Matibabu kwa kila siku |

Matibabu kwa kila siku


  1. Kila wakati unapotangaza kuwa uko kamili katika Mungu, hupitia mwilini nguvu inayoleta afya. Ukigundua ukweli huu wa ukweli, ya kwamba umekamilika sasa, sio utakamilika katika Mungu, bila tashwishi yoyote, mambo ya ajabu yatakujapita. Lakini niache nikushawishi, hata iwe ngumu namna gani, kutangaza nyakati bila idadi, ya kwamba umekamilika, uko na furaha, uko na ushindi na umekamilika.
  2. Sema mara nyingi: Mungu ni nguvu zangu. Mungu ni uhai wangu. Mungu ni afya yangu na ufahamu wangu.
  3. Ndani mwake uko na mamlaka juu ya dunia, mwili na shetani, mamlaka ambayo ina nguvu zote – maisha yako, yako ndani mwake. Hakuna nguvu inayoweza kukufunga. Mungu ndio uhai pekee, roho ndio dutu pekee, upendo ndio sababisho pekee, uwiano ndio sheria pekee, sasa ndio wakati pekee.
  4. Hii ndio nyumba ya Mungu ya kiroho; hakuna kitu ambacho kinachoweza kuingia ili kukasirisha au kuangamiza , kudhihirisha dhambi, ugonjwa au kukata tamaa; kwa sababu Mungu amejaza hii nyumba na upendo na amani kamili, na anatawala kila mshirika.
  5. Hakuwezi kuwa na nguvu ya nafsi, upinzani wala uovu wa kinyama wa kuleta giza katika mazingara ya nyumbani yoyote, kwa kuwa Mungu kwa kweli huishi duniani na anatawala kila tukio.
  6. Hakuna hali ya uovu wa mawazo ambao unaweza kugombana au shauri au kutengeneza sheria yoyote ya kunitawala, au kunitisha au kunivunja au kufanya uovu wowote uje kwangu, au kuzuia wema wowote usije kwa ufahamu wangu.
  7. Hakuna sheria ya kutofaulu, hakuna hitaji , hakuna umasikini, ukosefu au ukomo.
  8. Hakuna sheria ila sheria ya Kimungu , ambayo ni wingi, uwiano na mamlaka. Hakuna akili za kibinadamu , au mifumo ya akili, nzuri, mbaya au isiyo na maana, binafsi , jumla au kiulimwengu ambayo inawezakuniguza ama mtu yeyote aliye katika duara la mawazo yangu leo, kwa sababu Mungu, wema ananitawala na kila mmoja katika nyumba yangu kwa upendo kamili.
  9. Mpendwa Baba – Mama, nipatie hekima hii ya kukutana na matatizo yatakayotokea leo, nipatie ufahamu wa kukataa upotofu. Nipatie neema ya kukaa kimya wakati sio muhimu kuongea.
  10. Ee, upendo nipe nafasi, nipe Nafsi moja, ufahamu mmoja; na uniwezeshe kumpenda jirani yangu kama ninavyojipenda. Wakati ninapositisha kuhukumu, kukosoa au kulaani, ninaanza kupata maendeleo.