Kusikiliza Mungu |

Kusikiliza Mungu

Iliyoandikwa na Gilbert Carpenter


Ikiwa unatarajia kusikia sauti ya Mungu, lazima ukubali ukweli kwamba sauti yake sasa inatuma ujumbe bila kikomo, na ikifanya hivi kwa sababu unamiliki uwezo wa kusikia.

Mwanadamu hupokea na kusikia sauti ya Mungu. Akiitafuta na kufanya bidii kuipata lakini hana ufahamu wa kufanya haya hadi hitaji litakapojitokeza. Wakati anaposema yale ambayo yeye mwenyewe hakujua, kisha anajua ya kwamba ni Mungu anaongea kupitia kwake.

Kwa hivyo, ukitafuta kusikia sauti ya Mungu na unaonekana kama hufanyi hivyo, usihuzunike. Kila siku fanya juhudi ya kufungua mawazo yako na kuacha Mungu akuongeleshe; na kama hujasikia kwa masikio ya kiasili au una ufahamu wake kwa mawazo ya ufahamu, ichukue kwa imani nzuri. Amini ya kwamba imewekwa kwenye kumbukumbu ya kibao cha akili yako, ya kwamba unaweka hazina mbinguni, katika ufahamu wako wa roho, na wakati unaostahili ukija, utaweza kuitoa, na kujua yale Mungu amekuwa akisema kwako, kwa yale utasema kwa mwingine.