Mkate na Kikombe cha Sayansi ya Kikristo |

Mkate na Kikombe cha Sayansi ya Kikristo

KUTOKA KWA Kozi ya Dini na mkusanyiko wa Jumla {KITABU CHA SAMAWATI}

Na MARY BAKER EDDY


Ushirika unaweza kuja kwa njia ya kuzaliwa upya pekee, kwa ubatizo wa Roho, kama inavyofundishwa kupitia Sayansi ya Kikristo. Huu ubatizo wa moto huleta manukato ya kweli ya Uungu, ikiimarisha uwepo wa Mungu uliowekwa ndani ya mwanadamu kwa kuponya wagonjwa kwa njia ya wokovu kutoka kwa dhambi na kuwa na ushindi juu ya hisia za ufahamu ulio kufa na kuzikwa, na kufichua mfariji anaye ongoza kwenye amani. Hii ndio kukula mkate. Ni nini mkate wa Sayansi ya Kikristo? Ni nguvu na lishe ambayo Mungu hupatia moyo uliodhoofika na hatua zilizoteleza, kwa masaa mabaya ya udhaifu wa kibinadamu; ndio! Hio nguvu anayopatiana , ambayo tunapata utambuzi wake – utambuzi ambao haupatikani kwa maarifa, lakini kwa moyo ulionyenyekea. Ni nini kikombe cha Sayansi ya Kikristo? Ni kikombe ambacho hunywewa katika dhiki. Ni furaha kubwa, baada ya kushinda majaribu. Ni tunda la mzabibu ambao Baba ndiye mkulima. Ni shinikizo la divai ambao mbegu za dhambi lazima zivunjwe, na ambayo nyayo zilizochoka haziwezi ondoka mpaka kila mbegu imevunjwa – na kutoka kwa kiini hiki Mungu ataunda kiumbe kipya, ambacho kitatoa ushuhuda juu yake kama upendo unao ponya. Tunahimizwa kama washiriki wa kanisa hili, kushiriki katika sakramenti iliyo tulia, kuja kwa hii meza aliyo tayarisha kwa shukurani. Kwetu kumenenwa amri, “Mtoto wangu, nipatie moyo wako;” kama ni yetu kujibu.

Nikague ewe Mungu, na ujue moyo wangu;

Nijaribu na ujue mawazo yangu;

Na uangalie kama kuna njia mbaya ndani yangu,

Tumeitwa kujipatiana kila siku, kila saa juu ya madhabahu ya kujitoa sadaka, ya kumtegemea Mungu kabisa, kupata utukufu kwa kila majaribu mabaya, kufurahi kwa kila unyweo wa kikombe kile ambayo inatufanya wahusika na Yesu katika mateso na ushindi wake. Hii nguvu tunapata kwa kiwango sawa kama tunavyo karibisha hisia ya Roho iliyomuimarisha, na tunakuja kwa ukamilifu wa udhihirisho kwa kuwa tuko na Akili ile ile ambayo ilikuwa ndani ya Kristo Yesu.