Kubaliana na mpinzani wako haraka |

Kubaliana na mpinzani wako haraka

Tazama marejeleo binafsi kwa kila kidokezo kutoka kwa mwandishi


Kutoka kwa Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko, 1910, iliyoandikwa na MARY BAKER EDDY, ukurasa 162

Daktari anakubaliana na “mpinzani wake haraka,” lakini kwa vigezo tofauti kuliko mtaalamu wa metafizikia; kwa kuwa daktari wa maada anakubaliana na ugonjwa, wakati mtaalamu wa metafizikia anakubaliana na afya na kupinga magonjwa.

Kutoka kwa maandishi yaliyokusanywa, na Bicknell Young, ukurasa 58

Mtoe mgonjwa kutoka kwa shimo la mafadhaiko, ufasiri wa nafsi; mtoe kutoka kwake. Unaweza waambia, “bila shaka hauja kata tamaa;” toa akili ya kimwili kutoka ndani mwake. “Sijakatishwa tamaa na haiwezi nipata.” Hauwezi jaza wengine fikira; ni mvuto wa kinyama. Kumbana na mapingamizi haraka; haujaipata; ni akili ya kimwili.

Kutoka kwa mahubiri na Makala, na Doris White Evans, ukurasa 70.

Majibu ndio Daraja ambayo mvuto wa kinyama unatufikia. Wazo sumbufu ndio kifaa kikusanyacho mapendekezo ya makosa.

Suluhisho ni nini? Jibu lapatikana katika kukataliwa mara moja kwa mapendekezo makali. Bibilia yatuambia tukubaliane na mpinzani wetu haraka wakati tuko njiani naye. Mama Eddy anafafanua haya katika Sayansi na Afya kwa kusema, “Usiwe na madai yoyote ya dhambi au magonjwa kwa mawazo yako. Itoe fikirani kwa uhakika ya kwamba sio halali.” { ukurasa 390}

Mfanyi kazi mmoja mwenye hekima wakati mmoja akasema, kuwa na haraka katika ukweli ili kwamba makosa yatakuwa yanachelewa kila wakati.”

Kutoka kwa Sayansi na Afya, mafundisho yake sahihi, na Herbert Eustace, ukurasa 167 {nambari ilioko juu}, ukurasa 223 {nambari ilioko chini}

Amri ya Yesu “Kubaliana na mpinzani wako haraka,” inamaanisha kukanusha hisia ya uongo haraka kabla ya kuikubali. Wakati “unakubali,” utaona Akili moja ikiwa mambo yote mara moja, na kwamba kila neno linakiri ukamilifu huu.

Kutoka kwa “vidokezo juu ya uponyaji” na Rev. Frank E. Mason

Tena Yesu akasema: “Kubaliana {makubaliano} na mpinzani wako haraka wakati mko karibu naye; ili kwamba isije ukawekwa gerezani, ambapo utabaki mpaka ulipe ndeni yote.” “Mawazo ni vitu,” na tukikaribisha mawazo ya kuzozana, yatakuwa vitu kwetu na tutawekwa gerezani {ugonjwa}, ambapo tutabaki mpaka hukuma ya matibabu ya maada yametimika kupitia kwetu. Tunaweza kabiliana na mawazo haya mbaya na kuyamiliki kwa kujua ya kwamba chochote ambacho ni ushuhuda wao, ni uongo wa sasa.

Kutoka kwa Mary Baker Eddy, maagizo yake ya kiroho, na Gilbert Carpenter

Lazima tutambue kila siku ya kwamba mpinzani hawezi zuia wanafunzi wanaostahili na waaminifu kupokea baraka za Mungu. Wanafunzi waliopatiana miaka yao yote kwa kazi ya Sayansi ya Kikristo lazima walindwe ndio waweze kupokea zawadi yao yote, kama sio kwa sababu ingine yoyote ila kwamba dunia iweze kujua ya kwamba mtu hawezimfanyia Mungu kazi bila kutunukiwa zawadi tele naye. Baraka za huduma zilizo kusanyika hazitakiwi kuzuiliwa kwa wafanyikazi waaminifu, kwa sababu ya kukosa kukabiliana na uongo ambao unadai kuwaibia baraka kama ile.

Kuna wingi wa kungonja kwa kila mwanafunzi ambaye ni mwaminifu kwa kupatiana mda na kazi yake kwa Mungu. Fikiria vile Sayansi ya Kikristo itainuka kwa makadirio ya dunia, wakati imedhibitishwa wakati umri unapita mfanyikazi mwaminifu, inamletea amani ile ya Mungu ambayo inapita ufahamu wote, kutokuwepo kwa hofu na ukosekaji, ndio aweze kutazamia siku za usoni na shida zake kwa utulivu na ujasiri.

Kutoka kwa kukesha, maombi, na majibizano, iliyopatianwa na Mary Baker Eddy, ukurasa 124

Mwangaza wa milele unalinda mawazo katika dutu ya nafsi yake. Akili yenye uovu hazina nguvu za kukataa, kukatiza, kupinga au kukanusha Mungu; hakuna nguvu za kusimamisha kazi ya Sayansi ya Kikristo.

Kuna kukanusha kwa kila majibizano ya uovu na kuitangaza, kubaliana na mpinzani wako ‘’haraka.’’

Mungu atakanusha kila majibizano ya uovu, kabla itufikie, kupitia neno, ambalo ndilo upanga wenye ncha mbili, ambalo linaishi na kudumu milele.

Lazima tukumbane na madai ya ujanja, kueneza fitina, kuingilia kwa akili ya kibinadamu.

Kutoka kwa Mary Baker Eddy, nyayo zake za kiroho, iliyoandikwa na Gilbert Carpenter, ukurasa 236

Ikiwa mvuto wa kinyama ungeleta giza katika mawazo ya mtu yeyote kuhusu tajiriba yake, alijua maono kama yale yaliyopotoka yalikuwa dhibitisho kwamba mawazo ya ule mtu yalikuwa yamemilikiwa na mpinzani na kwa hivyo hangeweza kuelewa ufunuo wake sawasawa. Kwa hivyo kuambatanisha jina lake kwa ufunuo wake, alifanya vigumu kwa mtu yeyote kuja kwa Sayansi ya Kikristo kutoka kwa msingi wa mawazo usio sahihi, bila kufichua ukweli huu katika mtazamo wake ulio na makosa juu yake.

Kutoka kwa Mary Baker Eddy, nyayo zake za kiroho, iliyoandikwa na Gilbert Carpenter, ukurasa 139

Hakuna mtu ambaye angekosoa mbinu ya Mama Eddy, kwa sababu zilizaa matunda bora. Aliona umuhimu wa mwanafunzi kushinda uzoefu wa mwanadamu wa uzembe, ambao kwa njia zingine ungempumbaza kwa kukubalia mvuto wa kinyama na uongo wake. Alikubali kiwango cha juu nyumbani mwake, kwamba kuna wale waliona kama msukosuko usio na maana. Hata hivyo, aliweka lengo juu kwa kusudi, ndio iweze kutimika kupitia udhihirisho. Hatua kama hiyo ilikuwa yenye hekima ya kiroho, kwa sababu iliwafanya wanafunzi kuboresha juhudu zao zaidi, na kuwafanya kuwa maakini. Matunda yake yalionekana katika udhihirisho wao.

Paulo alitumia mbinu hii ya kujitahidi kuuleta wakati wa sasa, badala ya juhudi iliyochelewa, alipoandika, “ Sasa ndio wakati uliokubalika; tazama sasa ndio wakati wa wokovu,” ikimaanisha kwa hivyo ya kwamba sasa ndio wakati wa kumtafuta Mungu, kwa hivyo binadamu lazima afanye hima. Wito huu wa utendaji ni muhimu kuamsha wanafunzi kutoka kwa kuweka kando kwa uzembe juhudu sahihi kwa mstakabali.

Kutoka kwa pointi 500 za kukesha na Gilbert Carpenter, ukurasa 211

Tazama usije kosa kutilia maanani onyo:….”lile unalolifanya, lifanye haraka,” kama vile bwana alimwambia Judas. Ukichukua kaa lililo na moto na uliangushe haraka, halitachoma vidole vyako. Hivyo tambua mvuto wa kinyama kwa ilivyo na isivyo; lakini Fanya kwa haraka ndio usikawie kwake ili ukaitikia mapendekezo ya kwamba unapigana na kitu; tambua ya kwamba hakuna ukweli katika madai yote ya uovu inayopinga Mungu na watoto wake; jua ya kwamba hakuna nguvu za kishetani ambazo zipo kuzuia mwanadamu kuwa na haja na yale ambayo itamuweka huru kutokana na udanganyifu na kumrejesha kwenye uhuru dhabiti na uwiano – ambao kisayansi ni tajiriba ya ufalme wa mbinguni. Katika kukumbana na madai ya mvuto wa kinyama, uguse kwa wepesi na kwa haraka iwezekanavyo, kwa kuwa tafakari ya huu uongo wa kiulimwengu utakufanya kuujenga katika mawazo yako, badala ya kuubomoa. Wakati wa kuteleza kwenye barafu nyepesi, teleza kwa haraka iwezekanavyo, ndivyo isivunjike.

Kutoka kwa Sayansi na Afya, toleo la kwanza na Mary Baker Glover, ukurasa 394-398

“Kubaliana na mpinzani wako kwa haraka, wakati uko karibu naye, isiwe wakati wowote akupeleke kwa jaji, na jaji akupeleke kwa ifisa, na ofisa akufungie gerezani; Kwa hakika nasema kwenyu, hautatoka pale mpaka ulipe deni yote.”

Hii ilikuwa ni kanuni moja ya Bwana wetu ya kuangamiza makosa na kuponya wagonjwa. Ililejerea hata hivyo, sio kwa taratibu za kisheria, au mchakato wa maada, lakini kwa mahakama ya kiakili na hukumu. Mpinzani hakuwa binadamu, lakini makosa; na mwelekeo, vile kuendelea na dhambi au magonjwa ambao utalazimisha kupitia imani adhabu ya kukiuka sheria ambayo sio sheria, kwa kiasi kama haki ndio maana ya sheria, na ukosefu wa haki unaonyesha ukosefu wake. Mwalimu atalipa adhabu ya magonjwa kwa kutekeleza kazi yake vizuri? Au akili iliyo na ukuu, kwa sababu ya wema iliyotenda, ipate kuwa mawindo kwa magonjwa? lazima binadamu ateseke katika mikono ya Mungu, kwa Kutenda wema? Mama atanyong’ona au kuteseka, kwa sababu ya uzazi, kama hio ndio maumbo ya uwepo wake? Kwa sababu ya uchovu, baridi au kuvunjwa kwa ziitwazo sheria za afya, bila kujua tunakiri ya kwamba kuna hatari ya kuwa wagonjwa, na hali hii ya kiakili inaamua ile ya kimwili; kwa hivyo, “kubaliana na mpinzani wako haraka; sema kwa imani hii, “Rudi nyuma yangu, shetani, hauzingatii mambo yaliyo ya Mungu, lakini yale ya mwanadamu;” sio sheria ya maadili iliyovunjika ambao adhabu imeshikanishwa lakini hali ya maada, madai kutokana na kiyu ambacho hakina ufahamu na hakiwezi kuwa na haki. Mungu hana sheria ya ukosekanaji wa haki, makosa yatokana na imani, na sio Ukweli.

Kumalizia haraka kwa matibabu ya makosa, ndio ilikuwa kanuni ya bwana wetu alioacha ya kuitupilia nje. Hakupendekeza sheria za afya kwa ufahamu wetu. Juu ya sheria ambayo sio ya Mungu, tuko na haki ya maadili ya kutoa hukumu, na kutoa hukumu; katika kila tukio la maada, au mwili, ukitawala mwanadamu, inahukumiwa kwa haki, na haiwezekani kimaadili kama vile inaonyesha hitaji la hekima ambayo inaisambaratisha. Matumaini pekee katika magonjwa au dhambi, ni kukubaliana haraka na mpinzani wako; hivyo kusema, ukijaribiwa, au magonjwa yanapotokea, kuangamiza majaribu, au magonjwa, mara moja kutoka akilini na kuikataza kujitetea dhidi yake ili kwamba usije ukawa mawindo yake katika imani juu ya ile kesi. Katika msingi huu wa akili, wakati dalili za ugonjwa zinaonekana, ukijua zinapata msingi wake katika akili kabla ya mwili, “kubaliana kwa haraka na mpinzani wako,” kataa pendekezo la kwanza katika akili ya kwamba wewe ni mgonjwa; pinga hisia na Sayansi, na kama unaweza angamiza mchakato wa uongo wa sheria, kwa jina lingine imani yako katika ile kesi, hautawekwa gerezani au kifungo. Walio wagonjwa lazima wasiwahi kiri kuwa wagonjwa; kwa maneno mengine, kukubali ya kwamba wao ni wagonjwa, kwa kuwa wakati ule watakuwa wenye kuingia gerezani, kulingana na sheria ya imani. Tazama msimamo wa Sayansi katika tukio la kwanza, usiwahi kiri hisia katika maada, au kwamba mwili waweza kuwa na uchungu, au unaweza kuwa na madai yake wenyewe, au nguvu za kumfanya mtu ateseke; zingatia msimamo huu wa sayansi na kupigana na msimamo wa zamani mpaka uuharibu, na utapona. Kukubaliana haraka na mpinzani wako mwanzoni wa ugonjwa ni kuchukua msimamo ulio na mzozo juu yake, na kudhibitisha nguvu zako juu yake. Kutokiri ugonjwa, ndio kushinda ugonjwa; na kama unaelewa Sayansi ya uwepo, hautakiri ukweli kwa lingine ila kwa Mungu na wazo lake. Unaposema “ Mimi ni mgonjwa,” unakiri uko na hatia, ndivyo kusema, unakiri maada iko na hisia na utapelekwa kwa jaji, kwa maneno mengine, kwa mikono ya imani hii ambayo itakupatiana kwa ofisa {ugonjwa}, kiongozi wa binadamu wa kimwili ambaye anakurusha gerezani na kufunga utu wake wote. Lakini magonjwa hayana ufahamu wake yenyewe, au sheria, ya kufanya haya. Unajihukumu mwenyewe bila kujua, kwa hivyo, “kubaliana na mpinzani wako haraka;’’ kumbana na kila tukio kama mkubwa wake, na tazama imani yako, badala ya mwili wako; usifikirie juu ya sheria za maada, ndio uweze kuthamini vema sheria za kiroho za uwepo, ndio, utawala wa binadamu juu ya maada. Kumbana na kila hali mbaya kwa kutumia Sayansi, badala ya imani ya hisia, na utaweza kuimudu.

Makosa ni mnyonge mbele ya Ukweli, na kifo ni awamu ingine tu ya ndoto ya uhai katika maada, ambapo tunakutana katika kila pointi ufahamu wa uhai unaoendelea, na imani zilezile za kushinda, na makosa ya hisia na kushinda kupitia Sayansi. Lazima tuelewe njia ya kutoka kwenye dhiki, au kwa ukweli hatuko nje, na uwiano na maisha ya milele ya binadamu haitaeleweka kamwe mpaka kila kosa la hisia imeharibiwa. Kuelewa uchumi na uwezo wa uwepo wa mtu, metafizikia lazima ichukue mahali pa fizikia, na akili, badala ya maada, kushauriwa katika magonjwa, hofu, na adhari zake kwa mwili sio ya hiari. Hofu ya magonjwa na kupenda dhambi ndio msingi wa utumwa wa binadamu; lakini juu ya haya anaweza shinda juu ya mwili wake. Akili inafanya kazi juu ya mada kabla ugonjwa kuonekana juu ya mwili; lakini mtu hana utambuzi wa imani yake ukileta magonjwa mpaka uonekane. Tunatazama kwenye hisia kwa ushahidi wa ugonjwa, lakini hakuna hisia za kibinafsi, ila iwe maada ina ufahamu wake na inashikilia maswala ya Uhai. Kwa sababu akili inafanya kazi bila ufahamu wa hisia, wagonjwa wanasema ni kwa njia ipi akili ilisababisha magonjwa, “Sikuwai fikiria juu ya ugonjwa mpaka wakati ulipatikana kwa mwili wangu.” Lakini akili iko na haraka, na sababu; hakuna kitu kinachoanzia katika maada; mmea unakua kutoka kwa ufahamu wa milele – kabla tuuite maada; lakini upofu wa kimwili na matokeo yake kali, hudhibitisha haja yetu ya ufahamu utendaji wa akili na adhari zake; tunatakiwa kusoma akili zaidi na maada kwa upungufu, kama tutajipatiana kwa nafsi katika udhibiti wake juu ya hisia. Tunaweza angamiza ugonjwa , pia dhambi, kwa kusoma chanzo chake na asili yake katika akili, badala ya mwili, na kupata imani ambaye huileta.

Kutoka kwa hotuba na Martha Wilcox, ukurasa 328

Wakati umevamiwa na imani ya kwamba hakuna matokeo katika kazi yako, kumbaliana na mpinzani wako. Hakuna matokeo katika Akili. Matokeo pekee katika Akili ni utendaji au ushahidi, na hii imekuwa kutoka milele, kamilifu, ambayo haijaguzwa na imani yoyote au kukatizwa; uhai wote ukiwa kuakisi, ni kama ilivyo, na sio kwa hisia.

Wakati unapoelewa ya kwamba Akili moja na pekee, basi lazima ukubali ya kwamba kila kitu katika dunia yako yaja kama ufahamu. Kama hautageuka kutoka akili, kanuni, kuzingatia athari, utapata tajiriba kama athari kile ambacho pekee ni kweli, kizuri na charidhisha. Kama “ yote ni akili,” ni nini ambacho utageukia na ni wapi utakapogeukia? Kama “ yote ni Akili,” Akili ile haiwezi kuwa na ufahamu mwingine ila wake mwenyewe kama ushahidi.

Kutoka kwa Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko, 1910 na Mary Baker Eddy, ukurasa 463

Kuamua haraka kuhusu matibabu sahihi ya makosa -kama makosa yanaonekana aina ya magonjwa, dhambi au kifo ndio hatua ya kwanza ya kuangamiza makosa. Bwana wetu alitibu makosa kupitia Akili. Hakushikanisha utiifu kwa sheria za ulimwengu, kama kwa haya inamaanisha sheria za maada, wala hakutumia dawa, Kuna sheria ya Mungu ambayo inatumika kwa kuponya na ni sheria ya kiroho badala ya maada.

Kutoka kwa Umoja wa wema, na Mary Baker Eddy, ukurasa 57

Wakati Yesu aligeuka na kusema, “Nani ameniguza?’’ lazima alisikia ushawishi wa wazo la mwanamke yule; kwa sababu imeandikwa ya kwamba alihisi kwamba “wema ulitoka ndani mwake.” Ufahamu wake safi ulichagua, na kutoa hukumu hii isiyo kuwa na makosa; lakini hakushikilia makosa yake kwa karibu wala kwa udhaifu, kwa kuwa iligunduliwa na kufutiliwa.

Kutoka kwa Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko, 1910 na Mary Baker Eddy, ukurasa 430

Mgonjwa anasikia akiwa mgonjwa, anafikiria kwa kina, na kesi inaanza. Baraza la mahakama la hisia ilikubali mara moja juu ya hukumu, na ilisikika kwa hadhara kubwa – chumba cha roho mlio, hana hatia. Alafu mfungwa akasimama akiwa na nguvu, na huru.

Kutoka kwa Masomo ya Mungu na mkusanyiko wa ujumla. { “Kitabu cha samawati”}, na Mary Baker Eddy, ukurasa 199

Mvuto wa Kinyama, nakubali madai yako, lakini nakata nguvu zako. Wakati makosa yanaongea, hakuna kitu kinachosemwa. Wacha kujihalalisha katika makosa.