Ukweli kuhusu uongo |

Ukweli kuhusu uongo

Iliyoandikwa Na Gilbert C. Carpenter


Inawezekana wanafunzi kusoma maandishi na nadharia ya Sayansi ya Kikristo na wafanye matamko ya kisayansi ambayo hawajadhibitisha. Hali hii ilionyeshwa na mwanafunzi aliyejiwasilisha kwa Mama Eddy asubuhi moja na dalili za homa kali. Mama Eddy aliuliza alivyohisi na akapata jibu, “Niko sawa.” Onyo kali la Bi Eddy bado linalia masikioni mwangu kama hoja muhimu na ya kuangaza kwa kila mwanasayansi ya Kikristo ajue. Ni, ” Sema ukweli kuhusu uongo,” Angemaliza kumwelekeza mwanafunzi huyu huenda angesema, “Nikiwa na dalili kama hizo sisemi sina homa mpaka nijue, na ninapojua, dhihirisho limefanyika.

Kauli hii, “Sema ukweli kuhusu uongo” imekaa nami kama kitu kilicho na msaada zaidi alichokisema. Imebadilisha mawazo yangu hadi kufikia kipimo cha kuweza kudumisha uainishaji wa mawazo na kauli katika Sayansi ya Kikristo, hivyo kwamba naweka kila kitu chini ya vichwa viwili -aitha ikiwa kama ukweli kuhusu uongo , au ukweli kuhusu Ukweli.