Biashara
MARTHA WILCOX
Dunia kamwe haitawaijua mfanyi biashara mkuu kama Yesu. Hakuna taratibu zilizomzuia kufanya utoaji wa mikate na samaki, divai katika harusi, na pesa ya ushuru mara moja. Yesu hakujua kitu chochote kuhusu kuchelewa au uwasilishaji wa mustakabali. Yesu alitambua uwepo wa wema uliopo sasa, na kitu pekee kiliopo.
Kila shughuli ya Akili ya Kimungu kimsingi ni shughuli ya kibiashara, na kwa kikamilifu ni ya kiakili. Tukiongea kimwanadamu, kila shughuli ya akili ya kimungu ni ya kusudi ya kukidhi mahitaji ya wanadamu. Hakuna kitu kingine kinachoendelea ila shughuli ya biashara. Biashara za kila jina na aina ni shughuli ya milele; na kama Yesu, biashara ya kila mmoja wetu ni kutumia , kuonyesha na kuwa shughuli hii ya Akili ya kimungu.
Kwa kuwa hatujatenganishwa na Mungu, Akili yetu, sisi sio kitu kando na biashara yetu. Asili yetu na uwepo ni utawala, ni umiliki, ni imisho, ni ushahidi. Tunayo nafasi na uwezo. Kwajili tunadhihirisha umilele wa Akili ya Kimungu, kisha wakati wowote utambuzi wa juu wa biashara huonekana kwa ufahamu wetu, kunaonekana pia ushahidi wa biashara bora zaidi.
Wanabiashara mara nyingi hufikiria biashara zao zinadhibitiwa na serikali, au na hali mbaya ambazo hawawezi dhibiti. Lakini kwa kweli, biashara hutawaliwa na kanuni ya Kimungu pekee. Tunajumuisha biashara yetu katika mawazo yetu, na inategemea ufahamu ambao tunakaribisha kuihusu. Hatuko ndani ya bishara yetu, bishara yetu iko ndani yetu – katika mawazo yetu. Njia pekee ambayo tunaweza badilisha hali ya biashara ni kubadilisha mawazo yetu. Hakuna kitu kinachotekelezwa na hali za nje ambacho kinaweza ingilia biashara zetu.
Tunadhibiti biashara yetu kupitia ufahamu ya kwamba biashara ni ya kiakili na ya kiroho na inatawaliwa na Akili ya Kimungu, au biashara yetu inatudhibiti kupitia imani yetu ya kwamba iko kando nasi na ni ya kimwili na inatawaliwa na akili nyingi. Tuna dhibiti biashara yetu kwa ukweli ambao tunakaribisha, au biashara yetu inatudhibiti kwa imani ambazo tunakaribisha.
Uhusiano katika biashara “inategemea na inatoka kwa kanuni ya Kimungu.” Kanuni ya Kimungu ina njia nyingi za kumkabidhi ugavi mwanabiashara. Hizi njia ziko wazi, ni bure na hazina vizuizi. Zinafanya kazi kama sheria za kinyume za uwepo ambazozina mpangilio na zimeshikanishwa pamoja. Ile ambayo ni dhahiri kwa wazo la kibinadamu kama mtu mmoja au kitu akikidhi mahitaji ya mtu mwingine ni sheria ya kinyume ya uwepo, ikiakisi ukamilifu wake kwa kila imisho lake. Tunatakiwa zaidi na zaidi, kutambua na kutumia hii sheria ya kinyume ya uwepo ambayo milele inafanya kazi kwa niaba yetu na kwa niaba ya wale tunafanya nao kazi.
Hizi vitu za kina za Akili sio kila wakati rahisi kuelewa, lakini zitafunguka kwa wale wako na macho ya kuona na masikio ya kusikia. Kuna wale wataendanisha na mitindo ya kawaida ya mawazo ya kibinadamu kwa msimu mwingine, lakini kuna wengi ambao watainuka kwa viwango ambazo hazijajulikana mbeleni.