Kesi ya uponyaji |

Kesi ya uponyaji

Kutoka kw Hotuba na Martha Wilcox


Imani ya uongo haiendelei na haiwezi endelea katika ufahamu mara inapokubalika kuwa ni imani pekee na sio hali ya mwili.

Mwanamke alikuwa na mkono uliyoharibika na haukuwa na uwezo, hali ambayo ilisababishwa na ajali. Alikuwa amemaliza mbinu zote za watendaji na kila wakati mhadhiri alikuja jijini aliongea na wao na kupata matibabu bila mafanikio. Alienda safari mingi na bwanake na kila walipoingia mji mkubwa, alitafuta mtendaji mara moja, akaenda kwake, akamweleza kuhusu huu mkono na akapata usaidizi bila mafanikio.

Mwishowe walifika jiji la New York na mara tu walipotulia hotelini, alichukua jarida lake, kwa sababu juu ya yote alikuwa anataka mkono ule upone. Alipata jina na kufanya miadi. Lakini akingojea kama amekaa, akajiambia, ” Sitasema tena kuhusu huu mkono wakati mwingine. Nimechoka kurudia haya tena na tena na ni imani tu,” msemo ambao ulikuwa mdogo kwake

Alisema kwa mtendaji, ” Unajua Mungu huponya, sivyo? Unajua anaweza ponya kitu chochote?” Mtendaji akamjibu, naam, Mungu anaponya kwa kufunua kwetu kwamba kitu chochote kinachokaa hakijakamilika ni mzima, na imani ya uongo haiwezi kufanya tusijue vile mambo yalivyo, yamekamilika na mzima.”

Alimpatia matibabu yule mwanamke na kumzindikisha mpaka mlangoni mwa ofisi. Alipokua nje alipata mkono wake umerejeshwa kwa kimo na shughuli yake, kamilifu kama mkono wake mwingine. Alikuwa ameachilia imani yake ya uongo, na hatua yake ya kwanza katika mwelekeo huo ilichukuliwa alipoamua hataitambua hali ile tena. Imani yoyote mbaya inaweza achiliwa “bila kikwazo kutoka kwa mwili.” {S&H Ukurasa 253: 23}