Mchakato wa Uponyaji |

Mchakato wa Uponyaji

Kutoka kwa Hotuba na MARTHA WILCOX


Ni nini mchakato wa uponyaji? Uponyaji ni ongezeko la ufahamu wa ukamilifu, badala ya kuondolewa kwa ugonjwa. Tunatakiwa kutambua ya kwamba mchakato wa uponyaji hufanyika kulingana na ufunuo wa kiroho wa mtu binafsi.

Uponyaji wa Uvimbe

Mwanafunzi mwaminifu wa Sayansi ya Kikristo wa miaka mingi alijipata mfungwa wa ile inayojulikana kama uvimbe wa misuli. Kwa miaka uvimbe ulinenepa na ingawa alikuwa na watendaji kadha, hali ikawa mbaya zaidi badala ya kupata nafuu. Akaongozwa kuomba usaidizi kwa mtendaji mwingine aliyejitolea wakfu. Mtendaji akamwambia, “ Unatafuta urahisi katika kimwili; unatafuta njia ya ugonjwa kutolewa kwa mwili wako, au unatafuta njia ya kumpenda Mungu, Ukweli, na roho yako yote na kuomba kupata Akili ya Kristo?” Myendaji pia akasema, “ Kile ambacho kinatakiwa kutolewa au kufutwa ni imani yako ya kwamba wewe ni kiumbe kilichotenganishwa na Mungu, ambacho kimeundwa na mapenzi ya kibinafsi, kudai haki ya kibinafsi, na kujipenda; na kizingiti hiki cha makosa , hii imani ya akili mbili, inaweza tolewa tu au kuangamizwa na kisuluhishi cha ulimwengu cha Upendo.” Alafu akatazama Sayansi na Afya pahali Mama Eddy anauliza swali, “ Unampenda Bwana na Mungu wako kwa roho yako yote, na kwa nafsi yako yote, na kwa akili yako yote?” {S&A 9:17}.

Mwanafunzi akaona ya kwamba kama vile Upendo huu wa Mungu aliye mmoja uliendelea kuwa mkuu katika mapenzi yake, ukihamisha au kutoa kabisa, kwanza katika akili, alafu kimwili, chochote ambacho hakikupendeza au kisichokuwa kama Kristo katika ufahamu wake. Kwa wiki kadha alitumia wakati wake mwingi kwa masomo ya Bibilia na lwa maombi na mandishi ya kiongozi wetu, na akaanza kuwa na uhuru wa akili mpaka akasema, “Hata kama inaonekana ni kama kuna uvimbe katika mwili wangu, ninamjua na kumpenda Mungu aliye mmoja kabisa.”

Hatimaye hofu ya uvimbe ikaanza kupotea. Alafu ikaja utambuzi wa furaha ya kwamba kwa kuwa Mungu ni uhai wote, dutu yote na maarifa yote, kwa kweli kimwili haingeweza kumfanya kuamini ya kwamba ni kitu kinachoishi, kilicho na ufahamu na kinachokua. Siku kadha baada ya maono haya wazi ya ukamilifu wa Mungu, aliona matokeo ya fikira sahihi. Uvimbe ukatoweka bila uchungu na bila adhari za baadaye.

Huyu mwanafunzi alikuwa amepata mchakato wa kuponya magonjwa yote, KUFIKIRIA KIROHO. Alisoma kupitia tajiriba hii, kama vile sisi wote lazima tusome, ya kwamba lazima tuufanyie kazi ufahamu wetu wa Mungu, kama vile tunavyotakiwa kuufanyia kazi ufahamu wetu wa hisabati au muziki…..

Uponyaji haimanishi uangamizaji wa magonjwa. Tukifikiria ya kwamba tunapata afya tu kama tunaangamiza ugonjwa , tunaendeleza ugonjwa ule. Ufahamu wa Mungu aliye mmoja ndio afya yetu na ndio huangamiza magonjwa kabisa. Wakati Ukweli ulifunuliwa kwetu kupitia Sayansi ya Kikristo, ya kwamba binadamu amekamilika kama vile Mungu amekamilika, kulifunuliwa kwetu pia ukweli kwamba ufunuo wa kiroho ndio mchakato wa uponyaji.