Kanisa
Iliypandikwa na Martha Wilcox
Katika Sayansi na Afya na ufunguo wa Bibilia. Mary Baker Eddy anatupatia ufafanuzi wa kanisa kwa maneno haya, ” Ni muundo wa Ukweli na Upendo; chochote kinachoegemea na kinachoendelea kutoka kwa kanuni ya kimungu.”
Kanisa ni taasisi ile ambayo inapatiana uthibitisho wa faida yake na inapatikana ikiinua wanadamu, ikiamsha ufahamu uliolala kutoka kwa imani za kimwili kuelekeza kwa ufahamu wa mawazo ya kiroho na udhihirisho wa Sayansi ya Kikristo, hivyo ikifukuza mapepo, au uovu, na kuponya wagonjwa.” {583: 12-18}
Kusudi la shirika letu ni kukidhi hitaji la wanadamu la Ukristo ulio na vitendo na hapo Ukristo unaotosheleza. Ukristo unaweza tosheleza kwa kikamilifu wakati unapendelea sio tu kwa ufunuo, ila kwa fikra na mantiki. Ufunuo na fikra lazima ziendanishe.
Kama vile Yesu alikuwa zaidi ama chini kipengele kinachosumbua kwa maisha ya dini wakati wake, kwa kupuuza kwake kwa ushirikina na theologia ya uongo, ndio Ukristo wa Sayansi unapata upingamizi kutoka kwa wazo kihafidhina la dini tukisema, ” Kila kitu ni Akili isiyo na mwisho na udhihirisho wake kwa kuwa Mungu ni yote kwa yote.” Walisema juu ya Yesu nyakati za zamani, ” Anajifanya mmoja na Mungu.” Leo Mkristo msayantisti anajifanya mmoja na Mungu.
Theologia ya uongo, Mungu na binadamu, wawili, ambayo kwa vizazi vingi ndio imekuwa msingi wa dini zote na msingi wa kanisa zote, ndio utendaji mbaya au kinyume cha dhana ya Ukweli, ambayo kila kanisa la Sayansi ya Kikristo iko chini yake.
Huu utendanji mbaya unaweza kutushirikisha katika kuzingatia yale ni muhimu ambayo hayana umuhimu kabisa; Inaweza kutushirikisha katika kukimbiakimbia kwa ustadi, tukisumbuka kwa mambo mengi kama Martha wa zamani. Tukifikiria kutenda wema ni muhimu zaidi ya uwepo. Yesu alisema Mary alichagua vema, Kusoma kuwa badala ya kufanya.
Kuwa, kwa sababu ni Mungu akiwepo, siamilifu kamwe, kutojali; ingekuwa ingepinga wazo juu yake lenyewe. Mungu pekee aliyepo, ni akili, na hii Akili moja lazima itumiwe kama Akili yetu, au tuko na miungu wengine. Tunajaribiwa kuwa na hisia ya kwamba lazima tufanye kazi kumfikia Mungu na kwamba labda siku moja tukiwa wazuri kutosha, tutakuwa katika umoja na Mungu. Tunajaribu kila mara kuunganisha Mungu na mwanadamu kwa kujaribu kumfanya mwanadamu kuwa kama Mungu ilhali ni tu kama Wakristo wa kisayansi tunadhihirisha au kuwa mwanadamu aliyekamilika. Kuelewa Mungu, sisi ni wanadamu. “Mimi ni yote. Ufahamu mwingine kando nami hauwezekani.” { Umoja wa wema 18:25}
Mtazamo wa mawazo ambayo humwangalia Mungu sio heshima; sio ukristo au Sayansi; ni hali ya hisia ambayo inachochea maendeleo. Ni upagani kwa kweli. ” Tunapoteza umuhimu wa juu wa nguvu zote, wakati baada ya kukubali ya kwamba Mungu, au wema ako kila mahali na ana nguvu zote, bado tunaamini ya kwamba kuna nguvu ingine ambayo inaitwa uovu.
Hii imani ya kwamba kuna akili zaidi ya Akili moja ni mbaya kwa Theologia ya Kimungu kama hadithi za zamani na kuabudu sanamu na upagani.” {Sayansi na Afya 469: 25-30}
Kukubali imani ya kiulimwengu na kuwa kwa mawazo mtu anayehitaji ukombozi na dunia inayohitaji kuokolewa, kipande cha pili cha ufafanuzi wa kanisa imefuatiliwa kama amri na tumejaribu kufanya kitu kisichowezekana kwa kujaribu kupitia jitihada za kibinadamu, kuinua wanadamu kuwapatia uthibitisho kwa faida ya Sayansi ya Kikristo bila Sayansi ya Kikristo.
Dunia inajua ni nini kitakachoponyesha? Hakika ufahamu wa dunia unaohitaji uponyaji sio ufahamu wa Kristo ambao utaiponya. Hatuwezi peleka Sayansi ya Kikristo kwa mtu yeyote kwa wakati wowote. Kanisa letu sio la kusudi la kuleta wema kwa wanadamu lakini kuonyesha wanadamu wema ulioko tayari – uwepo wote, unaodhibitika kama Akili.
Ufunuo wa Kiroho lazima uongoze hamu ya Ukweli. Hatushiriki katika jitihada la ukristo kama makanisa mengine. Wao ni Wakristo kama vile dunia inavyoita Ukristo, lakini sisi ni Wakristo wa sayantisti na kama wasayantisti kwa kimsingi hatujishughhulishi na kuponya wagojwa na kuokoa wenye dhambi, hata hivyo kama Wakristo wanasayansi tunafanya yote
mawili. ” Yesu alikuja kuokoa wanadamu kutokana na ndoto hizi ambazo alikaa kama aliendanisha nazo; kutoka kwa udanganyifu unaoitwa dhambi ukweli, na binadamu mwenye dhambi, anayehitaji mwokozi; undanganyifu unaoitwa ugonjwa ukweli, na mwanadamu mgonjwa, anayehitaji mtabibu; udanganyifu ya kwamba kifo ni ya kweli kama uhai. Kutokana na mawazo kama yale – uvumbuzi wa mtu wa kimwili, moja na yote – Kristo Yesu alikuja kuokoa wanadamu, kupitia uwepo wa daima na wema wa milele.” {Umoja wa wema 59 :19-3}
Sisi ni Wakristo wasayantisti sio kwa sababu kitu kimetujia kutoka nje, lakini kwa sababu kitu kinaendelea ndani mwetu. Hii kuja kwa milele kwa Kristo, huu uwepo wa milele wa Ukweli ukifunguka kwa ufahamu wetu unatufanya kuwa Wakristo Wasayantisti. Sayansi ya Kikristo haingeletwa kwa mtu yeyote na yeyote, hata kama hivyo ndivyo inakaa kufanyika. Hakuna kitu kinachoendele nje kila mtu binafsi. Sayansi ya Kikristi ni ufumbuo wa Kristo na ufufuo wa ufahamu. Hakuna mtu anayefufuliwa kutoka nje; hakuna kitu kinachofanyika nje.
Roho ya msukumo, hamu ya kueneza injili ni theologia ya uongo. Ahadi yote ya msemaji wa neno ni kukubali binadamu aliye kandp na Mungu. Mtu binafsi aliyeamka kutosha kuona kitu kuhusu Kristo kila wakati atapata hisia za binadamu zikiwa karibu kuthibitisha kuamka kwake. Madai na ugavi ni moja.
Mama Eddy anasema, “Wapatie kikombe cha maji baridi katika jina la Kristo, {kwa jina la umoja} na usiogope matokeo.”
{ Sayansi na afya 570: 16- 18} Hii ndio kamili mwana sayansi Mkristo atafanya. ” Kikombe cha maji baridiā¦.na kadhalika.” ni utambuzi wazi zaidi wa sehemu ya mtoaji ya umoja wa Mungu na binadamu! Upendo mkuu kama huu hana mtu, ya kwamba aliweka chini hisia zake za asili kwa sababu ya marafiki wake; au anawashirikisha marafiki wake kwa kuangaza kwake kwa Mungu. Hii ndio umbo la Ukweli na Upendo ambao utapatiana uthibitisho wa faida yake na utainua wanadamu.
Hitaji kubwa leo sio metafizikia safi; Sayansi katika Ukristo ambayo itafanya kazi za Yesu. Njia pekee ambayo tutaanzisha kanisa letu leo ni njia ya uponyanji wa kisayansi. Mgawanyiko katika makanisa yetu huja kwa sababu wengi hawadumishi mtazamo wa kisayansi wa Akili; Migawanyiko yote huja kwa sababu ya hisia za ubinafsi au maoni ya ubinadamu ya sawa ua isiyo sawa.
Wema na uovu ni maneno ya uhusiano tukiyatumia kuhusiana na mwanadamu. Mkriso msayantisti anavutiwa tu na Ukweli; katika Ukweli na uovu – hakuna maoni juu ya swala hili. Tunaketi ndani ya hukumu ya jirani yetu, tukisahau ya kwamba Akili inaweza dhihirisha uwepo wake kama tu mawazo ya kweli, na kwamba hakuna kanisa lolote duniani linaweza dhibitisha faida yake mradi tu hakuna Ukristo wa Kisayansi.
Mawazo yetu lazima yainuliwe juu ya jambo la kibinadamu tunaloita kanisa. Kwa sababu hakuna kitu kinachokuwapo kikawaida ila dhana za kiakili kuhusu Ukweli au Mungu – kama mawazo ya Roho – Tukifikiria juu ya kanisa letu kama shirika la kibinadamu ambalo linafanya wema, hatufikirii Ukweli hata kidogo; na kwa hivyo, ambayo tunaita kanisa la binadamu haina uzima, hauna Uhai, haina Roho, kanisa letu ni wazo; umbo la Ukweli na Upendo. Kama la Ukweli, ni ya milele, haitingisiki, ni thabiti, safi. Kama wazo la Upendo, inashirikisha yote, inadumisha yote, inalinda wote, inaongoza wote. Hii ndio kanisa yako?
Kanisa yako ni kanisa ya Sayansi ya Kikristo au ni kanisa ya Ukristo ambayo iko na nadharia nzuri, imeundwa na washiriki wanaojaribu kueneza injili kwa njia tofauti, lakini bado wakiwa na wazo la Mungu akijali uumbaji wake mahali kwingine?
Tunabeba shirika hili mbele kama tu tunainuka kwa ufahamu wa umoja wa Mungu na binadamu na ukamilifu wa Mungu. Shirika la ubinadamu halitakiwi kutuweka katika utumwa tena kama vile tunaruhusu miili yetu ya kibinadamu kutuweka watumwa. Akili ya kimwili na mwili wake ni moja; Akili za kimwili ni moja na kanisa la kibinadamu ni moja. Tunachukua msimamo wetu kwa nguvu dhidi ya utumwa wa miili yetu juu ya maumivu na vikwazo, ilhali tunafurahia katika mwanadamu mzuri ndani ya kanisa letu.
Hakuna kitu kizuri katika muundo wa kimwili kama hivyo, wala hakuna kitu kizuri katika kanisa la binadamu kama hivyo. Kwa kweli, kama mwanadamu, sio mwili wala kanisa. Kama vile leo tunafananisha kwa agizo bora na utaratibu kwa maisha ya kila siku – tunakula, kulala, kuvaa nguo, kutenda kulingana na udhihirisho wa juu wa Akili kutuweka huru kutokana na vitu hivi vya kimwili, – kwa hivyo kwa kanisa tunafuata kulingana na utaratibu na amri bora zaidi -tuko na shughuli zetu mbalimbali;
Hotuba zetu, walimu, watendaji, vitabu; lakini lazima tutende kwa udhihirisho zaidi wa Akili, kutuweka huru kutokana na utumwa wa dhana ya uanadamu na kwa njia na sababu za binadamu.
Shughuli zetu za kibinadamu, hotuba, waalimu, watendaji ndio kuonekana kwa binadamu ufahamu wa Mungu, Upendo wa Kimungu, kuthibitisha uwepo wake kwa kukidhi mahitaji ya binadamu ili kwamba kama ufahamu wetu unakuwa safi, hotuba zetu, waalimu wetu, kanisa letu, kila kitu muhimu kukidhi mahitaji ya wanadamu kwa ukombozi -haitakuwa na vikwazo ambazo zinaambatana na dhana ya binadamu.
Katika kazi yetu ya Sayansi ya Kikristo, daima mbele yetu kuna huu mchakato wa ukombozi wa ufahamu na kwa hivyo mabadiliko yanayoonekana ya dunia yetu. Kuna madai kila wakati mbele yetu kuwa kile tulicho, – umbo na ufananisho wa Mungu, kile Mungu anachokifahamu.
Kwa hisia tunajua udhaifu wetu, magonjwa yetu, ukosekanaji wa furaha, sio zetu, na tunakimbia hapa na pale tukitafuta majibu kwa shida hizi. Mwishowe tunataambua ya kwamba dunia yetu inarudi kwetu ufananisho wetu; ni kwa utambuzi huu, marekebisho yetu na ukombozi zinaanza; kwa sababu tunaona, ingawa wa giza, kwamba majibu ya shida zote ni kabisa katika hatua ya ufahamu wetu, kwa sababu hapo ndipo shida ziko. Tunaanza kutambua ya kwamba hii hamasisho ya hisia au msukumo kulegeza minyororo yetu , kutoroka vikwazo vyetu, huu mtafaruku; unatoka kwa ukweli wa Kimungu juu ya ukamilifu wetu sasa; ya kwamba ufalme wa mbinguni sio tukio la mbali, lakini tajiriba inayowezekana sasa.
Kwa kiwango ambacho tunakubali ukweli huu, kwa kukaribisha mawazo ya kweli ambayo ni ya uwepo wa Mungu, tunapata ya zamani yamepita; tazama yote yamekuwa mapya. Tunaita huu mchakato ukombozi wa ufahamu.” Huu ufahamu wa Kristo unafamu kila wakati na tu juu ya mawazo ya Kimungu; kamilifu, isiyoharibika, isiyobadilika , isiyoonekana; na inapofunguka kama ufahamu wako {ambayo ni hiyo} wa mawazo ya Kimungu, ile inayoonekana ni akili mpya na mwili mpya. Tunapata tunamiliki kwa hisia uaminifu, haki na nguvu, huruma, ushujaa ambao tunaita tabia.
Tabia sio binafsi: ni mtu binafsi.Tabia ni sifa za Mungu, kutoonekana, kutobadilika, umilele, kujiendesha kuonekana kwa dhahiri kama sisi wenyewe kwa sababu ya ufahamu mmoja. Kumbuka marekebisho sio mabadiliko, kutengeneza kitu upya; ni utu wa Kimungu ukieleweka bora zaidi, mawazo ya Kimungu yakionekana kwa kibinadamu
Kama mwili na akili iliyobadilika. Kuonekana kulikobadilika kwa kibinadamu ni tukio la Kimungu na sio mabadiliko ya kibinadamu. “Imani iliyoboreshwa haiwezirudi nyuma.” {Sayansi na Afya 442:19}
Marekebisho haihusishi mapenzi ya binadamu, kujirekebisha au kujaribu kuhimili jambo fulani ; haihusiki na kukomesha jambo moja ile tunaita mbaya na kuanza kufanya lingine ambalo tunaita sawa. Hii ndio njia ya zamani ya mabadiliko. Kwa njia moja marekebisho ni kwa hisia, tunatamani kurekebisha kwa sababu kuna mwamko ndani ya ufahamu juu ya uwepo wa kweli.
Sayansi ya Kristo inadai marekebisho. Ni hitaji muhimu kwa sababu ya ghuba kubwa inayoonekana kuwepo leo kati ya udhihirisho wetu wa Ukweli na Ukweli wenyewe. Sayansi ya Kikristo inafunua umoja wa Mungu na binadamu, na ufunuo huu una uwepo au mwili halisi kama sisi wenyewe na dunia yetu kama tunavyoelewa ukweli huu.
Hii ghuba inakuwa nyembamba leo kwa kiwango ya kwamba tunaelewa na kutenda ufunuo wetu, tukihifadhi maoni sahihi, tukitumia Akili ambayo pia iliyokuwa ndani mwa Kristo Yesu. Kisha dhihirisho yetu na ufunuo zitashirikiana kama ilivyokuwa na Yesu. Pia atashuhudia Kristo kama amefanywa mwili kama binadamu aliyekamilika. “Vile ninavyoelewa ubinadamu wa kweli ndivyo ninavyouona ukiwa bila dhambi, -usiojua dhambi kama muumbaji aliyekamilika.” { Umoja wa Wema 49: 8-9}
Marekebisho ni ya kibinafsi kabisa; hakuna kitu kinachotoka nje kwa ufahamu. Hatuwezi rekebisha mwenzetu. Adui yako ni “kiumbe au kitu nje ya uumbaji wako?” { Mchanganyiko wa maandishi 8:9} Rafiki yako ni ” kiumbe au kitu nje ya uumbaji wako?” Marekebisho haiwezi onekana kwa ulimwengu bila kwanza kuonekana kibinafsi. Tukijirekebisha tunarekebisha ndugu yetu. Tumefanya kazi kwa mda mrefu chini ya imani ya kwamba tunaweza rekebisha mtu mwingine. Hii sio ukweli, na tunaweza saidia ndugu yetu mwanadamu kwa kiwango tu tunachojisaidia. Yote tunayoweza kufanya kwa marafiki au adui ni kwa mawazo au ufahamu, kwa sababu ndio mahali pekee ambapo pana uwepo kwetu sisi. Marekebisho kila wakati huleta mawazo ya nidhamu. Tunapata nidhamu kuwa muhimu kwa sababu ya hii imani katika pande mbili, hii ghuba kati ya binadamu na Mungu.
Nidhamu ya kujitengeneza bi utambuzi wa kudumu wa ukosefu wa kitu katika uhalisia na utambuzi wa utambulisho wa kiroho kama nafsi pekee ya kweli. Mama Eddy anasema, ” Kujinyima, ambako tunaweka chini yote kwa sababu ya Ukweli, au Kristo, katika vita vyetu dhidi ya uovu ni kanuni katika Sayansi ya Kikristo.” { Sayansi na Afya 568:30}. Tunapopata ufahamu ya kwamba hakuna kitu cha kubadilisha, tunapata kujua nidhamu sio muhimu tena.
Mpaka hii upande mbili hauonekani tena – mpaka ghuba iwe nyembamba kati ya ufunuo na dhihirisho la sasa – Nidhamu ni muhimu kwetu, muhimu kama tu chakula, nguo, nyumba zetu. Lazima tutumie hisia bora zaidi za nidhamu ambayo tumedhihirisha kuwa yetu. Kujiwazia kwa kimwili katika aina yoyote ni kujikataa kwa uwepo tuliopatiwa na Mungu, na wakati mapenzi ya kibinadamu na nidhamu ya kibinadamu sio Sayansi ya Kikristo, ni uovu mdogo, ambao unatokana na kiwango cha uamko wa kiroho kuhusu ukosefu wa ukweli wa binadamu wa kiasili.
Dhambi pekee ni hisia potofu ya Uhai katika mwili, na tukiendelea na dhambi kwa kuipa huduma, tutachelewesha dhihirisho letu la utawala. Hakuna kamwe utawala katika mambo ya kimwili; kwa kila wakati ni utumwa. Kuangalia Kimwili tukitafuta kitu chochote kunaondoa utawala wetu, uhuru wetu, heshima yetu, ambayo nidhamu{ uamko wa umuhimu wa kutojipenda} unarudi kwetu.
“Anayepata ufahamu wake mwenyewe , kujidhibiti mwenyewe, na ufalme wa Mungu ndani yake, ndani ya ufahamu wake, anaokolewa kupitia Kristo, Ukweli. Wanadamu lazima wanywe ya kutosha kutoka kwa kikombe cha bwana na mwalimu wao kutojijali uanadamu na kuharibu madai yake ovu.” { Mchanganyiko wa maandishi 161: 14-18} ” Sasa sisi ni wana wake Mungu.” Sasa sisi ni ufahamu wa Mungu wake mwenyewe. Huu Ukweli unapokubalika unakua nidhamu ya kujitengeneza kwa kutulazimisha kudhani hisia ya kiakili kuelekea kwenye kila kitu na kila mtu ambayo Akili, Mungu anatarajia. Imani fulani katika Mungu ni uzembe wa akili na kwa hivyo haituadhibu; inatuinua kihisia.
Bila ufahamu ambao Sayansi ya Kikristo hutupatia kuhusu Bibilia, marekebisho siku za zamani yalikuwa juu ya hofu. Sheria ya Musa na tafsiri yake ya dhambi, ilikuwa ni laana badala ya wokovu, na mpaka ufunuo wa Kristo, hukumu na adhabu ilitawala binadamu. Ukristo leo umedumisha kwa kutosha sheria ile kuweka hukumu na adhabu kama himizo la marekebisho. Hii sio Sayansi ya Kikristo. Marekebisho ni elimu; Tunafanya vyema zaidi kwa sababu tunajua vyema zaidi.
Paulo akasema, ” Sheria haikufanya kitu chochote kikamilike, lakini kuleta kwa tumaini bora zaidi kulifanya.” { Wahebrania 7:19} Marekebisho haipatikani kupitia kuendana kwa nje kwa mandiko ya sheria, wala hofu, wala kufanya nje ya sahani kusafi, lakini himizo la ndani, lakini utambuzi usioepukika na ambao ni halisi na kweli.
Utayari wetu wa kukubali sheria ya Upendo, kutenda ” Uwepo wa Mungu kila mahali tuendapo,” ni hatua ya kwanza ya mchakato wa marekebisho, na kujiwekea nidhamu kwenye nguvu. Kukubali huku kwa Mungu katika njia zetu zote kutafuta huku kwa ufalme wa Mungu kwanza na haki yake, ni mtazamo kwa kiwango wa umoja wa Mungu na mwanadamu na kwa hivyo makataa ya utambulisho wa uongo. Hatua hii inaweza onekana ikiwa na usaidizi wa kukosa raha wakati fulani katika tajiriba yetu, kwa sababu inatulazimisha kuachilia umwili unaodai kutembea nasi kila mahali tuendapo.
Kitendo hiki cha ndani, hii himizo ya kujua na kufanya mapenzi ya Mungu, wema, ni Akili ikitenda; ni kitendo cha kujitolea cha Akili kinachoonekana kwa binama isiyo ya hiari. Kwa maneno mengine, tunatamani kurekebisha, tunatafuta wema bila hiari, kwa sababu ya ukweli wa Kimungu, ya kwamba ” Yote ni Akili isiyo na mwisho na dhihirisho zake, kwa sababu Mungu ni yote kwa yote.” Kufikiria juu ya ijulikanayo kama tendo la kibinadamu, kufikiria juu ya msukumo au tamanio kama kitu chochote ila tendo la hiari la Roho, au Ukweli, ni idhini ya imani ya akili mbili. Tunatenda kwa hisia. Hata hivyo, wakati ambapo tunapatia wazo kwa utafutaji wa kibinadamu, tunakataa msukumo wa Kimungu na tunakosa kuthibitisha kifanano au umiliki wa yale milele ni yetu, lakini ambayo haiwezi onekana bila umoja, Mapenzi, tamanio, chaguo – yote ni imani ya uwepo ulio kando.
Tena , Akili hii moja milele inajifahamu na mawazo yake na mawazo haya yanaonekana kufunguka kama ufahamu wetu kupitia elimu, kusoma, wazo la asili, lakini yanaonekana kwa sababu Akili hii moja ndio Akili yetu. Elimu, kusoma, wazo asili inaonekana kama matokeo ya huu umoja, dhibitisho kwamba sisi ni kifano – Akili ikifahamu wazo lake.
Kuangalia uvumbuzi, kusoma na wazo la asili ni ghali na zinatakiwa kukuza akili ya kimwili kutokana na yenyewe, kutoka kwa yote ambayo ni ya kiasili. {Sayansi na Afya 195: 19-22} Tumaini, imani, na ufahamu inaonekana kuangazia na kuokoa akili ya binadamu, lakini yale ambayo yanafanyika kwa kweli ni ufahamu wa Kristo kuonekana kama imani, tumaini, ufahamu
na ile inayoonekana kama ufahamu wa kibinadamu na hofu yake, ujinga, kikomo inawekwa mbali.
Uwepo wa kila mahali wa Akili unatenda kama hisia ya kudumu ya kutafuta ile ambayo tunakaa kukosa, kwa hivyo mapenzi ya kibinadamu kwa kweli ni ushawishi wa Kimungu .Kutafuta, haijalishi ni nini tunachotafuta ni jitihada kuwa ambacho tulicho kwa Kimungu. Hata ambaye anatafuta pesa au kitu kingine cha asili anatafuta kwa majibu ya ukweli wa Kimungu wa uwepo wa milele wa wingi na kutosheleka; hii ndio dhana ya juu ya Ukweli, na anafanya kazi chini ya hisia yenye kikomo au isiyo kamilika ya ambayo ni kweli.
Wakati mmoja anatafuta ushirikiano au afya, mtu anadai tu yale ambayo ni milele yake. Kupitia kuvunjika moyo mara nyingi, kuna uamsho kuhusu ukamilifu wa sasa wa binadamu na Sayansi ya Kikristo inamjia mtu binafsi. Alafu mbinu inabadilika, ikiamshwa kwa kiwango kwa ukweli ya Akili moja kama Mungu, mtu anatambua ya kwamba hii Akili inajumuisha kila kitu ambacho mmoja anakaa kutaka au kuhitaji. Kabla ujue kama unaihitaji, uko nayo, kwa sababu Akili ile ni Akili yako; kwa kweli hungetaka ile hauna, na hauwezi pata ile hautaki.
Kama tunataka kitu, wakati tunaacha kukitaka, tunathibitisha tuko nayo kwa sababu tumeacha kukatisha uwepo wake. Uwepo wetu unajumuisha wazo sahihi ya yote ambayo tutawai taka. Kama Ukweli huu unafunguka, hakuna kutaka tena au kutafuta; tunatambua ya kwamba kutaka na kutafuta kunakatisha kupata.
Hakutakiwi kuwa na tamanio la kibinadamu, hakuna kutaka, hakuna kuelezea, hakuna kupanga. Wakati kuna tamanio la kujitolea kwetu, tunakataa uwepo wa kila mahali – tendo la kujitolea la Akili.
Njia ya kutotafuta ndio njia ya Sayansi. Kumbuka, ukweli ni hai , ikileta kwenye mwangaza dhana zilizoboreshwa. Kadri tunaweza pumzika kwenye kutokuwepo kwa uwezekano wa yale yanayoonekana kwa ufahamu wa kibinadamu kama ambayo tunahitaji, badala ya jitihada za kibinadamu kupata kitu, haraka zaidi tutathibitisha “Ufalme wa Mungu.”
Msimamo wetu lazima uwe ukamilifu, Mungu aliyekamilika na binadamu aliye kamilika – hakuna kitu kinachohitajika au kutamanika. Alafu tamanio la kusonga mbele, kutafuta wema kunabadilishwa na mchakato wa wema zaidi ya tamanio la sasa. “Kupitia kupaa kwa Roho, Mungu, kanuni ya Kimungu ya Sayansi ya Kikristo, kwa urahisi hutawala malengo na vitendo ya Mwanasayansi. Uamuzi wa Kimungu unapatiana busara na nguvu; inatupilia milele wivu yote, ushindani, mafikira maovu, kuongea mabaya na kutenda; na akili ya kibinadamu, hivyo inapoondolewa, inapata amani na nguvu nje yake.” { Mkusanyiko wa maandiko 204: 27 -2}