Maombi ya jioni
Kutoka Kukesha, maombi, na majadiliano Iliyoandikwa Na Mary Baker Eddy
Kabla ya kufunga macho yako ndiyo ulale, kuwa na uhakika haujashikilia kitu chochote kisicho cha kupendeza katika ufahamu wako, kitu chochote tofauti na Mungu; ukiweka kando hofu yote, jiweke kabisa katika ulinzi wake. Jitulize na wazo ya kwamba yeye aliye na uwezo wote atakulinda, atakupa afya na chochote unachohitaji kwa wingi, na ujue ya kwamba iwe umelala ama umeamka, uko salama, kwasababu maisha yako yamefichwa pamoja na Kristo ndani ya Mungu. Kutangaza kwamba wewe ni mzima, ni ukweli kamili; wewe sio wa kimwili, mbali ni mionzi ya mwangaza wa Kimungu ambao, ukiangaza juu ya mwili, unafanya uonekane hai. Wewe ni wa kiroho na hauwezi kuwa mgonjwa.
Kumbuka kwamba uweza unatumika kwa kusema ukweli tu. Ukweli wote ni neno la Mungu. Uthibitishe kila wakati, hata kama ijulikanayo kama akili yako ya kibinadamu inapiga kelele ikisema ni uongo. Ni kumhimiza,kufanya mawazo yako kumwangazia, kufaidika moja kwa moja na kazi ya wema.