Mwanzi na Kusudi |

Mwanzi na Kusudi

Kutoka Kwa mkusanyiko wa maandishi Iliyoandikwa Na Mary Baker Eddy


Wanafunzu wapendwa – Kwa kushukuru kwa zawadi ya mwanzi mzuri uliochangiwa kwa Pleasant View Concord, New Hampshire, sioni tofauti kati ya wanafunzi wangu na wanafunzi wenyu; kwa kuwa hapa yenyu inakuwa yangu kupitia shukrani na upendo. Kutoka dirisha langu la mnara, nikiangalia tabasamu hii ya Sayansi ya Kikristo, hii zawadi ya kutoka kwa wanafunzi wangu na wanafunzi wao, itaakisi upendo wao, uaminifu na matendo mema.

Suleiman alisema , “Kama maji sura hujibu kwa sura, hivyo basi moyo wa binadamu kwa binadamu.”

Maji ambayo yanapita kwenye mabonde, na ambayo mumevuta kwa njia yake ndio mniite,yamehudumia fikra kwa karne nyingi. Theologia kwa uaminifu huoga kwa maji, utabibu unaitekeleza kimaumbile, hydrologia huishughulikia kwa ile inayojulikana kama sayansi, na metafizikia inatumia kwa njia ya maudhui kama aina na kivuli. Kimetafizikia, ubatizo hutumika kukemea hisia na kuelezea Sayansi ya Kikristo.

Kwanza: Ubatizo wa toba hakika ni ufahamu wa binadamu ulioadhihirika, ambapo binadamu hupata maoni makali kuhusu wao wenyewe; hali ya akili ambayo inararua pazia inayoficha kasoro za akili. Machozi yanajaa machoni, shida na mapambano,kiburi kinaasi,na binadamu anakaa kama mnyama, giza, wingu la uovu lisilopenyeka; na kuanguka kwa magoti iliyoinama kwa maombi, aliyenyenyekea mbele za Mungu, analia, “Niokoe , au niamgamie.” Hivyo Ukweli, ukipekua roho, humaliza nguvu na kuangamiza uovu.

Kipindi hiki cha kiakili wakati mwingine ni sugu, lakini mara nyingi kali. Inasindikizwa kote na shaka, matumaini, huzuni, furaha, kushindwa, na ushindi. Wakati pambano nzuri linafanywa, uovu unasalimisha silaha yake na unakumbatia miguu ya upendo, kama amani yenye mabawa meupe inaimbia moyo wimbo wa malaika.

Pili Ubatizo wa roho mtakatifu ni roho wa Ukweli akiosha kutoka dhambi zote; akiwapa wanadamu nia mpya, kusudi mpya, mapenzi mapya, yote yakilenga juu. Hali hii ya kiakili inasimama kuwa nguvu, uhuru, imani yenye sauti nzito katika Mungu; na potezo lililoashiria katika maovu, katika hekima ya kibinadamu, sera ya kibinadamu, njia na hatua. Inasitawi uwezo binafsi, inaongeza shughuli za kiakili, na kwa hivyo inaharakisha hisia za maadili ya kwamba madai makubwa ya hisia za kiroho yanatambuliwa , na inakemea hisia za kimwili, ikishikilia kwa nguvu juu ya ufahamu wa binadamu.

Kwa kusafisha mawazo ya binadamu,hali hii ya akili hupenyeza na ongezeko la uwiano kwa hata madogo ya masuala ya binadamu. Inaleta pamoja mtazamo mzuri, hekima, na nguvu; inatoa ubinafsi katika kusudi la mwanadamu, inampa udhabiti wa kudumu, na mafanikio katika juhudi. Kupitia kuinuka kwa kiroho, Mungu,kanuni ya Kimungu ya Sayansi ya Kikristo, kimsimgi hutawala malengo, matamanio na vitendo vya Mwanasayansi. Uamuzi wa Kimungu unatoa busara na nguvu; Unafukuza milele wivu wote, ushindani, kufikiri maovu, kuongea maovu na kutenda; na akili za kimwili, basi zinapoodolewa, zinapata amani na nguvu nje ya nafsi yake.

Hii Sayansi ya Ukristo yenye vitendo ni Akili ya Kimungu, Ukweli na Upendo usiokuwa na mwili, uking’aa kupitia mvua ya ukungu wa kimwili na ikiyeyusha vivuli vinavyoitwa dhambi, magonjwa na kifo.

Katika tajiriba ya kimwili, moto wa toba kwanza hutenganisha taka kutoka kwa dhahabu, na mabadiliko huleta mwangaza unao ondoa giza. Hivyo utendaji wa roho wa kweli na upendo kwa mawazo ya binadamu, kwa maneno ya mtume Yohana, ” Nitachukua yangu na nitawaonyesha.”

Tatu Ubatizo wa roho au uzamisho wa ufahamu wa binadamu katika bahari isiyo na mwisho ya upendo, ndio kipande cha mwisho katika hisia za kimwili. Hiki kitendo chenye nguvu zote kinashusha pazia kwa mtu wa kimwili na kifo. Baada ya haya utambulisho wa binadamu au ufahamu huonyesha roho tu, wema ambao umbaji wake unao onekana hauonekani kwa hisia za kimwili; macho haijaona, kama vile ilivyo kwa mtu asiye na mwili roho – dutu na ufahamu inavyotajwa kwa metafiziki za Ukristo mtu anayefaa – milele amejaa na maisha ya milele, utakatifu, mbinguni. Mpangilio huu wa Sayansi ndio mfuatano wa nyakati, ambao unahifadhi mawasiliano dhahiri, na kuunganisha vipindi kwa kubuni ya Kimungu. Toba ya mwanadamu nakuacha kabisa kwa dhambi inatengua maisha yote ya kimwili au hisia za kimwili na ya kimwili au binadamu wa kimwili anapotea milele. Molekuli ambazo ni mzigo kwa binadamu ambazo zinaitwa mtu, zatoweka kama ndoto, lakini binadamu aliyezaliwa na Mkuu milele, anaendelea kuishi, amewekwa taji na Mungu na amebarikiwa.

Wanadamu ambao katika pwani za wakati wanajifunza Sayansi ya Kikristo,na kuishi kuambatana na yale wamesoma, huchukua usafiri wa haraka hadi mbinguni, – sihiri ambayo imegeuza mbadiliko yote, kiasili, kiraia au kidini, ya zamani yakiwa mtumwa wa mwisho, – kutoka mtiririko hadi kudumu, kutoka chafu hadi safi, kutoka iliyochanganyika mpaka tulivu, kutoka kali hadi kati. Juu ya mawimbi ya Jorodani, kuvuta dhidi ya pwani inayorudi nyuma, imesikia ukaribisho wa Baba na Mama akisema milele kwa wale wamebatizwa na Roho: ” Huyu ni Mwana wangu mpendwa.” Nini ila Sayansi ya Kimungu ambayo inaweza tafsiri maisha ya milele ya mtu, Mungu kwa Wote, na kutoangamizwa kwa kisayansi kwa ulimwengu.

Hatua zinazoendelea za Sayansi ya Kikristo zapatikana kupitia ukuaji, sio kwa kuongezeka; uvivu ndio adui ya maendeleo. Na ukuaji wa kisayansi hauonyeshi udhaifu, hakuna kugandamiza, maono ya undanganyifu, kutokuwepo kiakili, hakuna kuasi dhidi ya sheria zilizoko, hakuna hasara wala ukosefu wa kile kinachounda utu wa kweli.

Ukuaji unatawaliwa na akili; na aliye amilifu,mwenye busara yote, anayeunda sheria, sheria inayorekebisha, kanuni ya utii wa sheria, Mungu. Mkristo Msayantisti halisi huendelea kusisitiza uwiano kwa neno na vitendo, kiakili na kinywa milele akirudia huu mziki wa mbinguni: “Wema ni Mungu wangu, na Mungu ni mwema. Upendo ni Mungu wangu, na Mungu wangu ni Upendo.

Wanafunzi wapendwa , mmeingia kwenye njia. Endelea kwa subira; Mungu ni mwema, na wema ndio zawadi ya wale wamtafutao Mungu kwa bidii. Ukuaji wenu utakuwa wa haraka,mkipenda wema kikamilifu,na kufahamu na kutii mwenye kuonyesha njia , ambaye alipoenda mbele yenu amepanda muinuko mzito wa Sayansi ya Kikristo, na anasimama kwenye mlima wa utakatifu, mahali pa kuishi pa Mungu wetu, na anaoga kwenye kikombe cha ubatizo cha upendo wa milele.

Unapokuwa safarini na wakati unapovuta pumzi kwa mapumziko “kando ya maji tulivu,” tafakari somo hili la upendo. Jifunze kusudi lake; na kwa tumaini na imani, ambapo moyo hupatana na moyo ikirudi imebarikiwa ,kunywa na mimi maji ya uhai wa roho ya kusudi la maisha yangu, – kuhimiza mwanadamu na utambuzi halisi wa kazi ya vitendo ya Sayansi ya Kikristo.