Kazi isiyoweza kushindwa |

Kazi isiyoweza kushindwa

Kutoka kwa mahadhara ya Sayansi ya Kikristo ya PETER V.ROSS


Unaweza pata hofu ya kwamba ukosefu wa haki kutoka kwa wengine kunaweza shinda kusudi ile, inaweza zuia kupata mambo yote mazuri Mungu ametayarisha. Hakuna kitu cha aina hiyo kinachoweza fanyika. Hata sio upumbavu wako mwenyewe unaweza airisha bila kikomo hatima, mpango wako wa milele ” unapopiga hatua kuelekea kwa zawadi kuu ya wito wa Mungu katika Kristo.”

Unakumbuka asubuhi ile Yesu aliletwa mbele ya Pilatu kama amehukumiwa kwa kujipatia mamlaka ya kuwa mfalme. Wakati mmoja katika kesi, wakati alikataa kuongea, Pilatu alimwambia: “Hauniongeleshi? Unajua ninayo nguvu ya kukusulubisha au kukuachilia?” ” Hauna nguvu yoyote dhidi yangu, ” Yesu akajibu, ila iwe umepatiwa kutoka juu.”

Kisha Pilatu akampatiana kwa walio mshtaki na akasulubiwa. Lakini kwa leo Yesu alirudi akiwa hai kama vile alivyokuwa mbeleni. Jinsi kidogo njama ilivyofanikiwa isipokuwa kuharakisha na kutukuza kazi ya mtu yule wa ajabu. Hakukuwa na nguvu yoyote ile katika umati wa kelele au hata katika serikali ya Warumi kushinda kusudi ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa nayo juu ya mwanaye.

Hakuna hali, dhuluma, hakuna nguvu katika dunia ya kushinda kusudi ya Mungu ambayo ako nayo juu yako ikiwa utafanya chaguo sahihi na ukae nao kwa udhabiti. Na maisha bado yako mbele yako.