Mwili |

Mwili

Iliyoandikwa na Martha Wilcox


Mwanasayansi wa Kikristo anatambua thamani kuu ya mwili wake, kwa sababu mwili hubainisha au kutoa ushahidi kwa akili yake. Akili ya mtu itakuwa haijajidhihirisha au kutojulikana bila mwili wake.

Mwili halisi, maumbile ya mtu ni kwa urahisi wazo linaloonekana. Mwili au dhihirisho la akili, ni ya kiakili kama akili na unaambatana na akili.

Mama Eddy anasema. ” mambo yote ya kimwili yanatokana na akili kabla ya kudhihirika kama ya kiasili.” { Hea ukurasa wa 12}. Pia anasema, ” akili za kimwili zinasababisha hali zake za kimwili.” { S&H ukurasa 77}

Taaluma nyingi za matibabu zinaamini ya kwamba mizozo ya kimwili ni dhihirisho za mizozo ya kiakili, ya kwamba shinikizo la damu kikamilifu ni akili, shinikizo la damu ambayo huletwa na matukio ya kurudiwa kiakili, hisia, au msisimko wa uoga au mfadhaiko. Wanafupisha ugonjwa kama mmenyuko wa kimwili au mmenyuko wa mwili kwa hali ya kiakili au hisia za akili, wakisema kwamba hasira, kasumba ya maadili na hofu haijalishi ni jinsi gani imehalalishwa, iko na athari mbaya kwa kazi ya moyo na inasababisha shinikizo la damu sugu au shinikizo la damu la juu.

Katika Sayansi ya Kikristo, tunafahamu kuwa mwili unatawalwa na akili, sio kwa kiwango lakini kikamilifu, na kwamba njia pekee ambayo mtu anaweza kuboresha akili na kwa hivyo kuboresha mwili, ni kwa kujua ukweli kuhusu yote akili na mwili.

Kazi kubwa kwetu ni kupata makadirio halisi ya miili yetu ya kibinadamu. ” Tunaleta” kila wazo ambalo ni, kila sehemu ya mwili, “katika utiifu kwa Kristo.”

Usiogope kitu chochote ambacho mwili wako wa sasa unaonekana ukifanya. Kila kiini, nyuzi, tishu , tezi, kiungo au misuli ya mwili wa binadamu ipo sasa hivi katika Akili moja kama wazo, na kila wazo linatangaza, ” Ninaakisi Mungu, ninadhihirisha Mungu.” Kila kiini, nyuzi ya uumbaji wangu unadhihirisha uhuru wa Mungu, au kutangaza, “MIMI NI.” {S&H ukurasa wa 162}

Pale ambapo mwili unaonekana kuwa wa kiasili, hapo ndipo mwili wa kiroho, ukionekana kwa ufahamu wetu kama kioleshi, umbo, rangi, dutu, kitendakazi, na kudumu.

Mama Eddy anasema, ” Akili isiyokufa, inayowatawala wote, lazima ikubalike kama kuu katika isemekanayo kama ufalme wa kimwili, pamoja na ya kiroho.” {S&H ukurasa wa 427}.

Mwili wangu wa sasa sio umbo la undongo mbali ni hali ya kweli ya ufahamu.

Tukielewa mwili, tunaelewa Mungu, Akili. Mwili ni ukomo wa Mungu au Akili iliyodhihirika. Mwili ni mfano wa uwepo wa wazo zisizo na mwisho za kiroho za Akili.