirefu na kueneza mpaka ng’ambo tukio mpaka Yesu hangeweza kuingia mji kwa wazi na akasukumwa jangwani. Hitimisho kutokana na tukio lile ni kwamba huyu mtu alikubali nguvu za uponyaji za Yesu lakini sio hekima yake. Ila zote zilikuwa za Kimungu. Katika Sayansi ya Kikristo mkutano wa Jumatano jioni unasimamia kukubali uponyaji wa kiroho unaotokana na Akili ya Kimungu, na mkutano wa biashara unasimamia kukubali hekima pia ikiwa chanzo chake ni kile kile. Kanisa la Sayansi ya Kikristo imeanzishwa kwa kanuni hizi mbili muhimu. Ibada ya Jumapili inaweka bayana ufahamu wa Mungu na kanuni na sheria za Sayansi ya Kikristo katika matumizi yake pana. Mkutano wa Jumatano jioni unaweka bayana matunda ya kuponya wagonjwa na mkutano wa biashara matunda ya udhihirisho wa hekima ya Kimungu. Mkutano wa Jumatano jioni unasimamia matokeo ya uwezo wa mwanadamu kugeuka mbali na ushuhuda wa hisia za kimwili au kushawishiwa na mawazo ya wengine ili kuimarisha ukamilifu wa kila mtoto wa Mungu. Mkutano wa biashara unasimamia uwezo wa binadamu kugeuka mbali na ushahidi wa hisia za kimwili au kushawishiwa na mawazo ya wengine ili kuimarisha uwepo na kazi ya Akili ile moja katika mahali pa akili ingine yoyote. Ikiwa pointi moja ya hizi mbili muhimu haijatiliwa maanani, ingekuwa sawa na mtu kuendesha mashua akitumia kasia moja; anaweza tu zunguka kwa duara. Hivyo matangazo huita umaakini wetu kwa yale ambayo ni muhimu kwani kudhihirisha na kuakisi hekima ya Kimungu katika awamu zote za kazi ya kanisa na maisha ya kila siku, ikionyesha ikiwa na umuhimu sawa na kuponya wagonjwa. Tukikubali Akili ya Kimungu kama mponyaji wa wagonjwa na sio anayepatia wanadamu hekima, tunatuma wazo la Kristo kwenye jangwa ambapo mwishowe tutapelekwa kwenda kulitafuta, kama wana wa Israeli nyakati za zamani ambao kushindwa kwao kupata hekima, ambayo ni utiifu wa Kimungu uliwazuia wasiingie nchi ya agano.
-
FUNZO LA MAHUBIRI. Katika thiologia ya zamani mahubiri ilikuwa ni kiongezeo ya dhana mbaya ya kwamba Kristo alikuwa anaweza kumfanyia mwanadamu kazi yake. Hii inaonyesha mtazamo ya kwamba kupitia juhudi za muhubiri zizi lake lingeokolewa. Kama matokeo ya dhana hii waumini wanajitahidi kutekeleza matokeo ya uchunguzi wa Bibilia wa mchungaji wao ili kuokolewa. Katika ibada ya Jumapili ya Sayansi ya Kikristo funzo la mahubiri lahitaji akili ilio wazi kwa upande wa waumini, lakini hata kila mmoja aweze kupata ufahamu ambao utamuwezesha kufanya sehemu yake katika mpango wa wokovu; kila mshirika anatarajiwa kusaidia kufanya kazi ya kiakili ambayo italeta upokevu wa Ukweli. Ili kutimiza kusudi yake ya kiroho, ibada lazima iwe na mazingira ya uponyaji ambayo ni matokeo ya juhudi za kazi ya kila mtu binafsi. La sivyo kuna hatari ya kurudi nyuma kwa kutoendelea kwa thiologia ya zamani. Ukweli wa ibada za kanisa yetu ni mazingira hii ya uponyaji kwa sababu inatoka kwa Mungu kupitia binadamu, na yale yanatoka kwa Mungu ni ya Ukweli wakati wowote.
Mahubiri ambayo inawashirikisha wasikilizaji wasio changia inaweza kuwa mwakilishi wa utumwa wa kiakili ulioko, kwani kawaida hufanya mtu kuweka mawazo yake kwake yeye mwenyewe, ambayo ni aina ya kufikiria ilio ndogo sana. Watu wengi wanaokataa kuhudhuria kanisa hawana hisia mbaya juu ya dini, lakini dhidi ya Athari za kujipenda zinazotokana na mahubiri ya kawaida. Hata funzo letu la mahubiri linakosa katika kusudi lake ila ibadilishe mawazo ya binadamu kutoka kwake mwenyewe na kwa hivyo kuweka huru mawazo yake kuanza safari yake ya utukufu, akimimina wema kwa wanadamu wote, safari ambayo huelekeza kwa Mungu.
Funzo la mahubiri linasisimua utendaji wa akili, mtazamo wa kiroho, na umaakini. Inaonyesha muungano wa sheria na wanabii. Sheria au Ukweli unasisitizwa hasa katika Bibilia, na unabii unaelezewa kikamilifu katika Sayansi na Afya kama mbinu ya kiroho ambapo sheria ya Mungu hufanyishwa kazi.
Katika siku ya tano ya uumbaji tunasoma juu ya uzalishaji wa uumbaji wa Mungu kujaza maji katika bahari, duniani na mbinguni. Somo la mahubiri linakusudiwa kupanua wazo kwa upana na urefu wa matumizi ya Ukweli wa kiroho ndivyo tuweze kuangalia kwenye uumbaji wa Mungu na kusema kwa ukweli, “ Nikipanda juu mbinguni, upo. Nikichukua mabawa ya asubuhi na kukaa katika sehemu za mbali za bahari; hata pale mkono wako utaniongoza, na mkono wako wa kulia utanishikilia.” {Zaburi 138} Hivyo funzo la mahubiri, likifafanuliwa kwa usahihi linafunua ya kwamba giza ambayo inatokana na fikira mbaya zinaweza ondolewa kwa wakati wowote na mawazo sahihi ya kiroho, ambayo hufunua uumbaji wa kweli, ulio na matunda na wa milele.
-
MKUSANYIKO. Thiologia ya zamani ina juhudi ya kumfanya mwanadamu kufungua kibeti kulingana na mafundisho ya dini ya kwamba ni baraka kupatiana kuliko kupokea; pia anafanywa kuelewa hata hivyo, ya kwamba kutoa ni uwekezaji mzuri, ukimletea mafanikio ya mali pia. Hili kwa kweli ni jaribio la kuufanya wema wa kiroho kuwa wa kibinadamu. Sayansi ya Kikristo hufanya kila mshirika kuwa mweka hazina wa kanisa kwa hali ya kwamba kila mmoja anapata jukumu la kudhihirisha Akili kama chanzo pekee cha ugavi, na hivyo inawekwa wazi umuhimu wa kutoa ili kupokea, na sio baraka za mali ya kiasili, lakini kupaa kwa ukuu kwa wema wa kiroho. Mkusanyiko unaashiria ukweli kwamba, ingawa ukweli ni bure kwa wote ila unagarimu kitu hisia za kibinadamu za mwanadamu kupata uhuru huu.
Katika siku ya sita ya uumbaji tunasoma juu ya baraka kuu ambayo Mungu amempa mwanadamu. Lakini mwanadamu ameitumia vibaya kusudi ya hii baraka, akiifanya majaribio kwa uchovu, raha, na kutokufanya kazi, na pesa hupatiana alama ya utumiaji mbaya wa baraka hizi za Mungu, ambazo zikitumiwa vizuri zinapatia mwanadamu uhuru zaidi wa kazi ya Mungu, na ukitumiwa vibaya unaharibu hamu ya mafanikio na kumfanya mwanadamu kutosheleka katika mwili. Hivyo, mkusanyiko katika ibada ya Jumapili sio tu onyesho la udhihirisho wa washirika katika kuimarisha Akili kama chanzo pekee cha ugavi, lakini pia inaonyesha ya kwamba binadamu lazima aachilie au kutoa dhabihu ili kupata baraka za Mungu. Katika Ukweli mwanadamu tayari yuko na hizi baraka kutoka chanzo ambacho hakiishi, kwa hivyo dai la Sayansi ya Kikristo sio ya kwamba lazima aziachilie, lakini kwamba lazima aachilie utumiaji mbaya wa baraka zile, ambayo imemfunga macho kwa kazi yake sahihi kwa Mungu. Alafu utumiaji sahihi wa baraka za Mungu, amabazo amepewa bure, zitampatia uhuru zaidi wa kiakili ambao anaweza tumia kwa ukuzaji wa kiroho wa wanadamu.
Mary Baker Eddy, mgunduzi na mwanzilishi wa Sayansi ya Kikristo, alikusanya utajiri wa kutosha. Hata hivyo hakutosheka na ambacho pesa ingenunua. Kwa kweli aliteseka wakati mwanafunzi wake yeyote aliyepotoka, alijaribu kumfanya kuwa ametosheleka kupitia mali ambayo pesa inatii amri yake. Mama Eddy alitazama utajiri wake kama alama, inayopatiana uhuru wa kiakili ambao ulimpatia nafasi kubwa ya kubariki wanadamu.
Hivyo katika kanisa la sayansi ya Kikristo michango ambayo inaeleweka kwa kiroho yanamaanisha shukrani na udhihirisho, ukionyeshwa katika huduma ya ukweli kwa wanadamu wenzetu. Ikifafanuliwa kama alama ya binadamu au pesa, zinawakilsha anasa, umiliki wa binadamu, uzembe na hofu ambayo hufanya vita dhidi ya kiroho na ambayo lazima iachiliwe.
-
BARAKA YA MWISHO WA IBADA. Katika dini iliyopotoka sala ya mwisho inapendekeza wazo kwa mhubiri na washirika, “ Asante kwa Mungu, imeisha mpaka juma lingine.” Katika Sayansi ya Kikristo sala ya baraka ni tangazo la kipekee kwa washirika Kwenda moja kwa moja nyumbani kukamilisha udhihirisho ambao ibada imeanzisha kwa mgeni kwa kujua mbegu iliyopandwa ni nzuri, ya kwamba itabaki kwa mchanga uliomzuri na inazaa matunda. Hii inaambatana na siku ya saba ya uumbaji, siku ya sabato ya mapumziko ambayo Mungu aliyaona yote aliyoumba na tazama ilikuwa nzuri sana; na Mungu alipumzika siku ya saba. Sala ya baraka ni kukusanya vipande vyote ili hakuna kitu kinachopotea. Kile ambacho mgeni amepata kupitia masikio lazima ipandwe katika ufahamu. Ni vipi washirika wanaweza kufanya udhihirisho huu wa mwisho kama watabaki baada ya ibada wakijiingiza katika mazungumzo ya upotovu, ambayo inaweza ng’oa mbegu nzuri kabla ipate nafasi ya kupata mizizi? Mwanasayasi ya Kikristo anatakiwa kwenda nyumbani na kupumzika katika ufahamu ya kwamba yote ni wema , na wema unajaa kwenye nafasi yote, na mahali popote wema upo, hakuna kitu kingine chochote kinaweza kuishi; hivyo wema ambao umeletwa katika ibada unabaki na hakuna kitu kinachoweza kupotea. Kupitia juhudi hii ya mwisho, wema uliojaa ambao unafurika ili kuponya na kubariki utarudi kwa wale waliofungua madirisha yao kutoa.
-
MUHTASARI. Katika kumalizia tunaweza tangaza ya kwamba kauli ya kisayansi ya uwepo ikisomwa katika mwisho wa ibada, inasimamia kifuniko ambacho kinawekwa katika chupa ya mawazo, kuhifadhi yaliyomo dhidi ya kumwagika – ukweli ambao umefunuliwa, mazingira ya Mungu ambayo yamekubalishwa ndani, na uponyaji wa akili na mwili ambayo ni matokeo.
Kauli ya kisayansi ya uwepo ni kauli ya mwisho na ya kimsingi ya Sayansi ya Kikristo ambayo hujumuisha vipengele viwili ambazo zinajumuisha kila somo la mahubiri, kwa majina, kauli za kukubali au hofu, na kwa matumizi au udhihirisho. Haya yanasimamia Roho na bibi harusi, ukweli wa kimsingi na matumizi yake.
Wakati mmoja Mama Eddy alielekeza katika darasa mwakani 1866 ya kwamba lazima tujenge kutoka chini kwenye ardhi, na pia njenga kutoka juu mbinguni, na kwamba makutano ya juhudi hizi mbili ikp na alama ya ufahamu.
Kila somo la mahubiri limeundwa kusaidia mhusika kujenga daraja yake ya kiroho kutoka kwa hisia mpaka kwa nafsi, na kauli ya kisayansi ya uwepo inamalizia juhudi hii. Tukisisitiza ya kwamba “Kimwili ni kosa la kimwili,” tunajenga kutoka chini duniani; na tunapotangaza ya kwamba “Roho ni Ukweli wa milele” tunajenga chini kutoka mbinguni.
Yale ambayo yanahusikana na mbinguni lazima yakubalike kama yamekamilika tayari, kwa sababu mwisho wa daraja sio lazima ujengwe, umejengwa tayari. Unapoungana na mwisho wa daraja kutoka upande wa dunia, hakuna haja ya matumizi ya kibinadamu ya sayansi; kwa sababu kimwili na makosa yote yatakuwa yameangamia. Kujenga kutoka dunia kunamaanisha kupunguza Imani katika kimwili, na kujenga chini kutoka mbinguni, ni kuongeza hisia za kiroho mpaka Roho anatambulika kama yote.
Kukutana kwa pande zote mbili za daraja kunapatikana mahali matumizi yanakuwa uhakika. Ifikapo hapa majibizano yameondolewa kwa sababu mtu anaujua ukweli kwa asili kama vile anajua jua linang’aa hata kuwe na mawingu.
Wakati mwana mpotevu aliporudi nyumbani, au kujenga kutoka duniani, babake alikutana naye kwa umbali, au alitoka juu mbinguni kukutana naye, na pahali hapa pa kukutana pakakamilisha daraja ambayo ilimwezesha kurudi nyumbani.
Ni vizuri Mama Eddy alitumia mfano wa makutano ya pointi hizi mbili za daraja yetu kama ufahamu, kwa sababu tunahitaji ufahamu kuondoa uongo, na pia kuvalia ukweli au yaliyo kweli.
Kila somo la mahubiri katika robo yetu linajumuisha pande hizi mbili za daraja, na zimefupishwa kwa kikamilifu katika kauli ya kisayansi ya uwepo, kusoma kwake ambako kunafikisha kileleni mwa ibada ya Jumapili.